Hold on a minute!!.... Lengo la Mkutano wa Jangwani lilikuwa nini... lilifikiwa?

Nimesema:

Lengo lilikuwa ni kuitangaza Vodacom Mpesa.

Rostam Aziz ni kichwa hapana mchezo, unaijuwa "Hap Ki Do", ni kutandikwa kwa nguvu zako mwenyewe!

Ni nani abishae, hata mwakilishi wa Vodacom alipewa muda mrefu kuelezea hiyo huduma kuliko wana siasa.
 
Mimi kwa mawazo yangu naona CDM walifikia malengo na kuzidi,tunapoongelea M4C ni lazima ionekane
kweli kuna vuguvugu la mabadiliko na hii haiwezekani kuonekana kwa CDM kujifungia na kufanya vikao vya
ndani,lazima kuwe na mikutano ya hadhara ambayo itawahamasisha watu na kuwafanya kuelewa kinachoendelea.
Mkutano wa jumamosi ulikusanya watu wengi na kufuatiliwa live kwenye TV,ni kufikiwa kabisa kwa lengo la
kuteka akili za watanzania na kuwaingiza kwenye vuvguvugu la mageuzi.Na baada ya hapo kazi itakuwa rahisi
sasa kujipanga kuwaelimisha watanzania juu ya elimu ya uraia,katiba na mengineyo.Mimi nawapa Big up CDM,
maana nina taarifa nyingi kutoka mikoa ya kati juu ya mabadiliko yaliyoletwa na mkutano wa jumamosi.
CHADEMA KEEP IT UP"
 
gfsonwin ulienda kwenye ule mkutano? Nafikiri kila mwananchi aliyeenda pale anaswali kwa kamati ya katiba mpya kuhusiana na masuala ya Muungano. Lisu alitumia lugha nyepesi ambayo nahisi wengi tulimuelewa.

Tatizo la ule mkutano lilikua on time management.Kumbuka ungewaambia watanzania wafike pale saa sita ungeishia kuhutubia watu 10.

ma bro Mlachake sikwenda ila niliufuatilia kupitia ITV na kweli Lissu aliongelea swala la katiba ila tuiulize kwa makini na hapa tuache ushabiki hivi kwa muda ule unafikir elimu aliyoitoa imefanikiwa? malengo ya somo lolote ni kueleweka. sas je ukiennda hapo manzese tu na kuuliza kijana yyte aliyeenda nini alichoelewa juu ya hiyo katiba ataweza kueleza?

sitaki kumani kuwa malengo ya mkutano ule ulikuwa uelimisha kuhusu katiba mpya na kama wanalengo hili basi wawasiliane na wataalam wa community education waweze kuwasaidia katika hili but single day masaa 3 hayawez. Informal education minimumu required time far knowledge transmission is a week.

but atleast wmejaribu ila yetupasa kuwasahuri zaid in a positive manner. na nataman hii thread waipitie waisome ili kujua nini kilikuwa ni kosa.
 
Last edited by a moderator:
MMJ ukifuatilia nyuzi zako kama sio zote basi ni nyingi mimi huwa sizichangiaji sababu ni moja tu, nimegundua unapenda attention ya watu humu ndani naninakushauri hiyo tabia uiache sababu wanaokuona kama unamawazo yenye busara wakaja gundua unacheza na kalamu kuziteka akili zao itakukosti sana.

CDM ni chama cha Upinzani chenye vichwa makini na mipangilio makini, kwataarifa yako hii mikutano ni moja ya mikakati ya ndani ya chama ambayo si kila wakati itolewe nje, majibu yake subiria utayapata.

Jibu moja wapo nihili la wewe kupanga kufungua Tawi la CDM huko uliko, mbona hukufikiria kufanya hivyo tangu zamani na ukatangaza jmosi? Yako mengi mengine tutamfaidisha Nape na Magamba kama unataka kujua ni-PM

Na CCK amwachie nani?
 
