Hongera Chadema, Hongera Mch.Peter Msigwa Kwa mwanzo mzuri...

vangiling'ombe

Senior Member
Apr 2, 2012
103
25
Hongera Chadema kwa kuonesha njia ya uadilifu na uzalendo...
Hii ndio Hospitali mpya ya Manispaa ya Iringa ambayo mbunge Msigwa amekabidhi vitanda vya kisasa itaanza kutoa huduma jumatatu wiki ijayo


420652_2585087041049_1670723569_1602890_118557243_n.jpg


MBUNGE wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amekabidhi vitanda vya kisasa 30 pamoja na magodoro yake kwa ajili ya kusaidia kulalia wagonjwa na Baiskeli za walemavu (Wheel chairs) 19 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 50 na kuwapongeza wabunge waliomtangulia akiwemo Monica Mbega (CCM) kwa kazi nzuri.

Akikabidhi msaada huo leo kwa kaimu meya wa Manispaa ya Iringa Victor Mushi wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali mpya ya Manispaa ya Iringa iliyopo eneo la Frelimo mjini hapa ,mbunge Msigwa alisema kuwa amelazimika kutoa msaada huo kama njia ya kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kuboresha huduma za afya.

Hivyo alisema kuwa kwa upande wake ataendelea kufanya mambo ya kimaendeleo zaidi badala ya kutoa fedha za kula kwa mwananchi mmoja mmoja japo ambalo halitasaidia kuharakisha maendeleo ya jimbo hilo la Iringa mjini.

"Kiukweli kama rafiki zangu ninao wengi sana na leo hii nikaamua kugawa fedha shilingi 10,000 kwa kila rafiki yangu kama sehemu ya ahsante kwa kunichagua nitakuwa siwasaidii na njia sahihi ya kuwasaidia rafiki zangu na wapiga kura wangu ni kuwasogezea maendeleo kama hivi....hivi vitanda leo vitatumiwa na wana Chadema, CCM ,CUF ,TLP ,NCCR Mageuzi na wanachama wa vyama vyote na wasio na chama ambapo ni jambo la msingi zaidi kuliko kuwa mbunge wa kugawa fedha za kula...kweli wananchi wangu naomba mnisamehe kama nitawakwaza kwa kufanya shughuli za kimaendeleo"alisisitiza mbunge Msigwa.

Hata hivyo alisema kuwa si kwamba amekuwa akichangia shughuli za kimaendeleo kwa kutumia uwezo na maamuzi yake pekee bali amekuwa akifanya hivyo kwa kuzingatia zaidi mawazo na maagizo ya wananchi waliomchagua kupitia ofisi yake na mikutano mbali mbali ya hadhara aliyopata kuifanya kabla ya baada ya vikao vya bunge na mabaraza ya Halmashauri ya Manispaa.

"Katika mazingira hayo jukumu la mbunge na diwani makini si kuwapoza wananchi kwa kuwapa vijisenti na vizawadi vya kula leo na kumalizika leo ,au kuwadanganya kwamba naweza kuwaletea maendeleo kwa kutumia mshahara wangu wa ubunge ambao sote tunajua kuwa hautoshelezi watu wa jimbo hili ,bali ni kuhudhuria kwenye vikao hivi na kuhakikisha kuwa vinapitisha maamuzi na kutenga fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo yenu ...nashukuru kwa kunielewa kwani wajibu wangu kikatiba ni kuishauri na kuibana serikali kwa manufaa ya maendeleo yetu"

Mbunge Msigwa alisema kuwa mbali ya kukabidhi msaada huo katika Hospitali hiyo ya wilaya ya Iringa mjini kama njia ya kupunguza msongamano katika Hospitali ya mkoa wa Iringa bado amekuwa mbele kuchangia shughuli mbali mbali zikiwemo za michezo na kuona kuwa ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni zinatimizwa kwa wakati ikiwemo ahadi ya kuchangia shilingi milioni 12 kila mwaka kutoka katika familia yake kwa ajili kusaidia watu wenye matatizo .

Akielezea juu ya msaada huo alisema kuwa kila kitanda kimoja kinagharimu zaidi ya shilingi milioni 1.5 wakati baiskeli kila moja ni zaidi ya shilingi 700,000 pamoja na vikabati vya kuhifadhiwa vifaa vya wagonjwa katika mawodi na kuwa msaada huo ameupata kupitia wahisani wake R.T.C.O japo alisema hakupenda sana kutumia kutafuta sifa kwa msaada huo kwa kuweka thamani ya fedha kama ambavyo wanasiasa wengine wanavyofanya.

