Hongera CHADEMA, Tumekubali mmeshinda! Timizeni AHADI zenu!

Hapa ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine; mjadala wa siasa huwa haufungwi au ndio unatufunga midomo; mbona JK alishawahi kusema kuwa "MWISHO WA UCHAGUZI MMOJA UNAANDA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MWINGINE" MAANAKE SIASA ZINAENDELEA
 
Sasa hivi Nape watu wengi wameelimika japo elimu zenyewe ndo hz za kuunga unga kwa miaka 50 sasa!! badilikeni jamani kwani mnaojaribu kuwadanganya leo si wale baba zetu wa RTD wala si akina siye tuliokuwa tunakubali kwa kuwaheshimu wazazi wetu kwa sasabu tu walikuwa huko huko ulipo wewe, hawa wa leo ni watoto wetu. Hawataki kusika story, wao wanataka kuona reality!

Ebu jamani acheni bla bla mwambie huyo rafiki ya babako kuwa Mzee Mnauye angefufuka leo angemshauri kivingine kwa sababu hii ni Generation nyingine kabisa.
 
Nape ... where are you going to try your luck come 2015 .... don't ever dare to knock at Ubungo constituency ..... advice you to check out somewhere in Dodoma or Mtwara and Lindi .... all other remaining constituencies are too hot to chew
 
Mkuu Nape hongera kwa taarifa nzuri yenye mantiki. Katika siku zote za utendaji kazi wako kama Katibu muenezi leo (ktk hii post) umeonyesha ukomavu, nimeipenda. JIANDAENI 2015 ITAKUWA NI TSUNAMI, VIJANA TUMEJIPANGA POA!

Hizi salam za pongezi siwezi kuziamini hadi nipate uthibitisho kwamba aliyezitoa ni Nape Moses Nnauye.

Bado tunayo kumbukumbu ya uchaguzi wa Igunga, alipost matokeo hapa, kadri walivyokuwa wamechakachua na kabla hayajatangazwa na mkurugenzi kwa mujibu wa sheria.

Alipobanwa athibitishe alikoyapata matokeo akakimbilia kwenye vyombo vingine vya habari kukanusha kwamba siye na hana user ID hapa JF. Kama anataka taarifa zake tuanze kuziamini, ni lazima afanye kama walivyofanya Zitto na Mwigulu(kwa kutaja wachache) wame verify user ID zao.

Short of that, tutaendelea kuchukulia taarifa zinazotolewa kupitia hii ID kama si za Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ccm.
 
hongereni kwa kushindwa.
Huu uchaguzi ulikuwa wa muhimu sana kwa ccm kutambua uelekeo wa wananchi.
Na aliyedhani ana nguvu sana, imebainika ana nguvu sana ndani ya chama lakini kwa wananchi si kitu.

Hatuchagui chama, tunachagua mwakilishi.

Hii itasawasaidia kujithathmini kwa ajili ya 2015.
Hizo karata zenu mzipange kwa ustadi, kuna point mambo hayachakachuliki kabisa.
 
Chama Cha Mapinduzi, kimeyapokea matokeo ya kura zilizopigwa na kutangazwa na tume ya Taifa ya uchaguzi kwa chaguzi ndogo zote, ule wa Arumeru Mashariki na zile za kata nane zilizofanyika jana nchini kwenye maeneo husika.

Kwa heshima nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa dhati
watani zetu, CHADEMA kwa ushindi walioupata Arumeru Mashariki na kwenye kata tatu(Kirumba, Kiwira na Lizabon). ....
Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

Kwa picha hiyo ya kuona uchaguzi hu katika neno lenye rangi nyekundu kambi hizi mbili Wagalu na wagika sasa zitawafaha CDM na CCM.

Hakika tunakwokwenda kwa sasa CCM ningewashauri sana KUIGA MFANO WA NGOMA MBILI MAALUFU SANA KWENYE MIKOA YA KANDA YA ZIWA [Mwanza,Shinyanga na Tabora] maalufu kwa jina la BAGIKA NA BAGALU.