Kila mchangiaji hapa anasema alikuwa na wazo kama Mzee Mwanakijiji Mkutano ulikuwa juzi walikuwa wapi wasilete thread kama hiyo jana au leo kabla ya Mzee Mwanakijiji jamani tusiwe tukidandia thread kwa kusema mlikuwa mnafikiria kama yeye kwa vile anaheshimika sana hapa jamvini . Mzee Mwanakijiji mimi nakuheshimu lakini ukileta tena thread ya kutuvunja moyo kama hii naona utanitafutia ban tena ambayo iliisha jana. nilipewa ban ya siku 90 kwahiyo naomba uachane na hii thread haraka

Nikweli watu wamekuwa wakiuliza hili swali ila sio spesho sredi kama hivi bali walikuwa wanalichomekea ndani ya nyuzi nyingine za Mkutano, na majibu yalikuwa yakitolewa ndo maana nawaambia muwe makini na huyu mzee mwanakijiji sababu hakuona kuchangia mawazo yake kule kwingine bali afungulie uzi wake na mambumbu wa humu JF wanajichanganya sababu ya saikolojia yake ya kucheza na vichwa vya habari pamoja na kujazia nyama mawazo ya wengine, Mlimani mtu kama huyu tunamwita "Professional desa"
 
Malengo yalifikiwa. Kama alivyosema Mnyika kuwa CHADEMA ikikubalika katika jiji la Dar es salaam lenye wakazi zaidi ya milioni 4, na wanaotoka sehemu zote za Tanzania, unakuwa umefanikiwa kukieneza chama katika nchi nzima. Vile vile aliongeza kusema kuwa hata TANU, chama kilichodai uhuru wa Tanganyika, kilianzia na klifadhiliwa na wazee wa Dar es salaam. Kwa mfano, ushawishi wangu kwa ndugu zangu wanaotegemea msaada wangu (wa hali na mali), sisemi nitaingilia uhuru wao wa kisiasa, unaweza kuwavuta watu zaidi ya 50 kijijini kwangu.

Jiji la Dar es salaam lina ushawishi mkubwa katika siasa za nchi hii, hivyo ilikuwa sahihi kwa CHADEMA kufanya mkutano huo jangwani kwa kuwa mwangwi wake utaenea nchi nzima.
 
ma bro Mlachake sikwenda ila niliufuatilia kupitia ITV na kweli Lissu aliongelea swala la katiba ila tuiulize kwa makini na hapa tuache ushabiki hivi kwa muda ule unafikir elimu aliyoitoa imefanikiwa? malengo ya somo lolote ni kueleweka. sas je ukiennda hapo manzese tu na kuuliza kijana yyte aliyeenda nini alichoelewa juu ya hiyo katiba ataweza kueleza?

sitaki kumani kuwa malengo ya mkutano ule ulikuwa uelimisha kuhusu katiba mpya na kama wanalengo hili basi wawasiliane na wataalam wa community education waweze kuwasaidia katika hili but single day masaa 3 hayawez. Informal education minimumu required time far knowledge transmission is a week.

but atleast wmejaribu ila yetupasa kuwasahuri zaid in a positive manner. na nataman hii thread waipitie waisome ili kujua nini kilikuwa ni kosa.
gfsonwin Tatizo ni muda wetu sisi watanzania. uli mkutano ulihitaji muda zaidi. ni mtanzania yupo aliyetayari kwenda kwenye mkutano saa nne asubuhi? ni mtanzania yupo asiye na utamaduni wa kufanya mambo the last minute?
 
Last edited by a moderator:
ma bro Mlachake sikwenda ila niliufuatilia kupitia ITV na kweli Lissu aliongelea swala la katiba ila tuiulize kwa makini na hapa tuache ushabiki hivi kwa muda ule unafikir elimu aliyoitoa imefanikiwa? malengo ya somo lolote ni kueleweka. sas je ukiennda hapo manzese tu na kuuliza kijana yyte aliyeenda nini alichoelewa juu ya hiyo katiba ataweza kueleza?

sitaki kumani kuwa malengo ya mkutano ule ulikuwa uelimisha kuhusu katiba mpya na kama wanalengo hili basi wawasiliane na wataalam wa community education waweze kuwasaidia katika hili but single day masaa 3 hayawez. Informal education minimumu required time far knowledge transmission is a week.

but atleast wmejaribu ila yetupasa kuwasahuri zaid in a positive manner. na nataman hii thread waipitie waisome ili kujua nini kilikuwa ni kosa.

