Holy Week. Matukio ya Jumanne.

Andrew Nyerere

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
3,007
2,429
Holy Week.
Baada ya jana kuelezea matukio ya Jumatatu,sasa tuendelee na matukio ya Jumanne.
Saa moja asubuhi Yesu aliongea na Mitume wake, pia aliongea na Lazarus kumwambia atoroke kwenda Philadelphia.
Wakati wale Mitume wengine walipokwenda kuitayarisha kambi mpya karibu na bustani ya Gethsemane,Yesu alikwenda matembezi na Mitume wake wanne,Andrew,Peter,James na Phillip.
Kwa siku kadhaa,James na Peter walikuwa wanabishana kuhusu msamaha wa Mungu,na wakaamua watakwenda kwa Yesu awaamue. Kwa hiyo Yesu alipokuwa anaomhea kususu tofauti kati ya kusifu na kuabudu, Peter akamuuliza,''James na mimi tunabishana kuhusu msamaha wa Mungu. James anasema Mungu anasamehe kabla hajaombwa. Mimi nasema,mtu ni lazima atubu na kuungama dhambi zake kabla ya kusamehewa.
Yesu,baada ya kuwa kimya kwa muda mfupi,aliwajibu.''Ninyi hamuelewi kwamba binadamu ni mtoto wa Mungu,na kama mtoto hajakua anaweza kufanya makos . Mungu anaelewa hilo;ingawa mtoto ataelekea kuwa amefanya makosa,Mungu atamsamehe kwa vile anajua moyo wa binadamu;hata kama mtu atajisikia vibaya na kuona kwamba amemkosea Mungu,Mungu hataona wakati wowote kwamba utengano ulitokea,kwa vile Mungu anaelewa na kusamehe.''
Halafu Mafarisayo walikuwa wanajadiliana kumkamata Yesu. Wakaamua kwanza ni lazima wajaribu kumfanya ajikanganye mbele ya watu kabla ya kumkamata. Kwa hiyo wakatuma watu kumuuliza maswali. Wakamuuliza ,''Ni sawa kulipa kodo kwa Kaesari?'
Ndipo Yesu alipowaambia kama sarafu ina picha ya Kaesari,mpe Kaesari sarafu yake.
Masadukayo wakamuuliza kuhusu kaka saba walioamuoa mke mmoja. Baada ya kufa,yule atakuwa mke wa nani?'' Yesu akawaambia kwamba Mbinguni hakuna ndoa.
Halafu akaja mtu kumuuliza amri ipi ni ya kwanza. Yesu akasema,'Mungu ni mmoja. Mpende Mungu kwa nguvu zote ,na moyo wote,na roho yoye,na mpende jirani yako kama unavyojipenda.'' Na yule mtu akajibu,'Kweli,kumpenda Mungu na kumpenda jirani ni muhimu kuliko kutoa dhabihu'' Yesu akamwambia,''Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.'' Na Yesu aliposema hivyo,ilikuwa sawa kabisa,kwa sababu,jioni ile,katika kambi karibu na Gethsemane,yule mtu alibatizwa.
Wakafika Wagiriki kutoka Alexandria kumuona Yesu. Yesu akaongea nao na kusema,mafundisho yake ni kwa Wayahudi,lakini Wayahudi wamekaribia kuyakataa,lakini anafarijika kuona kwamba Gentiles wanayapokea mafundisho. Halafu akawakaribisha wote kwenda Heakaluni kutoa Khutba yake ya mwisho. Kwa mara ya mwisho akawaambia Mafarisayo wajirekebishe,wasimkatae Mwana wa Mungu. Pia akawaambia watu kwamba,''Wafuate wanayosema Mafarisayo,lakiniwasifanye wanayotenda.''
Ingawa Yesu alisema yote haya,lazima ikumbukwe kwamba hii haina maana kwamba ni halali kugombana na Wayahudi; Wayahudi as a group wameteswa kiasi cha kutosha kwa kumkataa Yesu,lakini hakuna sababu ua kugombana na Wayahudi mmoja mmoja,kwa vile Yesu pia alikuwa Myahudi,na Wayahudi wengi walijitolea maisha yao kwa ajili ya hii Dini.
Sanhendrin;yaani,Mafarisayo na Msadukayo wakakutana na kumhukumu kifo Yesu na Lazarus,it was a unanimous decision,wote waliafikiana,muda mfupi kabla ya midnight,Tuesday,April 4,A.D. 30. Wakatoa amri akamatwe na kuletwa mbele yao Jumatano asubuhi,lakini asikamatwe mbele ya watu.
Masadukayo walimpinga Yesu kwa vile walihofu Mafundisho yake yatawagombanisha na Utawala wa Roma.Pia Temple Reforms zake zilikuwa zinawakoseha mapato. Pia Mafundisho yake mapya ya kusema kwamba binadamu wote ni Ndugu Moja,waliona kama vile yanaweza kuleta vurugu za Kijamii.
Mafarisayo hawakupenda jinsi Yesu alivyokuwa anakiuka sheria kama vile kufanya kazi siku ya Sabato,au kujiita Mwana wa Mungu.
Yesu akaondoka na wafuasi wake,na walivyokuwa wanaondoka,wafuasi wake wakawa wanayatazama majengo makubwa waliyayaona pale. Yesu akasema,''Muda utafika ambapo haya majengo yote yatabomolewa.''
Walipokwenda mbele walipumzika kwenye Mlima wa Olives,na Yesu akawaeleza jinsi Jerusalem itakavyshambuliwa na Warumi,baada ya muda mfupi,na kwamba kila mtu itabidi atoroke Mji,na kuisalimisha nafsi yake.
Akawaeleza pia kwamba ataondoka lakini atarudi tena ,lakini kabla hajarudi,atamleta Roho wa Ukweli,kwa kila binadamu.
Waliporudi kambini,Yesu alielezea zaid kwa kuhadithia kuhusu mtu aliyesafiri na kuwapa wafanyakazi wake talanta,mmoja talanta tano,mwingine talanta mbili,mwingine talanta moja,na akawataka wazifanyie kazi.
Aliporudi alibishana na yule aliyeifukia talanta ile moja.
Hivyo,Yesu ametupa mafundisho pamoja na Roho wa Kweli,na inategemewa kwamba wote tutakua katika neema na Ukweli.
Iwapo Yesu atarudi tena,na tutamwambia,''Kweli uliyotukabidhi miaka mia au elfu iliyopita ,hatujapoteza kitu,tumedumisha kila kitu ulichofundisha;hatukukubali mabadiliko yoyote yafanyike katika yale uliyotufindisha;huu hapa Ukweli uliotupa'',tukisema namna hii,haitakubalika kwetu. Huu utakuwa ni uvivu. Kama tumefundishwe Kweli lazima tukue katika kweli.
Mambo ya Jumatano,tutajadili kesho Jumatano.
Siandiki haya kufunga mjadala,ila kuanzisha mjadala. Kwa hiyo naomba maoni ya wengine kuhusu Sikukuu ya Pasaka.

 
Masadukayo walimpinga Yesu kwa vile walihofu Mafundisho yake yatawagombanisha na Utawala wa Roma

watawala lazima watakupinga wakigundua mafundisho yako yatachochea kuondolewa kwap madarakani.
 
Back
Top Bottom