Holstein-Friesian

Discussion in 'Jukwaa La Biashara na Uchumi' started by Doltyne, Oct 21, 2011.

 1. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wadau naomba msaada wa mawazo na ushauri, Nimepitia pitia threads mbali mbali humu na nimehamasika na ufugaji wa ng'ombe wenye uwezo wa kutoa maziwa mengi kwa siku. Nina mpango wa kuanza na ng'ombe kama saba hivi wenye mimba.

  Kama kuna mtu anawafuga hawa Dar, naomba anialike kwake nikafanye site visit kidogo, na nimuulize maswali mawili matatu ya kinadharia kabisa ili niweze kuingia katika ufugaji huu.
  Natarajia kuwafugua Dar es salaam eneo lililo kati ya mbezi luguruni na bunju, almaarufu kama Mpiji Mahohe... Nina Heka 3 za kufanyia mradi huu, je kuna setbacks zozote au kuna challenges gani nijiandae nazo?

  Vipi kuhusu, chakula, maji, na uangalizi wao kwa ujumla.

  Naombeni msaada tafadhali.
  NB: Kama kuna mtu anaushauri zaidi wa namna ya kuwajengea mabanda madhubuti ningependa pia ushauri wake na mengineyo mengi.
  NB2: Nimeshapiga simu kwa mwalimu mmoja wa Kitulo kama alivyoelekeza Malila kwenye moja ya threads zilizopita na akanipa namba ya Muhusika na nimeshaweka booking ya kuwapata mwezi wa pili mwakani... Kama kuna mtu anajua shamba jingine naweza kuwapata kabla ya hapo ntafurahi pia akinihabarisha.

  Shukran sana.
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Umeanza vizuri sana,
  Ushauri wangu wa bure ni huu, nenda Ruvu darajani pale,kuna shamba la serikali. Pale utapata utalaamu na mtalaam wa kukusaidia kwa gharama kidogo. Mpigi Magohe ni sehemu nzuri kwa kuanzia kwa sababu soko la maziwa litapatikana huko huko mpigi.

  Kila la kheri mkuu.
   
 3. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shukran sana Malila, Ntajitahidi Jumatatu nikawatembelee, Nadhani ni pale kwenye ile ranch iliyo karibu na daraja, upande wa kulia kama unaenda moro na kushoto kama unarudi Dar, sio?
   
 4. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Najifunza mengi hapa wandugu
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Ndio penyewe, ukifika omba wakusaidie kuanzia ktk hatua za mwanzo kabisa. Uliza madawa, magonjwa, watalaamu wa ujenzi wa mabanda na madakitari walio karibu na eneo lako. Swala muhimu uliza pia kama kuna mfugaji aliyekaribu na sehemu yako.

  Banda zuri linapunguza gharama za matibabu,mtalaamu mzuri atakupunguzia gharama za matibabu.
   
 6. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Shukran sana aisee. Yaani j3 tu inshaallah nipo nao. Ntatoa mrejesho hapa.
  Kweli kabisa, mambo mengi yanayoyokea baadae ni mazao ya kukata kona mwanzoni mwa mchakato mzima.
   
 7. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,340
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  Hongera Kaka.
  Hivi Ng'ombe mwenye mimba ,Anauzwa Tsh Ngapi,kwa DAR.
   
 8. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa Dar sifahamu, ila kitulo ni sh laki saba (700,000).
   
 9. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,340
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  nimevutiwa na bei,gharama ya usafiri to Dar?
   
 10. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Gharama ya usafiri to dar sijajua bado. Ila mi ntawasafirisha kwa usafiri binafsi. Kwahiyo ni kulipia diesel tu.
   
 11. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,646
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimepata interest sana, tafadhali, ukotoka huko tujulishe mpango unaendeleaje...
   
 12. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna shaka ndugu, ntatoa mrejesho hapa, na wengine wafaidike.
   
 13. M

  Malila JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Ndio tunasubiri mrejesho ulioahidi mkuu. Jumanne hii inaondoka.
   
 14. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Leo nimeenda pale Narco (ruvu darajani). Nimekutana na Meneja wa ile ranch, kwakweli ni mzee mmoja mwenye subira na werevu wa hali ya juu. Nimemsumbua sana kwa maswali lakini amenielewesha mambo mengi sana. Tuliongea kama saa zima, akanitembeza kwenye maeneo baadhi ya ranch na akaniambia kama nahitaji msaada zaidi wa kujenga mabanda nimpitie siku twende wote nane nane wana mifano mizuri pale.