Aliyekwambia mwenye njaa ukimwelimisha ataelewa ninani wewe? Hayo ya kupanda Lissu na wengine ni moja ya vibwagizo tu ili walioshiba wasipate ya kuuliza kama huyu MMJ na wewe. Kwataarifa yako asilimia 80% ya waliofika ukiwauliza nini hasa kiliongelewa hawajui ila walihamasika na kuipenda CDM na sasa watu hawaogopi tena kujiita CDM. Na tayari Magamba wamebanwa hawana pakupumua. Yaani hii ni sawa na kusema kwanini unaswali swala tano kila siku? Au kwanini unaenda ibadani kila siku za ibada?
 
Last edited by a moderator:
Mwanakijiji I respect!! Unajua kama Mtihani Umewekwa after four Years!! Form one to form four na katikati Hakuna Form two exams wanafunzi wengi wanakuwa lazy!! Imagine CDM wawe lazy Kusubiri 2015!! What will Happen? Ninajua hakuna target iliyo karibu ila awareness ni Muhimu!! Kuna baadhi ya Vyama ili kukutana na wananchi wameshindwa na wanasubiri Hadi itokee misiba ya Watu Maarufu!! Ila kama imeweza kuwakusanya Watu just Kuwapa awareness Kwangu Mimi in first Place nasema ni achievement ya over 80%% Believe Me!! N.B Ila si Busara kuwachosha watu wasiokuwa na Mitihani Karibuni!!!
 
Tatizo ule mkutano haukuwa na dhamira yeyote. Yaani Chadema walikuwa na mambo lukuki wakalazimisha yote kuyabananisha ili itoshe kwneye Air time yao ITV. Next time jaribuni kuwa na dhamira moja huwezi kuongelea Katiba mpya, Mamlaka ya rais, Muungano, Ufisadi, Hali ngumu ya uchumi kwenye platform moja halafu ukaelezea kila moja kwa undani. Mwisho wa siku mtu anatoka hana moja!
 
Mkuu anaogopa hadithi ya bendera hufuata upepo...kumbe hata huku kwenye tasnia ya siasa kuna wakati akili inatumika zaidi kuliko emotions! Maana naona kama tunakwenda na emotions tu na kutishiana kwamba bila huyu au huyu mambo hayakamiliki. Kama tunatabia ya kujiuliza maswali kama MMKJ tutabadili status quo yetu,period!
 
siasa ni pamoja na matangazo, ili kuongeza hamasa na kuthibitisha kuwa cdm sio cha msimu wa uchaguzi ni lzm kuwe na matukio ya mara kwa mara ya kuwahamasisha watu na kuwafanya wazidi kujua njia ya kupita
watu 3000 sio wachache mkuu kumbuka 2na mbunge wa kura 1, kumbuka zanzibar komando alichukua nchi kwa tofauti ya kula 1500 cdm inahitaji kujitangaza zaid na kuhamasisha zaid wananchi
tusisahau kuwa ccm ni km mbwa mzee............ lzm 2pate mbadala kambwa kadogo kenye kujua mbinu mpya
 
The main objective of the Chadema rally was to sensitize the Dar population about the party!! Hawa waswahili wanadanganywa sana na chama cha magamba hivyo ni muhimu kuwaelimisha ili waamke. Ukiwapata hawa waswahili wana ushawishi mwingi nchi nzima na ndio maana kama mnakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu enzi za popularity ya NCCR mageuzi ,uchaguzi DAR ulibidi usimamishwe kwa mbinu za CCM walivyohisi kuwa majimbo yote yalikuwayanachukuliwa na upinzani!! Sasa hivi Chadema wamechukua Mwanza, Mbeya Arusha na imebakia DODOMA na DAR basi wakifanikiwa kuchukua miji hii miwili watakuwa wamechukua nchi!!
 
