Hold on a minute!!.... Lengo la Mkutano wa Jangwani lilikuwa nini... lilifikiwa?

Mwanakijiji bhana........ Hahahahaaaaaa.... This is politics....embu nisiseme mie nisije tukanwa Na kundolewa Na mood ya Kazi.
 
Mzee MM,

Mimi nafikiri lengo kuwa sana la CDM ni kuwasalimia wananchi wa DAR kabla ya kuelekea kusini kwani isingekuwa busara timu yote ya viongozi kutoka Kaskazini, Magharibi kupita hapa DAR kwenda Kusini bila kuwaambia wanaDAR nini chama chao kinaenda kukifanya Lindi na Mtwara.

Cha pili ilikuwa ni kuwaonyeha Umma wa watanzania jinsi gani kila korner ya nchi hii watu walivyobalika na ndiyo maana mkutano ule ulirushwa live na ITV yenye coverage kubwa nchi hii..

tatu ilikuwa ni kuwapa watu angalau easimame wapi katika swala la katiba mpya ingawaje watu wengi wanasema Lisu hakupewa muda wa Kutosha lakini nadhani ni kutokana na muda waliokubaliana na ITV kuwa Masaa mawili.

Ila kwa ujumla lengo lilifanikiwa na message imewafikia CCM, Polisi ppamoja na serikali.. Maana walikataza watu kuandamana kwenda kwenye mkutano wa CDM... watu wakaandamana hata baada ya mkutano ule na hii inaonyesha kwamba CCM hawana tena uwezo wa kuwakandamiza upinzani kwa tishila la polisi na taarifa za uwogo na kiinteligensia...
 
Nikweli watu wamekuwa wakiuliza hili swali ila sio spesho sredi kama hivi bali walikuwa wanalichomekea ndani ya nyuzi nyingine za Mkutano, na majibu yalikuwa yakitolewa ndo maana nawaambia muwe makini na huyu mzee mwanakijiji sababu hakuona kuchangia mawazo yake kule kwingine bali afungulie uzi wake na mambumbu wa humu JF wanajichanganya sababu ya saikolojia yake ya kucheza na vichwa vya habari pamoja na kujazia nyama mawazo ya wengine, Mlimani mtu kama huyu tunamwita "Professional desa"

Mmmmmmm.....hapa sisemi neno.
 
Kuna kitu kimeanza kunisumbua katika kufikiria muendelezo wa mikutano mbalimbali ya CDM.. ili nisije kujikuta napotoka nimeonelea kwanza niulize kwa wale wenye kujua lengo la mkutano mkubwa wa CDM Jangwani siku ya Jumamosi lilikuwa ni nini na kama lilifikiwa au la. Kuna uwezekano kulikuwa na malengo mbalimbali kama vile:

a. Kuanzia M4C kitaifa (ni marudi ya lile la Arusha ambalo nalo lilirushwa kitaifa?)
b. Kuwaambia wananchi kuhusu Katiba Mpya... (ilihitaji mkutano mkubwa?)
c. Kuwaeleza wananchi ubovu wa watendaji wa serikali (mbona kubadiilsha mawaziri ni ushahidi wa wazi)
d. Kupata wanachama wengi (idadi ya 3000 kama ilivyotangazwa ni kidogo sana kulinganisha kama ingeweza kufanywa kwa namna nyingine)
e. Kuchangisha fedha kwa ajili ya chama (za nini?zinachangia CDM taifa au CDM mahali?; zimepatikana kiasi gani hadi hivi sasa?)
f. x,y


Kwa maana ninaanza kutotaka kuona political acrobatics za kuvutia.. maana baada ya Jumamosi kupita leo Jumatatu na wiki hii watu hawa waliohamasishwa wanafanya nini? Na wale wa mikoani walikohamasishwa na wanakoendelea kuhamasika wanafanya nini baada ya kujiunga na mwamko wa mabadiliko a.k.a M4C?

Nitawasoma kisha nitatoa mawazo yangu - inshallah - kwenye toleo la Jumatano la gazeti..
na chama kina ruzuku ya kutosha na wanachama ni waaminifu kwa kulipia kadi , mi nadhani yale viongozi wetu wa chama wanayo ya hubiri hasa kuhusiana na matumizi mabaya ya hela za serikari wangari yatumia pia chamani nadhani ingeri saidia kuongeza kipato
japo wengi watanipinga lakini maisha yenu(viongozi) wengine yamegeuka ghafla ... tujichunguze kabla hatujaharibikiwa
M4C !
 
Ngoja niondoke hapa hichi kizee Mwanakijiji naona kinazeeka vibaya halafu kinataka kutukaririsha na hivyo vihoja vyake virefu Pambaf mods mpeni ban hako kadingi
 
Mwanakijiji kuna mahali pana shida au jambo ambalo halijajulikana sidhani kama CDM inahitaji kuita watu jangwani ili wavue gamba na kuvaa gwanda, pia sidhani kama wanaweza kuita watu jangwani ili kufanya harambee ya chama, pia siamini kama kwa muda ule wangeweza kuelimisha juu ya muungano au hata uundwaji wa katiba mpya.

Kwangu mimi nafikir malengo yao yalipaswa kuwa juu zaid ya hapo, unless kama wanayafanya siri ila kwa uelewa wangu mdogo CDM inatakiwa iuze sera zake mbele za watu ionyeshe japo ina M4C lakin wao wana sera gapi ambaazo zinamtetea mtanzania, na mpaka sasa katika sera hizo kwa kuwa ni chama kikubwa cha upinzani wamefanya nini.

Nahofia kuwa yawezekana kabisa kuna ambayo wao waliyatoa kama sehem ya hotuba zao za kuhamasisha lakni yatatumiwa na CCM kama ilani yao au moja ya sera ake kwa wakati ujao.

Namshauri Mbowe kaka yangu aangalie kwa makini watanzania wanataka nini na watueleze wa mikakati gani ya kutupa yale tunayoyataka. hili nafikir liwe ndio lengo kubwa la kampeni hii ya M4C. tena wawe makini sana manake kama vijana wa kiume ndio waliokuwa wengi pale, wakifuatiwa na vijana wa makamu basi ajue hapo pana mob psychology tu ambayo after certain period yaweza kuhamishiwa kwingine. Watu wanahitaji kujua sera za chama, na mbinu au njia gani zitatumika kutimiza sera hizo tena elim hii baada ya kuambiwa basi wapewe na vikabrasha vitakavyo elezea haya kwa umakini.
jamani naomba tu msinishambulie
I never new this!!
Kuna aina fulani ya siasa inayosema watu wanaokwenda kwenye mikutano ya vyama vya upinzani huwa hawapigi kura....
Naona hapa umekuja na aina nyingine ya msisitizo wa siasa ya kukata tamaa.

Nakubaliana na wewe kwenye kujua sera..........lakini vikabrasha?? watanzania huwa wanasoma?:sleepy:
Mzee Mwanakijiji, najua unataka mtazamo wa watu, sipendi kuamini kwamba hujui madhumuni ya mikutamo wa juzi au unaona madhumuni hayo ni mepesi.............:ranger: Nitakusoma Jumatano.
 
Last edited by a moderator:
kuna kitu kimeanza kunisumbua katika kufikiria muendelezo wa mikutano mbalimbali ya cdm.. Ili nisije kujikuta napotoka nimeonelea kwanza niulize kwa wale wenye kujua lengo la mkutano mkubwa wa cdm jangwani siku ya jumamosi lilikuwa ni nini na kama lilifikiwa au la. Kuna uwezekano kulikuwa na malengo mbalimbali kama vile:

A. Kuanzia m4c kitaifa (ni marudi ya lile la arusha ambalo nalo lilirushwa kitaifa?)
b. Kuwaambia wananchi kuhusu katiba mpya... (ilihitaji mkutano mkubwa?)
c. Kuwaeleza wananchi ubovu wa watendaji wa serikali (mbona kubadiilsha mawaziri ni ushahidi wa wazi)
d. Kupata wanachama wengi (idadi ya 3000 kama ilivyotangazwa ni kidogo sana kulinganisha kama ingeweza kufanywa kwa namna nyingine)
e. Kuchangisha fedha kwa ajili ya chama (za nini? Zinachangia cdm taifa au cdm mahali?; zimepatikana kiasi gani hadi hivi sasa?)
f. X,y


kwa maana ninaanza kutotaka kuona political acrobatics za kuvutia.. Maana baada ya jumamosi kupita leo jumatatu na wiki hii watu hawa waliohamasishwa wanafanya nini? Na wale wa mikoani walikohamasishwa na wanakoendelea kuhamasika wanafanya nini baada ya kujiunga na mwamko wa mabadiliko a.k.a m4c?

Nitawasoma kisha nitatoa mawazo yangu - inshallah - kwenye toleo la jumatano la gazeti..
malengo yalifikiwa kwa zaidi ya 100%, kama chama cha siasa kinatakiwa kufanya kazi ya siasa, na fahamu mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine, kila wanapopita wanaongeza hamasa kwa wapenzi na mashabiki ya kuwa chadema ni chama mbadala, chadema ni chama cha watu kipo kwa ajili ya kumkomboa mtanzania kutoka katika utawala wa kifisadi

hata ccm juzi juzi hapa, nape alienda bukoba kwenda kufufua uhai wa chama ila hakuweza kuhamasiha vijana kama ilivyofanikiwa kwa chadema juzi, na mwanakijiji nadhani labda hukulijua hili au ulilijua ila hujalisema sababu halikuwa na mashiko kwa wanabukoba

kama chama cha siasa kilitoa maoni ya kulifumua balaza la mawaziri, cc ya chadema ilikaa ikatoa mapendekezo kadhaa kuhusu kulisuka upya baraza la mawaziri lakini walipuuzwa

cag akaja akatoa ripoti iliyoonyesha ubadhirifu... Mawaziri wakagoma kujiuzuru rais akasema msijiuzuru hili swala ni upepo acheni utapita baada ya wabunge hasa wa chadema kuhamasisha kukusanya sahihi kwa lengo la kumtoa pm baraza likarekebishwa

je? Kushinikizwa kufanya mabadiliko ndio uwajibikaji?

Je? Ukishinikizwa kufanya mabadiliko utafanya mabadiliko yatakayoleta utofauti wa utendaji au mabadiliko yatakayoleta sura mpya?

Mabadiliko ya baraza la mawaziri yapo kwa maslahi yale yale ya wachache na m4c ipo mpaka tunaingia kwenye uchaguzi 2015 kuhakikisha watanzania wanaelewa tunachodai



joash mussa
mwanachama chadema
 
Kwetu wakristo kusali hakusubiri Christmas.....ni kila jumapili.......Siasa nayo vilevile usisubiri mpaka uchaguzi ukaribie ndio uwafuate wananchi......haya ndio matatizo yaliyoipata NCCR-Mageuzi ile 1995, uchaguzi ulipoisha hawakurudi kwa wananchi tena mbali na mvuto waliouonyesha....matokeo yake tunayaona leo....nadhani CDM waendelee tu ila wafanye maboresho katika maudhui......hasa kuhimiza wananchi wajiandikishe katika daftari la kupiga kura.....tatizo la watanzania wengi hawapigi kura na kuwaachia wengine wawachagulie viongozi
 
Mhh mzee mwakijiji,
Kazi ya siasa kamanda, sio wengi wenye mitandao kamanda, redioni tunabanwa, luninga wanaminya lazima tuonane ana kwa ana. Tunahamasisha base mkuu. Tunafikisha ujumbe mzima mzima. Lengo lilifanikiwa. kazi yetu kubwa ni kuelimisha jamii. Tutatumia njia zozote zile kuifikia jamii. Hakuna njia mbaya kama inasaidia.

Tunakaribisha mawazo. Chadema ni watu na watu ni mimi na wewe ndio maana ya nguvu ya umma. Vilevile sio rahisi kuwapata viongozi wa kitaifa kwenye kila kijiji, hivyo inasaidia kuchochea viongozi wa tarafa, kata, matawi na vitongoji, inasaidia kuwaamsha wengi ama kujiunga na kuchangia na kuelewa nini tunakipigania. Mikutano kama hii inahitajika mingi sana. wenzetu wanajitangaza kwa muda mrefu, kumbuka bado tunajenga chama tunapenyeza mtandao kwa kila kaya. Wanachama 3000 sio haba chama miaka 20 iliyopita kilianza na mwanachama 1. Kumbuka kuna swing vote nyingi sana Tanzania na Dar es salaam ambazo ndio muhimu sana.

Peoplessss.......................power.............................
 
Suala la kuelewa mafanikio ya mkutano huu...yanahitaji zaidi qualitative research....unaweza ukaangalia mtazamo wa waandishi wengine na watu walivyochangia kupitia kwenye vyombo vya habari na social networks kwa kutumia content analysis technique!
Pia unaweza ukabuni maswali ambayo umeyadizaini katika conceptual framework nzuri...kwa kuangalia information needs........
Otherwise...kwa mtindo huu hautapata kitu na suala la impact ya elimu na mawazo hayapimwi quantitavely kama hivi.....!
 
Ile sadaka na mimi ilishangaza ingawa si sana. Utaratibu wake haukunivutia na hasa kutoka kwenye chama kinachoaminiwa kuwa makini na cha kisasa zaidi. Sisi huku vijijini sadaka hatuna!

Kumbuka sio watu wote wana Mpesa ama akaunti ya benki. Na vilevile elewa kwamba mtu akikuchangia hata kama ni kiasi kidogo kwa namna moja au ingine anakuwa anaji commit au ana solidify relationship yenu. Chama kinakuwa "chake" sio tena chama cha "wale". Unaweza wewe ukaliona ni jambo dogo au ni ghasia lakini kwa mmachinga kutoa pesa yake adimu mfukoni na kuumpa mbunge ni jambo ambalo hawezi kulisahau kirahisi lina impact kubwa kwenye maisha yake. Ni vigumu akuchangie pesa halafu siku ya uchaguzi asiende kukupigia kura. Zile ni "kura" zinakusanywa sio sadaka.
 
Ukitafuta hard facts kwamba nini kimepatikana kwenye mkutano wa Jangwani unaweza usipate jibu. But symbolically, the signifacancy ya CHADEMA kufanya mkutano mkubwa wa hadhara Dar should be understimated.

Hata hivyo sehemu ambayo nadhani ilipungua ni hotuba ni Mwenyekiti Freeman Mbowe. I expected to hear mambo mengi na ya msingi zaidi ya michango. Nilitarajia agusie mambo yanayowagusa watanzania on daily basis. Dr Slaa alifanya vizuri na hata Lissu aliongea mambo ya msingi. Pengine muda ulikuwa hautoshi.
 
Kuna kitu kimeanza kunisumbua katika kufikiria muendelezo wa mikutano mbalimbali ya CDM.. ili nisije kujikuta napotoka nimeonelea kwanza niulize kwa wale wenye kujua lengo la mkutano mkubwa wa CDM Jangwani siku ya Jumamosi lilikuwa ni nini na kama lilifikiwa au la. Kuna uwezekano kulikuwa na malengo mbalimbali kama vile:

a. Kuanzia M4C kitaifa (ni marudi ya lile la Arusha ambalo nalo lilirushwa kitaifa?)
b. Kuwaambia wananchi kuhusu Katiba Mpya... (ilihitaji mkutano mkubwa?)
c. Kuwaeleza wananchi ubovu wa watendaji wa serikali (mbona kubadiilsha mawaziri ni ushahidi wa wazi)
d. Kupata wanachama wengi (idadi ya 3000 kama ilivyotangazwa ni kidogo sana kulinganisha kama ingeweza kufanywa kwa namna nyingine)
e. Kuchangisha fedha kwa ajili ya chama (za nini? zinachangia CDM taifa au CDM mahali?; zimepatikana kiasi gani hadi hivi sasa?)
f. x,y


Kwa maana ninaanza kutotaka kuona political acrobatics za kuvutia.. maana baada ya Jumamosi kupita leo Jumatatu na wiki hii watu hawa waliohamasishwa wanafanya nini? Na wale wa mikoani walikohamasishwa na wanakoendelea kuhamasika wanafanya nini baada ya kujiunga na mwamko wa mabadiliko a.k.a M4C?

Nitawasoma kisha nitatoa mawazo yangu - inshallah - kwenye toleo la Jumatano la gazeti..

Mimi nadhani lengo lilikuwa kupima upepo wa Dar. Harakati za CDM toka uchaguzi wa 2010 zimekuwa zikifanyika mikoani kwa sana na sikumbuki tangu mkutano wa ufunguzi wa kampeni 2010 kama CDM iliwahi kufanya mkutano wowote Dar. Tumepima kumbe tunakubalika tofauti na hoja za CCM kwamba Dar ni stronghold yao na CDM haina chao. Ninaamini kuwa safari nyingine mkutano ukifanyika Dar itakuwa mara kumi ya huo wa Juzi.

Kwa ujumla yaliyozungumzwa juzi yamekuwa yakisemwa kila mahali, hivyo hilo haliwezi kuwa core lengo la mkutano wa juzi. Sasa chachu imewekwa Dar, kwani hatimaye Dar ndipo patakuwa kitovu cha ukombozi wetu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
inamaana Mwanakijiji huoni if there is something gained by CDM from the meeting? Do you mean CHADEMA's Popularity in Dar is just the same as it was before the meeting?

Do you mean the 'fear' that CCM has on CDM is just the same as it was before the meeting?

1. Haya yaweza kuwa ni malengo ya mkutano ule?????
2. Hivi kwa mawazo ya kawaida ule umati yaweza kuwa kuna mtu alikuwa hajawahi kuisikia CDM kweli????
3. To instill fear on the other side????? The other side you mean wanachama au viongozi wao??? Is fearing some one a good strategy to success?????
4. Ule umati uliokuwepo pale na wengine waliobaki majumbani na chama chenyewe wangeweza kufaidika zaidi na mkutano ule kama ungefanywa vinginevyo?????

Hebu leo tujaribu kuzumgumza hapa bila matusi na kejeli tufikie muafaka
 
Mimi naona lengo lilitimia. Kumbuka Wahenga walisema Mwenda bure si mkaa bure, huenda akaokota. Ukiangali mahudhurio ya mkutano wa Jangwani, utaona kwamba watu walihudhuria kwa wingi. Kitendo cha watu kuhudhuria wengi namana ile, ina maana kuna kitu kinaendelea vichwani mwao kuhusiana na CDM. Aidha, ikwembukwe kwamba baadhi ya vyama hukodi magari ya kusafirisha watu kwenda kwenye mikutano ya namna ile, sina uhakika na watu waliohudhuria Jangwani kama walisafirishwa maana mimi nilwaona kwenye picha. Kama walisafiri wenyewe kuhudhuria ule mkutano, CDM inafanya vizuri, ifanyie kazi mapungufu yanayojitokeza. Kitendo cha watu kuhudhuria mkutano ambao sio wa kampeni za uchaguzi ni dalili tosha kwamba hicho chama kipo mawazoni mwa watu, maana kuna uwezekano hao wakirudi makwa kila mmoja wao atafikisha ujumbe kwa wastani wa watu watatu, hivyo CDM itazidi kuenea.
 
Mi nadhani kama chama Chadema kazi iliyopo mbele ni kubwa mno kuliko iliyopita.Kwangu mimi wanachokifanya viongozi wa Chadema ni kumantain jina la chama kwenye masikio na akili za washabiki na wapenzi wao.Kama chama kukaa muda mrefu bila ya kukutana na Wananchi ni tatizo ambalo litafanya wananchi waone kama wametengwa.
 
Awali lazima uelewe kuwa ni jukumu la kisiasa kufanya mikutano ya hadhara mara kwa mara hasa kwa vyama vya upinzani vinavotafuta ridhaa ya kuingia madarakani! kuna malengo mbalimbali ya mikutano mojawapo ni kukiweka chama hai na kukusanya wanachama wapya!pili kunapokuwa na tukio kubwa la kisiasa kama hili la sasa la kuandika katiba mpya (kama ni mpya kweli???) chama kinatoa maono yake na maelekezo kwa wanachama wake wafanye nini wakati wa zoezi zima hili! Kila chama kina staili yake ya kupata funds wengine wanategemea wafanyabiashara wakubwa {mfano ccm} ambao in turn hawalipi kodi wengine wafadhili wa nje na sasa CDM imekuja na style mpya ya kuwahamasisha wanachama na wapenda mabadiliko wachangie chama chao sasa kwamba imepatikana shilingi ngapi na itatumika naamini zipo kamati husika ndani ya chama kazi yao ndio hiyo ku allocate resources according to the needs!unasema wanachama wangeweza kupatikana kwa njia zingine zipi?? Turn up ya watu na hotuba zilizojaa hamasa na elimu ya uraia ni kigezo kuwa mkutano ulifanikiwa!!kutoka hapo sasa harakati zitaelekea sehemu zingine na kuwa watu wapoje baada ya mkutano hili ni swala la viongozi wa sehemu husika kukazia maarifa na mwisho mabadiliko hayaji over night kunatakiwa mbinu na mikakati ya kila aina!!
 
Hakuna hata mmoja aliyegusia hoja ya kuwa huu mkutano ulikuwa ni kuitangaza vodacom ambayo mmiliki wake mkuu kwa Tanzania ni Rostam Aziz na mpiga debe mkuu ni Binti Makamba. Kwa maana hiyo hii ni milki ya makada na wadau wa CCM wakubwa sana.

Kikowapi?
 
Back
Top Bottom