Hold on a minute!!.... Lengo la Mkutano wa Jangwani lilikuwa nini... lilifikiwa?

Mh! mimi nadhani kwa siasa zetu za kiswahili CDM walijitahidi kukusanya watu wengi ambao wote wanaonekana wanawaunga mkono! ilhali TV ikionyesha tukio hilo live kitu ambacho kinazidi kusisimua watu wengine ambao huenda walikuwa na mashaka na chama hicho!...

Naona ni vizuri kunoa zaidi mikakati ya chadema...., lkn nohofia mambo mawili, Kwanza kuwachanganya watz waliozoea siasa zetu hizi za kiswahili, Pili Tusije tukaiua kabisa CCM maana pia mbele ya safari tutaihitaji kama chama imara cha upinzani....tusitegemee kuendelea kuwa na viongozi wazalendo kama kina dr slaa..!(kwani hata ccm walikuwa na mvuto kama cdm sasa)

Nawasilisha!
 
Hili haliwezi kuwa lengo kwani uchaguzi wa 2010 ulishalithibitisha hilo na wapiga kura wa Tanzania walishakataa hoja hizo za ukanda na ukabila; au CDM wamesahau kuwa wamepata wabunge na madiwani kuanzia Kusini hadi Kaskazini, Mashariki hadi Magharibi? Mbozi, Maswa, Kiwira, Songea,? Wanataka kuthibitisha nini? So hili haliwezekani kuwa lengo kwani ni redundant.

Mimi nadhani walitaka kuendelea kum-prove wrong Kikwete kwamba kama vyama vya upinzani ni vya msimu basi Chadema siyo cha Msimu. Bado naendelea kutafakari malengo mengine ya mkutano ule ambao hata mimi nilihudhulia.
 
Afadhali umeniwakilisha ktk hili. Nami pia nilikuwa najiuliza vivyo hivyo. Lakini pia ningependa kutoa ushauri kwa CDM kwamba sisi watz wa vijijini ambao ni wengi tunahitaji sana elimu ya uraia ili tujitambue (sijui kwa mijini ingawa picha ya mkutano wa jumamosi imeonesha kwamba tuko kwenye 'mtumbwi' mmoja). Vinginevyo, pamoja na kuvuna wanachama wengi, haitakuwa na maana iwapo tutavua magamba ya mwili tu lakini fikra zetu bado ni zilezile za 'zidumu fikra za mwenyekiti'. Tunahitaji kufunguliwa na kuaminishwa kwamba tunahitaji mabadiliko na ni mabadiliko ya namna gani na kwamba sisi wenyewe ni sehemu ya mchakato wa mabadiliko. Picha niliyoipata jumamosi haitofautiani na iliyoko vijiji vya huku kwetu, kwamba mabadiliko yataletwa na viongozi. Tunashangilia kwa nguvu zote mikutanoni lakini baada ya hapo tunayaacha hapohapo na kama tunaondoka na kitu basi ni kuelezana namna mlivyokuwa mkitiririsha vina jukwaani. Uchaguzi ukifika mnajua kinachotokea. Ni kwa sababu imani ya wananchi kwa CDM haikulelewa. Niliona jumamosi walalahoi wenzangu wanashangilia lakini kwenye mambo ya msingi wa ukombozi wao walikaa kimya, ilinionesha hawakuelewa. Kwa hiyo kazi bado ni kubwa. Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa ila naamini ktk mabadiliko. Natamani kuendelea lakini simu ya mchina inanitesa.
Maamuma hapa pana kitu kingine umekisema na mimi nakichukulia kwa umakini zaid.. je kweli CDM wametoa elim ya uraia ya kutosha kwa watu? hili likifanikiwa naamin watakuwa pia wameuza sera zao kwa watu kitu ambacho ni cha muhimu sana.