Kwa watu wa makabila ya wasukuma, wanyamwezi na wasumbwa wanazijua ngoma hizo ambazo zina asili moja nzuri sana inayoleta msisimko kwa wapenzi na washriki wake kwa uchezaji wake,mbinu na mikakati yote yenye kila dalili za kuleta ushindani kati ya ngoma hizo mbili yani Bagika na Bagalu.

Dunia uendeshwa na uvumbuzi wa nadhalia [theory] ambazo zimetokana na matendo tofauti tofauti kama vile jinsi wadudu kama siafu [Kwa lugha ya Wasukuma na Wanyamwezi maalufu kama sungusungu] wanavyofanya kazi,utaratibu wake ule umeweza kutumika na binadamu kujipatia maendeleo kwa kufuata mtililiko mzima wa kazi husika unavyofanywa na siafu hao.Vivyo hivyo kuna mifumo kama matumizi ya conveyer belt nayo yametengeneza mfumo wa kufanya kazi na kugeuka kuwa kanuni ya binadamu kuitumia kama njia yake ya kumuongoza kufanya kazi kimaamuzi ya kikanuni.Ilikuwa ni kwa mfano wa siafu [sungusungu] ndipo wazee wajadi wa makabila ya Wasukuma,Wanyamweiz na Wasumbwa waliibuni jeshi la ulinzi la kienyeji lenye sura na muonekano wa kimatendo kama siafu [sungusungu-au maalufu kwa lugha ya vijana mikoa hiyo Wasalangata].

Nimetafakari sana kuwa tunakokwenda CCM kama chama kikongwe watake wasitake hawana budi kujifunza kwa kuangalia wazee wa makabila ya Wasukuma,Wanyamwezi na Wasumbwa wanavyoweza kuwa na ngoma hizo maalufu kwa makabila hayo zinavyochezwa na kuwa kama simba na yanga kwenye soka huku wachezaji hao wakiwa na urafiki na maelewano bilal kujali tofauti na itikadi zao za mapenzi ya ngoma zao husika.

CCM na dhama hizi za siasa zinazoangukia ushindani na chama kikuu cha upinzania cha CDM ambacho kinaonekana kuwavuta vijana, yawabidi kutafuta njia bora za kukubalika kucheza ngoma ya Bagika na Bagalu watake wasitake [Kwa Wasukuma wanajua watu maalufu katika makundi hayo ambao ni SAWAKA MWANAGANDILA NA TAGALA].Hawa watu wawili Sawaka na Tagala walipokuwa wanakuta hakika utapenda kuona michuano ya hali ya juu,ufundi,maarifa na buradani kali kali zenye kusisimua.Hatimae ya yote mwisho wa ngoma kati ya watu hawa wawili Swaka na Tagala lazima mmoja awe mshindi kama ni ngombe kumi au gari atachukua yeye na team yake.

Vivyo hivyo CCM, wanapaswa kutambua kuwa ile ngoma waliokuwa wanatawala na kuicheza kwa mdundo wanaotaka wao, kwa maarifa, mbinu,mizengwe na changamoto kadha wa kadha ambazo walizijua wao pekee yao sasa hawazichezi pekee yao na kuwa NGOMA IMEPATA MCHEZAJI WA PILI wamepata MPINZANI wa dhati tena mwenye nguvu ya vijana wenye damu zinazochemka vibaya sana na mfano wake ni Arumeru Kaskazini na wako tayari kuicheza ngoma hiyo kwa masafa malefu.

Kwa lugha nyingine yaweza kuwa Sawaka ni CCM na Tagala ni CDM,kwa wenyeji wa Mwanza,Shinyanga na Tabora wanajua shughuri ya watu hawa walipokuwa wakikutana.Hawa ni Team mbili tu yani mmoja ni Mgika na mwingine ni Mgalu. Vituko, miujiza, uchezaji, udanganyifu,mizengwe,uchakachuaji,na mengineyo yote kuwavuta watazamaji kujaa kwenye ngoma moja na kuacha nyingine ni ubunifu wa hali ya juu sana unatafutwa na kuchezwa na timu hizi mbili za ngoma.

