Hongera Dr.Marina Njelekela

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
imepita takribani miaka mitatu kabla ya hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) kufikia uamuzi wa kuteua mkurugenzi mtendaji ambaye kwa sasa atakuwa Dr Marina njelekela.
huyu mama amewahi kuwa mwenyekiti wa chama cha madaktari wanawake Tanzania na anaheshimika kwa mchango wake hasa katika kuhamasisha kampeni ya kugundua kansa ya matiti Tanzania.namuona ni kati ya wanawake wenye mafanikio makubwa hapa Tanzania,ni mwanamke jasiri na mbunifu.namtakia mafanikio mema katika kazi yake mpya pale muhimbili.
HONGERA MAMA MEWATA!!!!
 
tanzania tunahitaji watu kama njelekela,mtu anayeweza kuendesha kampeni kwa kushirikisha wadau wa ndani ya nchi
 
tanzania tunahitaji watu kama njelekela,mtu anayeweza kuendesha kampeni kwa kushirikisha wadau wa ndani ya nchi

Umenena mkuu, twahitaji watu Kama huyu mama, tatizo serikali ya magamba kuwaambia wasiombe misaada through media kwa ajili ya uchunguzi
saratani za matiti wanaona wanaaibika sasa naona MEWATA itakufa
 
Hongera sana Marina kwa kupata hii promotion kubwa sana ambayo imetokana na utendaji wako mzuri wa kazi na umakini mkubwa uliokuwa nao. Nakutakia kila la heri na baraka katika nafasi yako mpya hapo Muhimbili.
 
kwa kweli hapo muhimbili imeumia, huyo mama hawezi kuendesha taasisi kubwa kama hiyo. nimemfahamu kama mkuu wa department, ni mtu ambae anaongoza kwa hisia na ni rahisi kuwa distracted. labda tumpe muda tuone.
 
Mimi nampongeza nafasi aliyopewa nakumbuka alikuwa mwalimu wangu wa physiology pale muhas, na pia nimfahamu coz alikuwa mkti wa MEWATA kwa kweli aljitahidi kuhalalisha watu na kweli walihamasika. Lakin naomba niungane na ndugu yangu Kwetu Iringa, kwamba kwa taasis kama MNH ipo complex sana na inawatu mahiri ambao wanamfahamu Dr Marina in and out na mpaka katoka kapitia njia zipi watu wanajua. Pia tutambue kuwa kuendesha taasis zinazovuta hisia za watu kama MEWATA ni tofauti na MNH. Prof Lema mwenyewe alifanikiwa coz ya kutumia ubabe kidogo, mwulize Dr Lipyoga alopokaimu hadi panya walianza kuhamia thietre. Kwa hiyo akitaka aendeshe kwa hisia kama Mewata anaweza akashindwa any way tumwombee afanikiwe. Time will tell. Good luck Dr Njelekela
 
ni wakati wa huyu binti kuonyesha kwamba kweli alistahili kupewa ile tuzo kule merekani.
 
sina hakika kama kuhamasisha kampeni ni sawa na kuongoza taasisi.lakini tumtakie mafanikio mema katika kazi yake mpya.
 
Njelekela ni mtu mwenye jazba na wakati mwingine hutumia hisia zaidi kuliko busara, clinician wengi huwa hawapendi kuongozwa na watu wa basic science najua kutakuwa na mvutano mkubwa kiutendaji lakini nakutakia mafanikio mama!!!!
 
Hongera mama, umewasaidia kina mama wengi walau sasa kansa ya matiti imetambulika hata vijijini japo msaada wa matibabu na diagnosis bado ni issue. Ungeweza kujenga hosp ya kansa za wanawake tu ungekua mchango mkubwa zaidi kwa taifa. Usikatishwe tamaa na negativity, go for it! Make me proud!
 
hongera dadangu

naomba uondoe wale vitimoto kule nyuma, komaa na barabara za ndani na pia punguza ile migubeli mule ndani haina kitu zaidi ya kubwabwaja tu
 
Back
Top Bottom