Binafsi nilitegemea waje wakituelezea sera kama vile za uchumu hali ilivyo na wao katika hili wamejipangaje na watatumia mbinu gani. tena wasituhadae watoto wetu watasoma bure bali watuonyeshe uwezo tutakao jengewe wa sisi kuweza kuwasomesha watoto kuliko kuitoa bur hii elimu.

kadhalika haya wangefanya kwenye afya, utumish wa umma, uwekezaji nk. Hivi sasa wao kama wana kitu kimoja tu basi kinabaki kuwa wimbo badala ya kukiweka in a way kwamba kitatumikaje katka kujenga hili taifa.

Mthalan tumeona wakilala mikia sana ishu za ufisadi hata kupelekea watu kuwajibishwa lakin CDM hawajatuambia sera na ilani zao zinaasemaje juu ya ufisad na watakabiliana nao vipi. siamini katika utatuzi wa tatizo bali naamini katika kuzuia tatizo lisitokee.
 
Last edited by a moderator:
inamaana Mwanakijiji huoni if there is something gained by CDM from the meeting? Do you mean CHADEMA's Popularity in Dar is just the same as it was before the meeting?

Do you mean the 'fear' that CCM has on CDM is just the same as it was before the meeting?

Ma bro Mlachake popularity siyo bid deal kwani CDM haiitaji kusmama jangwani kujitangaza, kwani watu wanaijua vizuri kwani kuna mtanzania mpenda siasa au mfuatiliaji asiye jua kilianzishwa na edwin mtei?

au je unafikiri CCM hawahofii upinzani? ingekuwa hawahofii wasingefanya kampeni au kujitetea wanapoguswa so sidhani kama haya yana mantiki kwenye hili la M4C. Unless you convice us otherwise
 
Last edited by a moderator:
kama lengo lilikuwa ni kufanyia mkutano dar basi limefikiwa, kama lengo lilikuwa ni kupima upepo na mwitikio wa watu wa dar basi limefikiwa(kumbuka watu waliacha kwenda kuangalia soka uwanja wa taifa wakaenda mkutanoni), kama lengo lilikuwa kujenga awareness kwa watu wa dar nalo lilifikiwa maana dar ni sehemu ambayo wengi huwa hawaiamini.huo ni kwa mjibu wa mtizamo wangu but je malengo yao kama chama yamefikiwa kwa kiasi gani na je huwa wanajitasmini baada ya mkutano na kama uwa wanajitasmini ni kwa vipimo gani? kiukweli unachojaribu kukisema mm ni kuwa si kila mala watu wafanye tu mikutano ambayo haina tija, ni lazima kila linafanywa liwe linapimwa na kuelezeka, yaani pawepo na matokeo yanaoonekana.
 
Lengo lilikuwa ni kuitangaza Vodacom Mpesa.

Rostam Aziz ni kichwa hapana mchezo, unaijuwa "Hap Ki Do", ni kutandikwa kwa nguvu zako mwenyewe!
 
Kimsingi malengo yalifikiwa, japo si 100% yamesemwa sana kuwa Cdm ni ya kikabila, ni ya kikanda yaani kaskazini hususa wachaga. Na walisema haikubaliki pwani, Dsm na kusini, sasa waliwadhihirishia wabaya wao kuwa Cdm ni ya Watanzania wote, bila ya kujali kabila, dini, ukanda wala jinsia, na iko tayari kushika dola 2015. Mungu ibariki CHADEMA.

Mkuu kama lengo lilikuwa hilo jua Dar es Salaam si kipimo muafaka.
 
Kuna kitu kimoja tu nilisikia nacho ni kuhamasishana kufungua matawi na mashina ya CDM; hilo tu lakini yale ya Lema kupita na kapu kukusanya pesa ilikuwa kama sadaka vile!
 
Kimsingi malengo yalifikiwa, japo si 100% yamesemwa sana kuwa Cdm ni ya kikabila, ni ya kikanda yaani kaskazini hususa wachaga. Na walisema haikubaliki pwani, Dsm na kusini, sasa waliwadhihirishia wabaya wao kuwa Cdm ni ya Watanzania wote, bila ya kujali kabila, dini, ukanda wala jinsia, na iko tayari kushika dola 2015. Mungu ibariki CHADEMA.