  Kuhusu upatikanaji wa Ng'ombe pale kwa sasa hakuna Friesian wa kweli, wapo chotara na ni wachache hata 10 hawafiki na hawana mimba. Kwahiyo kanishauri niende kwenye ranch nyingine kama vile Ngerengere (morogoro) na mwanza, karibu na mpaka wa shinyanga.

  Ntaenda kote huko inshaallah, weekend hii ntaenda ngerengere na baada ya wiki 2 ntaenda mwanza.

  Kuhusu jamaa wa kitulo, nimempigia tena simu leo baada ya kutoka ruvu, akaniambia alivyonipa jibu nimcheki february hakumaanisha watakuwepo wa kununua, alimaanisha ndio anaweza kuchukua order yangu.

  Nadhani nimeweza kufupisha msafara wa leo. Samahanini sana sikuweza kuwaupdate jana, kwani nilitingwa na shughuli za mjini hapa nikakosa muda wa kwenda ruvu.

  Kama kuna mungine ana taarifa zaidi atusaidie.
  Nb: kutokana na safari yangu ya leo. Nimeongeza hamasa ya kuwatafuta hawa ng'ombe mpaka niwafuge. Kwani ni lulu.

  Kuna mtu anashamba mbele ya vigwaza la nyasi za ng'ombe. Nimeambiwa huyo ndio tegemezi kuu la wafugaji. Anauza nyasi kama njugu. Aisee hizi business ideas nyingine ni big soo. Sijui mzee aliwazaje wazaje....!!!
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Safi mkuu.
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mkuu, good work

  very inspiring
   
 17. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuko pamoja, I'll keep you updated. Tuombe uzima.
   
 18. Mwanakilimo

  Mwanakilimo Member

  #18
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nini unaamini H. fresian ni lulu mkuu?

  Je, utawfahamuje ukiwaona kuwa huyu ni pure breed n sio chotara?
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Aina hii hutoa maziwa mengi sana,ushauri wa kwenda ktk mashamba ya serikali ni kwa sababu ya kutaka kupunguza uwezekano wa kubambikiwa, unadhani kama lingekuwa sio la serikali,si angeuziwa hata hao chotara kwa jina la pure breed. Ni mawazo yangu.
   
 20. Mwanakilimo

  Mwanakilimo Member

  #20
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukweli ni kwamba hakuna shamba la serikali Tz hii kwa sasa lina uhakika wa kuwepo kwa HF pure breed. Kuna ranchi moja ipo Kagera, zamani ilikuwa na pure breeds lakini hata yenyewe sasa inaaminika imeshachakachua. Kitulo pia waliopo sio pure breed, japokuwa kwa kiasi fulani wanakaribia.

  Kwa maoni yangu ni kuwa ufugaji wa ng'ombe sio kitu cha kuanza leo na kuona mafanikio kesho. kwa hiyo kama ni ng'ombe wanaotoa maziwa kwa wingi, then ni bora mtu ukjitahidi kuwazalisha mwenyewe kwa kufanya selection na planned breeding. Kwa maana hiyo, ni bora mtu ukanunua tu ngombe (chotara may be) kwenye shamba ambalo lina historia ya kuwa na ng'ombe wanaotoa maziwa mengi (hata karibu na Dar siku hizi yapo), then ukaenda kufanya breeding kwa kupandikiza kwa chupa, hadi ukapata line ya ng'ombe wanaotosheleza malengo yako...
   
 21. M

  Malila JF-Expert Member

  #21
  Oct 25, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  ASAS Iringa wanaweza kuwa nao, tatizo ni namna ya kupata bahati ya kumpata japo mmoja. Kilolo kulikuwa na shamba la mitamba la serikali, sijui kama bado lipo au ndio kama kawa.
   