Kuna kitu kimeanza kunisumbua katika kufikiria muendelezo wa mikutano mbalimbali ya CDM.. ili nisije kujikuta napotoka nimeonelea kwanza niulize kwa wale wenye kujua lengo la mkutano mkubwa wa CDM Jangwani siku ya Jumamosi lilikuwa ni nini na kama lilifikiwa au la. Kuna uwezekano kulikuwa na malengo mbalimbali kama vile:

a. Kuanzia M4C kitaifa (ni marudi ya lile la Arusha ambalo nalo lilirushwa kitaifa?)
b. Kuwaambia wananchi kuhusu Katiba Mpya... (ilihitaji mkutano mkubwa?)
c. Kuwaeleza wananchi ubovu wa watendaji wa serikali (mbona kubadiilsha mawaziri ni ushahidi wa wazi)
d. Kupata wanachama wengi (idadi ya 3000 kama ilivyotangazwa ni kidogo sana kulinganisha kama ingeweza kufanywa kwa namna nyingine)
e. Kuchangisha fedha kwa ajili ya chama (za nini? zinachangia CDM taifa au CDM mahali?; zimepatikana kiasi gani hadi hivi sasa?)
f. x,y

Kwa maana ninaanza kutotaka kuona political acrobatics za kuvutia.. maana baada ya Jumamosi kupita leo Jumatatu na wiki hii watu hawa waliohamasishwa wanafanya nini? Na wale wa mikoani walikohamasishwa na wanakoendelea kuhamasika wanafanya nini baada ya kujiunga na mwamko wa mabadiliko a.k.a M4C?

Nitawasoma kisha nitatoa mawazo yangu - inshallah - kwenye toleo la Jumatano la gazeti..
Nina shukuru Mkuu Mwana Mwanankijiji kwa changamoto uliyo itoa, kwa maoni yangu naona lengo la CDM lilifikiwa kabisa maana wameonyesha wazi kuwa CDM ni ya Watanzania wote si ya kanda wala kabila wala dini ni kwa ajili ya wanyonge wote wanaonyanyaswa na serikali hii ya CMM. Wametoa mesegi kwa nchi nzima kuwa mageuzi kwenye capital city Dar pia yapo hai yanafukuta kuelekea nchi nzima, hayo ni mafanikio makubwa!!! Hivyo ni wazi ujumbe umefika na Watanzania wote watajua kuwa ukombozi unazidi kupamba moto!!! VIVA CDM, VIVA UKOMBOZI WA NYONGE, VIVA MAKAMANDA KUONYESHA DIRA!!!

MMJ ukifuatilia nyuzi zako kama sio zote basi ni nyingi mimi huwa sizichangiaji sababu ni moja tu, nimegundua unapenda attention ya watu humu ndani naninakushauri hiyo tabia uiache sababu wanaokuona kama unamawazo yenye busara wakaja gundua unacheza na kalamu kuziteka akili zao itakukosti sana.

CDM ni chama cha Upinzani chenye vichwa makini na mipangilio makini, kwataarifa yako hii mikutano ni moja ya mikakati ya ndani ya chama ambayo si kila wakati itolewe nje, majibu yake subiria utayapata.

Jibu moja wapo nihili la wewe kupanga kufungua Tawi la CDM huko uliko, mbona hukufikiria kufanya hivyo tangu zamani na ukatangaza jmosi? Yako mengi mengine tutamfaidisha Nape na Magamba kama unataka kujua ni-PM

Josephine03 hongera kwa hoja nzuri sana uliyoitoa hapo, Lakini mbona umetutukana?

Miaka minne iliyopita wakati najiunga humu JF, Mwanakijiji alikuwa hivyo hivyo! personally nimekifuza vingi kwake, kujenga hoja, kujibu hoja, na kuangalia mambo in 3D if not in 4D! lakini bado tumebishana, tumekosoana, tumejengana na this forums is all about that...to change someone the way u want somebody to be..that can be achieved only by hoja kwa hoja!

Kuwa CDM ni chama makini sio hoja hapa, hakuna aliyesema si chama makini.....ila umakini wa chama ni pamoja na kujibu hoja..ambazo wewe haujazijibu. Tatizo la kufikiri liko hivi.....kila mtu anaona anaweza kufikiri...mwingine akifiri kwa niaba yako au akaja na kile ambacho haukuwahi kufikiria unaona kama umekuwa betrayed na wale walio ku drag kufanya vitu pasi kufikiria..in the name of change! sasa mnajiandaa kushika nchi huwezi kujibu maswali madogo hayo hapo juu...unasema nyie chama makini

Tofauti yako na Nape ni nini sasa??