Cha msingi CCM wanapaswa kutambua sasa kuwa CDM sio watoto tena hata kama wao ndio waliofungua milango ya vyama vya siasa na kuwa wao ndio wamekuza na kulea siasa za vyama vingi na diplomasia ya maneno mengi, leo hii mtoto wa demokrasia anakaribia kugraduate hivyo hawana budi kujiandaa kuishi nae kama mtu mzima mwenzao mwenye ufahamu mkubwa wa mazingira na nyakati zijazo kuliko mzazi.

Hivyo kwa CCM kuiga mfumo wa ngoma za jadi za Wasukuma na Wanyamwezi watapata jawabu la kuona ni jinsi gani wataendana na ngoma [Tanzania] huku wakishindani kushinda ngoma hiyo wakiwa na mpinzani wake CDM.Ubabe mizengwe na ujanja ujanja wa KICCM sasa umekwisha umebeki ujanja na maarifa ya kuwakamata Umma na hasa vijan wa kizazi kipya wakubali kutoa support na kuwapa imani kuwa wao ni zaidi ya CDM,na wakati huo CDM nao wakipambana kuonyesha wao ni zaidi ya CCM.
 
Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao.


Umekubalina na nguvu ya umma ?
Niiledhana ya ccmitatawala daima je?

Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

Nyie mmetekeleza yale yote mlio ahidi?

Waacheni watumie muda kujenge chama kwanza
 
Ni vzuri umekuja mwenyewe hapa.

Mnashíndwa kutokana na dharau zenu kwa watanzania. Mnawaadanya watu kwa ahadi za uongo,mnakitetea chama kilicho na harufu mbaya rushwa.

Hii ni trailer movie inakuja 2015 kwa sababu hamsikii endeleni na kauli za kishamba ''ccm itatawala milelé'' ushindi lazima etc.
 
Matokeo ya kura hizi kwa ujumla yameonyesha sauti ya wapiga kura kwenye maeneo husika, ndo maana tunaheshimu maamuzi yao. Tunatoa wito kwa vyama vilivyoshinda kwenye maeneo hayo kuhakikisha vinatumia muda na dhamana waliyopewa kutekeleza yale waliyowaahidi wapiga kura wao.

CCM tutatumia matokeo haya kufanya tathimini ya kina na kuangalia wapi tuliteleza ili tufanye marekebisho kuhakikisha makosa hayarudiwi tena. Kimsingi uchaguzi huu umeisha na tufunge mjadala wa uchaguzi tujikite katika kuwaletea maendeleo wale waliotuchagua.

Nawatakieni kila lakheri wote mliochaguliwa, nawatakieni utumishi uliotukakuka!

Hapo ndipo ulipochemka. CCM wameshindwa kwa kushindwa kuwatumikia wananchi

Kwenye REDI. Ni ukweli usiofichika kwamba Uwanja wa Ndege wa Misenye, na Uwanja wa Ndege wa kimataifa Kigoma hamjatekeleza na hakuna namna mnaweza kutekeleza.
Sawa.
 
Ndg.Nape,

Hongera pia kwa kata mlizoshinda.Tunaomba ustaarabu huu wa kukubali kushindwa muendelee nao hadi 2015.Uchaguzi umekwisha tujenge nchi yetu.Ningependa kuwashauri msije mkaingia mtegoni kwa kutafuatana wachawi.Jitahidini kuishinikiza pia serikali yachama chenu kutekeleza ahadi za uchaguzi uliopita wa mwaka 2010.Katika utekelezaji wa ahadi za uchaguzi,CCM ni mfano mbaya kwa vyama vingine na mmekosa moral authority ya kuhimiza vyama vingine katika utekelezaji wa ahadi

vyama vyote vinatakiwa kufanyia kazi mapungfu yaliyojitokezakatika kipindi cha uchaguzi.