 22. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #22
  Oct 26, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,340
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  naomba kujuzwa tofauti ya maziwa ya ng'ombe ambaye ni pure breed na chotara ,pia wanatofautiana kwa lita ngapi kwa siku.
  2.Magereza- kingolwira walikuwa na ng'ombe wazuri tu,niliwahi kumsindikiza mzazi wangu kuchukua ng'ombe ktk hilo gereza miaka ya 80's
   
 23. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #23
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwakweli sidhani kama unaweza kutofautisha pure breed na chotara kwa macho. Tunategemea uaminifu wa muuzaji au mfugaji kutupa uhakika kuwa ni wenyewe si sio. Kwakuwa kupima dna ni ngumu kidogo. Kwasababu hizi ndio maana tunapendelea zaidi kwenda kwenye mashamba ya serekali au kwa wasio na njaa kama asas na farmbase nk. Utofauti katika uzalishaji ni mkubwa sana, pure breed wanatoa kati ya lita 30 na 40 kwa siku. Na chotara ni kati ya 15 na 20 kwa siku. Hii ni pamoja na kuzingatia chakula, concentrates, maji, kujisaidia kwao na wingi wa hewa safi na vivuli vya kupumzikia watakapo ndani ya masaa 24. Kwa wastan ng'ombe anatakiwa kula 35kg za majani kwa siku, 2kg za concentrates kwa siku na almost 8litres za maji kwa siku au zaidi. Kwa muda wake autakao within those 24hrs. Hii sio shughuli ndogo kwani kama utanunua species za majani wanayopenda na yanayoshauriwa kuliwa ili kuongeza uzalishaji kutokana na upatikanaji wa nutrients sahihi basi ng'ombe mmoja anahitaji kama elf 12kwa siku ili akupe hizo litres za maziwa uzitakazo. Asipopata vitu hivi ndio hapo hata chotara atakutolea lita 5 kwa siku badala ya 20.
   
 24. L

  LAT JF-Expert Member

  #24
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mkuu

  only 8ltrs? it should be 80ltrs, isn't it !
   
 25. Chasha Poultry Farm

  Chasha Poultry Farm Verified User

  #25
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 5,054
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 48
  Wakuu hata chuo cha mifugo tengeru Arusha kuna kipindi walikuwepo now day sijajua labda kama kuna mtu mwenye contact za mtu wa pale chuoni ajaribu kuulizia hawa ng'ombe.
  Nilitembelae pale mwaka fulani nikawakuta na kuna waliokuwa wanatoa lita 60 kwa siku hawa walikuwa ni wa kubwa ajabu na kiwele chao kilikuwa kikubwa kiasi kwamba walikuwa hata kutembea ni shida
   
 26. Mshawa

  Mshawa JF-Expert Member

  #26
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 673
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 18
  Mkuu nashukuru kwa thread nzuri, na nakupongeza kwa uamuzi uliochukua,
  Ushauri na uelewa wangu ni kwamba ni vyema ukatafuta ngombe hapa dsm wanaweza wakawa wazuri ,lililo la msingi ujue kwanza historia ya ngombe, umri uwezo wa kuzalisha maziwa, etc.

  Hii ina maana kwamba unaweza kupunguza garama nyingi za usafiri, strees factor kutokana na safari, mnyama kubadili mazingira kotoka kwenye high altitude kuja kwenye low altitude pia ni problem, unaweza kumuomba hata Malila akawa key informant wako kwamba ni wapi kuna wafugaji/mfuji ngombe wazuri ambao hata yeye ana history yake.

  Ukinunu ngombe, mfano mtamba hakikisha unanunua mwenye mimba, na ukinunu ngombe aliyekwisha zaa uhakikishe pia ana mimba lakini pia akamuliwe uone mwenyewe ni kiasi gani anatoa on the spot ili ujiridhishe usije pewa history ataoa lita 10 kumbe uwezo wake ni lita mbili, lakini pia ku avoid conception failures, kama utawahitaji ni pm nikuelekeze kwa mfugaji. kila la heri.
   
 27. M

  Malila JF-Expert Member

  #27
  Oct 27, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Kweli kabisa, kubadili hali ya hewa ni changamoto kwa wafugaji wote, iwe samaki,kuku,nk Kiegea Moro kuna mjeshi mmoja ana ng`ombe balaa, au kama unaweza kwenda Kwa Pm mmoja mstaafu, unaweza pata mbegu na kwa gharama ndogo sana. Najaribu kumtafuta Vert.officer mmoja rafiki yangu, alikuwa anauza hawa ng`ombe na yupo Ubungo. Nikimpata nitaweka data hewani.
   
