Hongera CHADEMA Singida mjini kwa kutimiza ahadi

MADORO

Senior Member
Nov 12, 2011
198
117
Nimekumbuka kuwa mmoja ya Ahadi za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia CHADEMA ilikuwa ni kulinda Ardhi ya wananchi wa Singida kutoporwa na kampuni ya Kifisadi ya Wind East Africa Ltd, iliyokuwa inasaidiwa kwa nguvu zote na Mkuu wa Mkoa wa singida ndg. Perseko Kone. Kampuni hiyo ilifikia hatua za mwisho za kujimilikisha isivyo halali ardhi ya wananchi masikini. Tunampongeza Josephat Isango kwa kusimama kidete kuhusu suala hilo na kupambana na Mkuu wa Mkoa, mpaka sasa siku hizi Mkuu huyo hawezi hata kufanya mikutano ya hadhara kwa jinsi alivyoumbuka. Sakata hilo sasa limeisha wananchi ardhi yao imelindwa na kweli kijana amepambana. Tunatoa changamoto kwa wagombea wengine wa CHADEMA hata kama walishindwa wajaribu kutekeleza ahadi zao kwa wananchi hasa zile ambazo ziko chini ya uwezo wao. Bravo vijana wa CDM.
 
Hivi MO naye ni Mbunge? Kwako huna hata televisheni? Umewahi kumwona Bungeni? Yule ana dili zake tu, yeye na singida wapi na wapi? huwa anawatumia watu kalenda kila mwaka, yeye anaendelea na misele yake ya biashara. Sijui hata kama alijua kuwa wananchi walikuwa na shida ya kunyang'anywa ardhi. Aibu sana. hongera kijana wa Chadema kaza buti kitaeleweka tu
 
Nimekumbuka kuwa mmoja ya Ahadi za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini kupitia CHADEMA ilikuwa ni kulinda Ardhi ya wananchi wa Singida kutoporwa na kampuni ya Kifisadi ya Wind East Africa Ltd, iliyokuwa inasaidiwa kwa nguvu zote na Mkuu wa Mkoa wa singida ndg. Perseko Kone. Kampuni hiyo ilifikia hatua za mwisho za kujimilikisha isivyo halali ardhi ya wananchi masikini. Tunampongeza Josephat Isango kwa kusimama kidete kuhusu suala hilo na kupambana na Mkuu wa Mkoa, mpaka sasa siku hizi Mkuu huyo hawezi hata kufanya mikutano ya hadhara kwa jinsi alivyoumbuka. Sakata hilo sasa limeisha wananchi ardhi yao imelindwa na kweli kijana amepambana. Tunatoa changamoto kwa wagombea wengine wa CHADEMA hata kama walishindwa wajaribu kutekeleza ahadi zao kwa wananchi hasa zile ambazo ziko chini ya uwezo wao. Bravo vijana wa CDM.

Hivi hiyo kampuni hapo kwenye red si ile ya kina Dr. H. Mwakyembe?
 
Huu ndiyo utashi na upendo wa dhati kwa wananchi, kila moja akiwajibika namna hii tutasonga mbele na tutakuwa na Tanzania tunayoitaka.
Mungu ibariki Tanzania.
 
tatizo la watu wa singida wakiona ngozi nyeupe sijui wanajua ni mungu?

kuna tetesi wanamwandalia riz 1 jimbo la misanga.
 
Hivi MO wanampendea nini jimboni kwake?
Wanampenda kwa wali na nyama ya ng'ombe anazogawa wakati wa kampeni, halafu ng'ombe wenyewe huwa ananunua walikaribia kufa kwa ungonjwa wa malale baada ya kuumwa sana na mbung'o.Si unajua tena pale uswahili umejaa kazi kunywa kahawa tu,,Munio wake mkonongo usuu".
 
Wind East Africa Ltd, ni kampuni iliyopewa leseni DAR ES SALAAM, INASEMEKANA NI YA Lowassa, Rostam, na Dogo mmoja anayetumiwa katika kampuni hiyo anaitwa RASHID SHAMTE, ana kiburi sana cha pesa, aliwahi kumtishia huyo Kjana wa CHADEMA yeye na Mkuu wa Mkoa wa Singida walifunguliwa mashtaka Singida mjini lakini mpaka leo hawajawahi kutiwa hatiani. Jeshi la polisi linazidi kujidhihirisha kuwa ni la Mafisadi. Actually Mwakyembe hahusiki kabisa na Kampuni hiyo iliyo na hisa za Six Telecom, iliyo karibu kabisa na Mafisadi wakuu nchini. Nilisoma detail zao kwa huyo huyo kijana wa CHADEMA wakati anapambana na RC wa Singida, jamaa alienda deep kuwapata data zao ndo maana RC wa Singida ameufyata.
 
Hongera Josephat Isango kwa mapenzi mema kwa ardhi ya baba na mama yako. Wema huishi milele.
 
Back
Top Bottom