Pia natarajia wewe kamakiongozi mwenye dhamana ya kueneza itikadi ya chama chako basi uhakikishe makada wa cahama chenu wanajikita kwenye siasa za hoja kwa kuzingatia itikadi.Isije ikatokea aibu/fedheha nyingine kwa chama chenu kama ilivyotokea Arumeru baada ya makada wenu kuamua kuingia kwenye itikadi ya matusi na majungu.Sisi sio watani zenu,tunawachana kweli kweli msije mkasema ilikuwa utani.Huwa hatuna utani na CCM.tunawapinga na kuwakosoa kweli kweli

Siasa za matusi,mapanga na marungu huchochea chuki kwa wananchi na kusababisha mgawanyiko usio wa lazima ndani ya jamii husika.Nilitegemea ungetumia nafasi hii kukemea siasa(uhalifu) za aina hiyo


Naamini chama chako pia kitakaa chini kuangalia mweleko wa siasa za chama chenu kuelekea 2015 na kubuni mkakati au programu ya kuwaandaa makada na wafuasi wenu kisaikolojia kupokea matokeo ya wimbi hili la mabadiliko .Chama changu kimepewa Ridhaa,kimepewa nafasi na hakitaitumia vibaya.tutaitendea haki dhamana tuliyokabidhiwa,na historia yetu kiutendaji inatutea katika hilo na ndiyo muongozo wetu kimtazamo katika kuwatumikia Wananchi
 
Sijui unaitwa Nape sijui nani. Acha unafiki, haiwezekani sasa unawataka hawa walioshinda watekeleze ahadi zao ambao nini wenyewe (nanukuu Dr. Mary Nagu) mnasema wanawadanganya wananchi na hawawezi kufanya chochote kwa sababu hawaongozi serikali. Katika hali ya ninyi mlioshika serikali kushindwa, asiyeshika atawezaje?? Kwa Meru, madiwani wote ni CCM, ingekuwa wametekeleza chochote - ushindi kwa CCM ungekuwa rahisi.

Acha unafiki na jiandae kukabiliana na upinzani siku zijazo!! CDM sio watani zako, labda CUF!! Naomba tu hiyo tathmini mtayoifanya isihusishe mbinu chafu za wizi wa kura, kutumia nguvu za dola kulazimisha mambo, kupiga na kujeruhi watu. Tathmini yenu ianze na mmeshindwaje kumletea "MAISHA BORA" mpiga kura na iishe "MTAMLETEAJE MAISHA BORA" na kulitekeleza hilo.

Naomba msitufukuzie Lusinde (tunamuhitaji katika mikutano yenu mingine). Tunahitaji kuwahafamu hawa "top brass" wa chama chenu!!! Jinsi wanavofikiri na ukomo wa mawazo yao. Inatusaidia kujua ni kiasi gani nchi inaanguka, ili tuinyanyue.

Kwa taarifa yako,
 
WEWE NAPE,
kwanza sisi sio watani zenu kama watani ni cuf mliowauwa kwa risasi badae mkawatuliza kwa pipi (makamu wa rais zanzibar)

utani wakati mali ya umma imeibiwa na chama chenu?

kama mnataka kurudisha heshima yenu fanyeni yafuatayo.
1.kamateni mafisadi wa epa,meremeta,rada,reli,ttcl,kiwira nk.
2.rudisheni nyumba za serikali.
3.waprudishiewameru ardhi yao.
4.mtimueni mliyempa ardhi ya wanambarali.
5.mnyanganyeni kiongozi wa ccm mliyempa mashamba ya chai lupembe.
6.karudisheni twiga wetu kule qatar.
7.fukuzeni mafisadi wote wanaosababshia nchi yetu umasikini kwenye sekta ya umeme.
8.karudisheni mitambo ya kiwanda cha tail pale dodoma iliyoibiwa na kupelekwa uganda.
9.futeni mikataba yote ya kinyonyaji katika madini yetu.
10. mawaziri wote waliolihujumu taifa kwa mikataba ya kifisadi washtakiwe kwa sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 1981.

baada ya hapo urudi na kutuita watani.
 
Yawezekana kabisa kuwa ccm walilegeza wizi ili kumkomoa ba mkwe na kumvunja kisiasa. Ndio raha yetu. Piganeni na sie tupete
 
Back
Top Bottom