Paragraph ya mwisho umejaribu kujibu hoja...kwani ndicho kilichotokea jangwani..japo sicho kilichokuwa sababu ya ule mkutano!!?? right?? na ndio lengo la mtoa hoja..lengo lilikuwa ni nini na mlilifikia?

kwa chama makini kama chako, hii evaluation sheet ya mwanakijiji haikutakiwa kusubiri JF!! mlitakiwa kukaa huko huko na kuji-tathimini na ama ungekuwa umefanya hivyo, basi pengine ungekuja na report kamili ya your evaluation! ha ha ha!

Lakini kusema mwakajiji anacheza na akili za watu, sijui na kalamu na itakuja kum-cost is 'out of point statement' the statement is just hanging somewhere in air, haingii akilini wala haishikiki! edit that please!! acha kututukana watu na akili zetu-kuwa eti tunamwona ana mawazo ya busara, siyo tunamwona ana busara...ndivyo alivyo ana busara!!! mbona hata wewe unayo..mmetotofautiana viwango ila busara ya mwanakiji wengi wana ikubali! au haukubali wingi wa watu...kusupport kitu au mtu?? kwani pipoz pawa imeanzia wapi na how it works??

Ni kama unasema kwa sababu chadema inapendwa na watu wengi basi iwe makini inacheza na akili za watu na itakuja kuki-cost..kuwwa kinapenda attention ya watu..ha ha ha!!

katika walio makini wa chadema wewe haumo!! kwani si wewe ndiye uliyemkaribisha Shibuda na leo unataka kumfukuza, au umakini unapimwa katika nini??

haumini nguvu ya watu kukubali jambo au mtu! why are you in chadema anyway!

its morning!
 
Kuna kitu kimeanza kunisumbua katika kufikiria muendelezo wa mikutano mbalimbali ya CDM.. ili nisije kujikuta napotoka nimeonelea kwanza niulize kwa wale wenye kujua lengo la mkutano mkubwa wa CDM Jangwani siku ya Jumamosi lilikuwa ni nini na kama lilifikiwa au la. Kuna uwezekano kulikuwa na malengo mbalimbali kama vile:

a. Kuanzia M4C kitaifa (ni marudi ya lile la Arusha ambalo nalo lilirushwa kitaifa?)
b. Kuwaambia wananchi kuhusu Katiba Mpya... (ilihitaji mkutano mkubwa?)
c. Kuwaeleza wananchi ubovu wa watendaji wa serikali (mbona kubadiilsha mawaziri ni ushahidi wa wazi)
d. Kupata wanachama wengi (idadi ya 3000 kama ilivyotangazwa ni kidogo sana kulinganisha kama ingeweza kufanywa kwa namna nyingine)
e. Kuchangisha fedha kwa ajili ya chama (za nini? zinachangia CDM taifa au CDM mahali?; zimepatikana kiasi gani hadi hivi sasa?)
f. x,y

Kwa maana ninaanza kutotaka kuona political acrobatics za kuvutia.. maana baada ya Jumamosi kupita leo Jumatatu na wiki hii watu hawa waliohamasishwa wanafanya nini? Na wale wa mikoani walikohamasishwa na wanakoendelea kuhamasika wanafanya nini baada ya kujiunga na mwamko wa mabadiliko a.k.a M4C?

Nitawasoma kisha nitatoa mawazo yangu - inshallah - kwenye toleo la Jumatano la gazeti..

mkutano ulitangazwa zaidi ya wiki(kabla). ulikuwa na nafasi ya kushauri nini kifanyike. kwa hadhi yako nadhani ungesikilizwa, kuliko kusubiri watu wafanye jambo, then uanze kukosoa. huo ni uswahili.
 