Pia alitaka wananchi wa jimbo la Iringa mjini mbali ya kusubiri kusaidia na serikali kwa kila jambo bado wanaweza kujitolea kusaidia huduma za afya ,elimu na maendeleo mengine katika maeneo yao na kuwa ofisi yake kuanzia sasa itafanya kazi ya kupokea misaada na michango mbali mbali kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya jimbo la Iringa mjini.

Kwa upande kaimu meya wa Mnaispaa ya Iringa diwani wa kata ya Mtwivila Victor Mushi (CCM) mbali ya kumpongeza mbunge Msigwa kwa msaada huo mkubwa bado alitaka vifaa hivyo kutunzwa zaidi ili kuweza kuendelea kusaidia katika Hospitali hiyo .

Huku kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) alisema kuwa msaada huo utasaidia kupunguza matatizo ya akina mama wajawazito ambao wamekuwa wakipata shida na kuwa tukio hilo la kukabidhi vitendea kazi katika Hospitali hiyo ni tukio la kupongezwa na kuwa katika shughuli za kimaendeleo wanasiasa wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja katika kuharakisha maendeleo badala ya kuingiza mivutano ya kisiasa isiyo na tija katika maendeleo ya wananchi

Huku wananchi wa jimbo la Iringa mjini wakiwemo wana CCM na wanachama wa vyama vya upinzani wamepongeza jitihada za mbunge wao Msigwa kwa msaada huo na kutaka wabunge wa CCM kuiga mfano huo katika kuchangia maendeleo badala ya kutoa takrima kwa wapiga kura.

John Kalinga ni mwana CCM mkazi wa Frelimo amesema kuwa wengi walikuwa wakishindwa kumuelewa mbunge Msigwa ila sasa wamemtambua vema kuwa ni mbunge wa kazi katika jimbo hilo na kuwa jitihada hizo zinaweza kuja kuwa mwiba kwa CCM kulichukua jimbo hilo kutokana na mambo ambayo anayafanya kuwa makubwa zaidi ukilinganisha na yale ya CCM.

Huku Sarah Sanga mwana TLP amepongeza jitihada hizo na kutaka wana CCM kuacha kuelekeza mashambulizi kwa mbunge Msigwa badala ya kuelekeza mashambulizi ya kimaendeleo kwa wananchi .

Viva Chadema, Viva Wa-Tanzania.
 
Asee hii kama ya zamani

Big up msingwa. Enzi za ubishi wa siasa tukiwa kwa mama solemba tunapuga kitu cha ugali kuku zimekufikisha mbali sana.

Big up!
 
Lazima kuonesha tofauti na mbadala wa ccm ktk kila nyanja. Hongera CDM! Hongera wananchi wa Iringa!
 
Outdated material,

ila anyway kwa kuwa hana jipya jimboni basi si vibaya akaileta mara nyingi nyingi, magodoro 30 ya futi 3x6 kila moja sh

50,000/= jumla Sh 1500,000/= kweli tuna kazi tanganyika. we 1.5m anauzia sura kiasi hiki? wakati znz raza

mshahara wake wote wa ubunge anaupeleka jimboni na hakuuza sura.
 
haya ndiyo tunayo hitaji yafanyike nchi nzima na tunatarajia wabunge wote wataiga mfano huu kwa vyama vyote
 
Iko pande zipi manispaa pale? amesaidia maana mji unakua na hakukuwa na hosp mbadala zaidi ya ile ya mkoa
 
:love:Tusiseme msaada jamani ni kazi aliyo chaguliwa kuifanya kwani wanaotoa msaada tuwaweke mahali tofauti na wanaotekeleza majukumu yao kijamii. Natoa pongezi kubwa sana kwa mchungaji kwa kuonyesha hata upinzania wanafanya makubwa wananchi wasidanganywe kuwa wawe wanachagua mafiga mtatu.
Mungu BARIKI WAPENDA MAENDELEO YA TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA.
 
Hongera Jk kwa kutimiza ahadi ya hospital nzuri,hongera msigwa kwa kutimiza ahadi ya vitanda bora!
 
Outdated material,

ila anyway kwa kuwa hana jipya jimboni basi si vibaya akaileta mara nyingi nyingi, magodoro 30 ya futi 3x6 kila moja sh

50,000/= jumla Sh 1500,000/= kweli tuna kazi tanganyika. we 1.5m anauzia sura kiasi hiki? wakati znz raza

mshahara wake wote wa ubunge anaupeleka jimboni na hakuuza sura.

Kama Raza hakuuza sura we umejuaje kama mshahara wake anautoa??acha kufikiri kwa kutumia magamba ya masaburi..ukitumwa uwe makini!!ni heri uagizwe na aliyetoa buku 50 kwa ajili ya kununua sindano box moja!!
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom