Hongera CHADEMA, Tumekubali mmeshinda! Timizeni AHADI zenu!

Mkichagua CCM huduma zitakuja haraka; mkichagua mpinzania tutacheleweshachelewesha!!

Na kinyume chake ni kweli, wakichagua upinzani maendeleo yanaonekana wakichagua CCM mbunge anakuwa likizo na maendeleo yanaenda likizo nani anaweza kuyasimamia wakati yeye muda mwingi yupo busy Dar na vimada
 
Nnauye umeonesha ukomavu but you are running short of something. Japo CDM wameshinda chaguzi hizi kama wawakilishi wa wananchi nina imani watakuwa sauti ya wananchi na wataipaza sana na kwa nguvu zao zote. Kwa kuwa chaguzi hizi haziwapatii CDM authority ya kukusanya kodi na kuitumia ni dhahiri kuwa the burden of proof kuhusu ubora wa maisha ya watanzania popote walipo bila ya kujali wanawakilishwa na chama gani cha siasa yapo kwenye chama chenye dhamana ya kukusanya kodi ya wananchi na kuitumia kwa manufaa ya wananchi wote (CCM).

Ulichotakiuwa kuongezea Ndugu Nnauye ni kusema 'kwa kuwa chama chako cha CCM ndicho kinaunda serikali yenye dhamana ya kutoza watanzania kodi na kuitumia kwa manufaa yao kitafanya kazi kwa karibu na wawakilishi wote wa wananchi bila kujali wanatoka vyama gani kwa faida ya Taifa na wananchi kwa ujumla', kukaa kimya kuna maana kuwa CCM inakubaliana na matamshi ya waziri Nagu kuwa wakichagua wapinzani watahujumiwa kwa kucheleweshewa maendeleo na serikali ya CCM. Huko ni kuvunja katiba na kiapo kuwa Rais ataitumikia nchi na watu wote bila kujali itikadi zao.

CCM itakuwa salama kama ndani ya utawala wake wananchi watapata maendeleo bila ya kujali walimchagua nani kuwa mwakilishi wao. Mkihujumu majimbo yanayowakilishwa na vyama vingine mtakuwa mmeihujumu Tanzania as a country na hamtakuwa na Legitimacy ya kuongoza baada ya 2015.
 
Ndg.Nape,

Sisi sio watani zenu,tunawachana kweli kweli msije mkasema ilikuwa utani. Huwa hatuna utani na CCM.tunawapinga na kuwakosoa kweli kweli

Mie bado sijaelewa anaposema nyie ni watani wao. Huu utani umeanza lini? Maana huko nyuma alikuwa wanawaita Chandimu mara ghafla bin vuu sasa mmekuwa watani. Kawapandisha daraja kutoka Chandimu mpaka watani kwa uchaguzi mmoja tuu?
 
hahahaaaaa baada ya sungura kuruka weweweeeeeee baadae akasema sizitaki mbichi hizi
 
C.c.m cant compete with C.d.m,the only way c.c.m can compete is cheating!bravo c.d.m
 
Mkuu ndio haswa Nape Nnauye umjuae. Na kayasema haya kwa hakika. Uzuri ni maandishi so yatasimama daima. HOJA HAPA NI JUU YA AINA YA UWAKILISHI SI UNAJUA HUYU NI KATIBU MUENEZI? Je kasema haya kama Nape as Nape or Nape as Party Secretary? Na jee hii ndio taarifa rasmi ya chama? NAPE NNAUYE HEBU TUFAFANULIE JUU YA UTATA HUU.
Nina uhakika wa 100% hujamsoma na kumuelewa vyema Mwita Maranya.......rudi kwenye post yake na umsome vyema ndio utamuelewa.
 
We Nape wewe!! hivi niwapi ambapo unaweza ukaifanyia marekebisho ccm? Kama ni kitambaa, chote kimeliwa na mchwa, utaweka wapi kiraka? Mbona ulizunguka nchi nzima kupiga kelele za magamba, kelele zako zimeleta tija gani?
 
RIP CCM. Kama kwenye chaguzi ndogo ulikuwa unashinda 80 - 90% na sasa unaanza kuambulia 40% basi ujue kifo kimekukaribia. Hakika ccm itakufa, maana hamna njia ya kijitibu na kujiponyesha ugonjwa wenu.
Aisee hujui hesabu. CCM imepata asilimia 50(50%) katika chaguzi ndogo wa diwani 8 CCM imeshinda kata 4, CDM kata 3 sawa na 37.5% na CUF kata 1 sawa na 12.5%. kwa tathmini CCM imeshindana na wagombea zaidi ya 3.
 
A photo can speak thousands language!!.....
[h=6]Nape Nnauye
[/h][h=6]Hongereni watani (Chadema) kwa ushindi Arumeru Mashariki. Ninawapongeza mmeshinda! Ndio kauli ya wana Arumeru Mashariki nasi tunaiheshimu! Fanyeni kazi kutimiza mliyowaahidi wapiga kura. Kila lakheri!![/h]

Hahahahaha! Vita ya wenyewe kwa wenyewe!
 
hujafurahi CHADEMA kushinda
umefurahi LOWASSA kushindwa......

i know you are happy leo.....
Hahahaha Umeniwai Inawezekana hata JK mwenyewe anachekelea.

Hiyo heading lol wacheni longolongo ahadi za CCM huwa zinatimizwa?????
Mbunge wangu kwa tiketi ya CCM aliahidi maji, barabara nk nk mpaka leo hakuna maji wala barabara na sijawahi kumsikia anaongea Bungeni na sijui amejificha wapi?

FL umemaliza hapo sema Nape kaandika KISIASA zaidi . Inawezekana hata hayo maadishi sio yake ni draft ya kwenye archive ya kuuai kushindwa kachukua na kuedit neno arumeru kutoka kwenye USB
 
Mie bado sijaelewa anaposema nyie ni watani wao. Huu utani ulianza lini? Maana huku nyuma alikuwa wanawaita Chandimu mara ghafla sasa watani. Kawapandisha daraja kutoka Chandimu mpaka watani kwa uchaguzi mmoja tuu?

Actually he's trying to paint a scenario that doesn't Exist ! CCM kweli hizi bakora chache hivi zimewarudisha kwenye line? na bado watakiona cha mtema kuni.............!
 
Nina uhakika wa 100% hujamsoma na kumuelewa vyema Mwita Maranya.......rudi kwenye post yake na umsome vyema ndio utamuelewa.

Nimemuelewa, post yake ni muendelezo wa post yangu kwa Nape. Anyway si mbaya!
 
Back
Top Bottom