Inawezekana unahitaji kufikirishwa zaidi,au kujua wengine wanaza nini,au kukosoa au pengine kuelimishwa. Yote mema kabisa!
Kusaidia tu kwenye kukufikirisha:
  1. Mosi naamini Lengo la wazi kabisa ambalo hata CCM hawafichwi ni kuhamasisha mabadiliko ya kifikra, za kisiasa hasa. Pengine unaweza kuja na smarter ways kama ulivyodokeza kwenye maswali yako,lakini hii ya juzi ilifanikiwa katika mazingira tuliyopo. (Tupo Tanzania). Hebu fikiri kwamba mikutano na maandamano yote iliyofanywa tangu enzi za NCCR mageuzi ya akina Mrema,Marando na lamwai mpaka juzi ISINGEFANYIKA, tungekua wapi leo?
  2. Wewe pamoja na wengine wengi wamedokeza kutokuwepo na haja ya kutoendelea kuelinisha uma na kujisafisha kutoka katika propaganda chafu za udini,ukabila,ukanda n.k. kwa kile kinachoelezwa kuwa "wananchi wamekwisha kuwaelewa tayari"...Pyuu! How much would be enough?
  3. Kama lengo ni kuelimisha wakati huu tukielekea kwenye kutoa maoni ya katiba mpya, nadhani limefanikiwa pia. Mmejaribu kudokeza kutokuwepo umuhimu wa kuwaita watu jangwani kwa hilo. Hivi mnafahamu ni watanzania wangapi wana mwamko wa kukaa walau kwenye TV kutazama mihadhara ya Prof. Shivji na vipindi vya akina Ulimwengu kuhusu katiba? Mnajua kati ya hadhira ya taarifa za habari na zile za tamthilia na soka zipi ni kubwa zaidi? Kibongo-bongo walifanikiwa nadhani
  4. Kuchangisha pesa?: Aa hili hata huko ulipo wanafanya bana,labda sie tulio mbali hatuelewi wanafanyaje hasa,lakini michango mingi ya kifedha ilikua ni moja ya chachu ya ushindi wa rally za Obama 2008. Kuna time bibi Clintoni ni kama alifulia vile..don't take me seriously in this.
  5. Kuongeza wanachama? Kama mkakati wa kitaifa lengo linakua ni kutia hamasa tu ya watu kuchukua kadi za uanachama na kwenda kufungua matawi huko makwao. Hili nalo nadhani lilifanikiwa japo litategemea sana utendaji katika ngazi za chini kuichukua hamasa ile na kupeleka mitaani na vijijini. Zile kadi 3000 ni token tuu,sidhani kama lilikua ndilo lengo hasa,ndo maana lilifanyika mwisho kabisa kama sikosei.

Hizi ni siasa jamani! Theories and practices might be confusingly contrasting!!!
 
WATU WANAFIKI SANA HAPA NDANI..HII THREAD INGEANZISHWA NA Ritz ANGETUKANWA MPAKA ATAPIKE!!!

Na ndo maana me sikuanzisha. Ningeazisha ningeambulia vipigo. Wengine wangetumia jina langu kama sehemu ya madongo. Utasikia oh we maamuma unajua nini! Kwahiyo naishia kuchangia nyuzi za 'wanaokubalika'.
 
Mwanakijiji, katika tathmini ni lazima uwe na goals au malengo yaliyowekwa kabla ya huu mkutano. Sasa wewe unapoleta hii mada bila kutueleza kwa kina malengo yalikuwa yapi, itakuwa ngumu kwetu kujua kama yalifikiwa.

Cha muhimu ulete malengo kutoka kwenye chanzo cha CDM kwa uhakika ili tuweze kuangalia kama malengo yalifikiwa.

Ila binafsi na kwa mtazamo binafsi naona positive effects kwenye jamii ya Dar na Taifa ilipatikana. Nilipata kitu kikubwa kuhusu mchakato wa katiba na katiba mpya, swala la muungano , kwa ujumla sehemu ya Tundu Lisu ilinigusa sana,

Pia niliona umoja wa kitaifa ukijengwa, usidhani kuna umoja wa remote management, umoja ni lazima watu wakutane na kushirikishana maisha.

Kusema nguvu iliyotumika yaweza kuwa kubwa sana sidhani kama ni kweli, kwani tuliitaji kukutana ili kuimarisha umoja. Pia hotuba ya Dr Slaa, Mbowe zote zilikuwa safi sana.
 
Back
Top Bottom