Hata haya maswali ni sehemu ya mafanikio. Mbna lengo mojawapo lilikuwa kuibua mjadala ktk jamii kuhusu mabadiliko ya katiba, M42 na mengine.
 
Ndugu Mwanakijiji, political landscape ya TZ ni vigumu kweli kuipima na kuielewa. Hatuna opinion polls, ambazo kwa kiasi kikubwa hutumika kwenye nchi zilizoendelea kupima matokeo hata ya single events kama mkutano. Kipimo kizuri huwa kinakuwa wakati wa uchaguzi, kama utakumbuka watu walibeza sana oparesheni SANGARA, lakini matokeo yake yalionekana 2010.

Getting back to the main agenda, mafanikio yapo in the sense that watu wameweza kukumbushwa mambo kadhaa muhimu.

1. CDM sio chama cha kidini wala kikanda. Hili jambo kama ulivyosema lilijibiwa vizuri tu kwenye uchaguzi 2010, lakini bado CCM na washirika wao bado hawataki kuliacha liende kimya. Ni muhimu likazungumzwa tena na tena nafasi inapopatikana.

2. Nafasi ya katiba kwenye ustawi wa maisha na matumizi mazuri ya rasilimali zetu. La muhimu zaidi ni hili forbidden ghost called MUUNGANO. Kama unavyosikia chokochoko zimezidi upande wa pili huku kwetu CCM inawaambia watu wakae kimya!!

Lakini kama nilivyosema awali, ni vigumu kupata quantitatively ni kiasi gani imefanikiwa. Kupata watu wengi pale Jangwani plus wengine wengi zaidi kuangalia, hakukwenda bure.
 
Kuna kitu kimeanza kunisumbua katika kufikiria muendelezo wa mikutano mbalimbali ya CDM.. ili nisije kujikuta napotoka nimeonelea kwanza niulize kwa wale wenye kujua lengo la mkutano mkubwa wa CDM Jangwani siku ya Jumamosi lilikuwa ni nini na kama lilifikiwa au la. Kuna uwezekano kulikuwa na malengo mbalimbali kama vile:

a. Kuanzia M4C kitaifa (ni marudi ya lile la Arusha ambalo nalo lilirushwa kitaifa?)
b. Kuwaambia wananchi kuhusu Katiba Mpya... (ilihitaji mkutano mkubwa?)
c. Kuwaeleza wananchi ubovu wa watendaji wa serikali (mbona kubadiilsha mawaziri ni ushahidi wa wazi)
d. Kupata wanachama wengi (idadi ya 3000 kama ilivyotangazwa ni kidogo sana kulinganisha kama ingeweza kufanywa kwa namna nyingine)
e. Kuchangisha fedha kwa ajili ya chama (za nini? zinachangia CDM taifa au CDM mahali?; zimepatikana kiasi gani hadi hivi sasa?)
f. x,y

Kwa maana ninaanza kutotaka kuona political acrobatics za kuvutia.. maana baada ya Jumamosi kupita leo Jumatatu na wiki hii watu hawa waliohamasishwa wanafanya nini? Na wale wa mikoani walikohamasishwa na wanakoendelea kuhamasika wanafanya nini baada ya kujiunga na mwamko wa mabadiliko a.k.a M4C?

Nitawasoma kisha nitatoa mawazo yangu - inshallah - kwenye toleo la Jumatano la gazeti..

MMM, ni swali zuri sana ambalo ata mini nimekuwa likinisumbua sana!

nilichokiona pale ni kwamba viongozi wa CDM wanatumia njia ya mob psycology kugain popularity ambayo kwa kiasi kikubwa watu wenye nguvu kama vijana ni rahisi sana kuwateka, lakini nachelea kusema kama ni mkakati endelevu, niseme ni mkakati hatari sana kwa chama kinachotegemea kushika dola, kwani watu hawa ni hatari sana hawachelewi kukusau kabs kama umewahi kuwafanyia lolote. CDM inacheza na kizazi cha hatari sana katika siasa, ambacho kinatatak kuona mabadiliko, (inovationa) si kuambiwa tuu kwenye majukwaa.... vitendo hasa ndio wanataka. tofauti na wazee wa wenzetu NYINYIEM, ambao afta all wamebakisha muda kidogo kumaliza muda wao hapa duniani, so wanahitaji kuona wanamaliza vizuri tifauti na vijana ambao wataka kuona future YAO.