 28. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #28
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,340
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 38
  Duh! Asante,nimesitisha zoezi la Ng'ombe wa maziwa.ngoja sasa niwekeze nguvu zote ktk Mbuzi kwa ajili ya nyama.nikishajipanga ntarudi tena
   
 29. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #29
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 466
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 16
  Wakuu asanteni sana kwa michango yenu:
  Hii nchi yetu haina mipango yoyote ya maana, nd'o maana Malila uliomba uuziwe shamba la Kitulo ili uliendeleze na ulifanyie kazi ya maana.
  Pale Kitulo wanatoa pure breed Freishian wanaotoa maziwa 30-40 lts in 24 hours.
  Wanapandisha mitamba, wanapima kama imepata mimba kila baada ya miezi mitatu (wale wanaopatikana wana mimba wanagawanywa sehemu mbili, nusu ya kwanza wanabakizwa kwa kuendeleza kizazi, nusu nyingine wanauzwa kulingana na order; japo mtu mmoja anatakiwa kuchukua ng'ombe mmoja tu kwa sababu ni wachache). Aibu hii! Mi' nimeweka order toka August, 2011 ili nichukue November, 201; watapima tena mwezi February, 2012.
  Kuna mfugaji mwingine ambaye nilishapewa contacts zake ambaye yeye niliambiwa ni Mkurugenzi sijui wa nini, anashamba kubwa. Nilimtumia email toka August, nikawa nimekata tamaa kwa kutojibiwa, lkn this week alimwomba msimamizi wake anijibu, nikajibiwa kuwa wana ng'ombe 300, lkn wanahitaji wawe 450, kwa hiyo na wao wanatafuta 150 zaidi kwa sababu wameshaanzisha milk processing plant. Hii ni sehemu ya email hiyo: ".....Dear ....,
  My name is ...... coordinator of Molomo and Gararagua Farm situated West Kilimanjaro.
  Regarding your information of keeping dairy cattle is the good idea

  1.0 For the time being we are not able to sell to you our dairy cattlle because our road map shows that we have to increae dairy cattle up to 450 from current 300 dairy cattle

  2.0 Concering selling of heifers we cant afford while are looking for heifer to increase our milk production.

  For your information we have managed to build our own milk processing plant and we still in trials run.

  3.0 The current price of dairy catle in open market it range from 800,000/= to 1,200,000/=

  4.0 The minimum and maximum amount of milk production per cow depend on compound meal you feed you dairy cattle and weather

  I think you got my concept

  Best regards,

  ............
  ..........."
  Sikukata tamaa nikajikuta najuana na mTz aliyepo Republic of South Africa (through mtandao) akaniambia nicheck www.investindairycattle.co.za na www.hooggekraal.co.za. Nikamchokoza huyu jamaa anyepatikana kwenye website ya pili (www.hooggekraal.co.za) akaniomba namba ya simu ili YEYE ND'O ANIPIGIE aniulize vizuri.
  Anasema:
  (1)Heifer (mtamba) mmoja mwenye mimba ya miezi 6 anauza kwa 1,550 rands sawa na 3,25,000 Tshs
  (2)Hauzi ng'ombe wasio na mimba, mfano: ndama wa umri wa miezi 8-9
  (3)Kama ni kusafirisha, KIASI CHA CHINI KABISA anachoweza kusafirisha ni ng'ombe 40 - chini ya hapo hafanyi biashara hiyo.

  Mnaona nchi za watu wanavyotupiga bao?
  Linganisha na kwetu:
  (1)Kupata mtamba bora wenye mimba ni issue
  (2)Hata kama wenye mimba wapo hakuna atakayekubali kukuuzia
  (3)Serikali yetu haina uwezo wa ku-supply ng'ombe kwa watu kutokana na mahitaji, KIASI CHA JUU KABISA ambacho serikali yetu inaweza kumuuzia mtu ni ng'ombe mmoja (1)!

  Kwa sasa nasubiri kang'ombe kamoja toka Kitulo, hopefully nitapata kengine February.
  Inamaanisha kuwa nikitaka niwe na ng'ombe 20 kuanzia November, 2011 basi ujue nitafikia lengo hilo November, 2015 wakati huo huo hawa wa mwanzo watakuta walishajichokea! Shame on you Tz!
   
 30. M

  Malila JF-Expert Member

  #30
  Oct 27, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,047
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 48
  Nikufanyie mpango upate ka pili?
   

Share This Page