Nilitegemea tungepewa feedback ya trial ya Arusha ilikwendaje (tulihitaji feedback) sio one way communication! hii itatuangusha, VIJANA wetu wengi tunamatumaini makubwa sana na CDM ndo maana hata kama wamekosea utakuta mtu yuko tayari kukataa kabs kama chama komekosea wakitumaini kwamba sio hulka yao na kabda watabadilika kesho!! na hoja ya leo ndo itakufa (HII VIONGOZI WA CDM wasipokuwa makini na strategy zao) tumekwisha.

Kuhusu mob pycology inatakiwa kwa kuanzia lakini sio kama mkakati wa kuendeleza (this is very wrong) MM, umeuliza swali zuri sana kuwaambia watu kuhusu katiba je ilihitaji mkutano mkubwa? jibu no NO NO!!! viongozi wetu wasitumie mikakati ya zamani mimobilize morden age!! tuende kisasa zaidi na kuwa na inovative na mambo yetu. Tuwe watu wa vitendo zaidi kwani tungeweza kutumia mkutano wa CDM square kwa lengo moja tu just kutoa feedback ya mambo ya msingi wananchi waliyoshirikishwa na kutoa strategy ahed ili wachama washiriki kama inabidi

nafikiri niishie hapa
 
Ma bro Mlachake popularity siyo bid deal kwani CDM haiitaji kusmama jangwani kujitangaza, kwani watu wanaijua vizuri kwani kuna mtanzania mpenda siasa au mfuatiliaji asiye jua kilianzishwa na edwin mtei?

au je unafikiri CCM hawahofii upinzani? ingekuwa hawahofii wasingefanya kampeni au kujitetea wanapoguswa so sidhani kama haya yana mantiki kwenye hili la M4C. Unless you convice us otherwise
gfsonwin ulienda kwenye ule mkutano? Nafikiri kila mwananchi aliyeenda pale anaswali kwa kamati ya katiba mpya kuhusiana na masuala ya Muungano. Lisu alitumia lugha nyepesi ambayo nahisi wengi tulimuelewa.

Tatizo la ule mkutano lilikua on time management.

Kumbuka ungewaambia watanzania wafike pale saa sita ungeishia kuhutubia watu 10.
 
Last edited by a moderator:
Kuna kitu kimoja tu nilisikia nacho ni kuhamasishana kufungua matawi na mashina ya CDM; hilo tu lakini yale ya Lema kupita na kapu kukusanya pesa ilikuwa kama sadaka vile!

Ile sadaka na mimi ilishangaza ingawa si sana. Utaratibu wake haukunivutia na hasa kutoka kwenye chama kinachoaminiwa kuwa makini na cha kisasa zaidi. Sisi huku vijijini sadaka hatuna!
 
tukianza ku rate the extent of success nadhani kila mmoja atakuja na jibu lake.
hapa nadhani CDM wanachofanya ni kuhakikisha lengo la kisiasa linatimia. hii ni strategy mojawapo. so, nakubaliana nanyi kwamba kukipa maoni pale ambapo tunaona mambo si sawa(kama political analysts) ni vema sana ktk kukikomaza chama. ahsante
 
Kila mchangiaji hapa anasema alikuwa na wazo kama Mzee Mwanakijiji Mkutano ulikuwa juzi walikuwa wapi wasilete thread kama hiyo jana au leo kabla ya Mzee Mwanakijiji jamani tusiwe tukidandia thread kwa kusema mlikuwa mnafikiria kama yeye kwa vile anaheshimika sana hapa jamvini . Mzee Mwanakijiji mimi nakuheshimu lakini ukileta tena thread ya kutuvunja moyo kama hii naona utanitafutia ban tena ambayo iliisha jana. nilipewa ban ya siku 90 kwahiyo naomba uachane na hii thread haraka
 
Ulikuwa humjui huyo, muulize Ribosome!
 
MMJ ukifuatilia nyuzi zako kama sio zote basi ni nyingi mimi huwa sizichangiaji sababu ni moja tu, nimegundua unapenda attention ya watu humu ndani naninakushauri hiyo tabia uiache sababu wanaokuona kama unamawazo yenye busara wakaja gundua unacheza na kalamu kuziteka akili zao itakukosti sana.

CDM ni chama cha Upinzani chenye vichwa makini na mipangilio makini, kwataarifa yako hii mikutano ni moja ya mikakati ya ndani ya chama ambayo si kila wakati itolewe nje, majibu yake subiria utayapata.

Jibu moja wapo nihili la wewe kupanga kufungua Tawi la CDM huko uliko, mbona hukufikiria kufanya hivyo tangu zamani na ukatangaza jmosi? Yako mengi mengine tutamfaidisha Nape na Magamba kama unataka kujua ni-PM
 
I expected a lot from Chadema lakini sikuona lolote jipya, labsa sana sana kusalimia wananchi tu na wengine wakapata fursa kuwaona kwa macho watu waliokuwa wanawasikia kwenye vyombo vya habari!
 
Kuna kitu kimeanza kunisumbua katika kufikiria muendelezo wa mikutano mbalimbali ya CDM.. ili nisije kujikuta napotoka nimeonelea kwanza niulize kwa wale wenye kujua lengo la mkutano mkubwa wa CDM Jangwani siku ya Jumamosi lilikuwa ni nini na kama lilifikiwa au la. Kuna uwezekano kulikuwa na malengo mbalimbali kama vile:

a. Kuanzia M4C kitaifa (ni marudi ya lile la Arusha ambalo nalo lilirushwa kitaifa?)
b. Kuwaambia wananchi kuhusu Katiba Mpya... (ilihitaji mkutano mkubwa?)
c. Kuwaeleza wananchi ubovu wa watendaji wa serikali (mbona kubadiilsha mawaziri ni ushahidi wa wazi)
d. Kupata wanachama wengi (idadi ya 3000 kama ilivyotangazwa ni kidogo sana kulinganisha kama ingeweza kufanywa kwa namna nyingine)
e. Kuchangisha fedha kwa ajili ya chama (za nini? zinachangia CDM taifa au CDM mahali?; zimepatikana kiasi gani hadi hivi sasa?)
f. x,y

Kwa maana ninaanza kutotaka kuona political acrobatics za kuvutia.. maana baada ya Jumamosi kupita leo Jumatatu na wiki hii watu hawa waliohamasishwa wanafanya nini? Na wale wa mikoani walikohamasishwa na wanakoendelea kuhamasika wanafanya nini baada ya kujiunga na mwamko wa mabadiliko a.k.a M4C?

Nitawasoma kisha nitatoa mawazo yangu - inshallah - kwenye toleo la Jumatano la gazeti..

Natofautiana na wewe, hapa malengo yamefikiwa sana, tena sana. Kwa Dar CDM imetikisa!
 
MMJ ukifuatilia nyuzi zako kama sio zote basi ni nyingi mimi huwa sizichangiaji sababu ni moja tu, nimegundua unapenda attention ya watu humu ndani naninakushauri hiyo tabia uiache sababu wanaokuona kama unamawazo yenye busara wakaja gundua unacheza na kalamu kuziteka akili zao itakukosti sana.

CDM ni chama cha Upinzani chenye vichwa makini na mipangilio makini, kwataarifa yako hii mikutano ni moja ya mikakati ya ndani ya chama ambayo si kila wakati itolewe nje, majibu yake subiria utayapata.

Jibu moja wapo nihili la wewe kupanga kufungua Tawi la CDM huko uliko, mbona hukufikiria kufanya hivyo tangu zamani na ukatangaza jmosi? Yako mengi mengine tutamfaidisha Nape na Magamba kama unataka kujua ni-PM

Kuna Chadema damu na chadema asili nishagundua...
 
Back
Top Bottom