Hoja za uamsho hazitozimwa na mabomu ya machozi

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Hoja yangu


Lula wa Ndali Mwananzela

Toleo la 244
20 Jun 2012
















KIKUNDI cha uamsho cha Zanzibar pamoja na makundi kadhaa yanayopinga Muungano kinasema Tanganyika inaidhulumu Zanzibar.
Baadhi ya wahubiri wake wanaenda mbele zaidi na kudai kuwa Tanganyika imeigeuza Zanzibar kuwa koloni lake. Baadhi ya wahubiri wengine wanaenda mbele zaidi na kudai kuwa matatizo mbalimbali ya kiuchumi na hali ya wananchi wa Zanzibar yanatokana na kuminywa kunakofanywa na Serikali ya Muungano ambayo ndiyo “Serikali ya Tanganyika” vile vile.
Wanasema kwa ufupi kuwa Muungano ulivyo sasa unaionea Zanzibar na unaibana kama koti linavyombana mtu na sasa wakati umefika kwa koti hilo kuvuliwa.
Wanajenga hoja nyingi sana za jinsi gani Zanzibar inadhulumiwa; kuanzia muundo, mgawanyo wa mapato, suala la mafuta, OIC, mambo ya misaada ya kigeni na hata nafasi mbalimbali za utumishi wa Muungano. Hoja zao ziko wazi na wala hazina kificho.
Wanazitangaza hoja hizo kwenye makongamano na kwa kweli si hoja mpya. Ni hoja hizi hizi ambazo ziliwahi kumletea matatizo Mzee Aboud Jumbe, na ndizo hizi hizi kwa namna yake ziliwaletea matatizo kina Shaaban Mloo na wengine. Ni hoja hizi hizi ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara.
Ni mara moja tu kiongozi wa Bara aliwahi kusimama hadharani na kujibu hoja hizi bila kutumia virungu. Mwalimu Nyerere mara zote aliwashughulikia viongozi wa kisiasa wa hoja hizi. Aliwashughulikia kwa sababu wale walioapa kulinda Muungano hawawezi kukaa kimya wakati Muungano unatishiwa na bado wao wakakinga mikono ya kupokea mishahara, posho na mapochopocho ya Muungano!
Nyerere aliwajibu wale wa Tanganyika waliotaka serikali ya Tanganyika katika lile kundi la G55 lililoongozwa na Njelu Kasaka. Na hata hoja ilipofika hadi bungeni Nyerere alijitokeza na kuwajibu na kudai wazi kuwa serikali yetu (ya Muungano ikiongozwa na Mwinyi na Malecela) “imesurrender” yaani imesalimu amri.
Nyerere alionyesha vizuri kabisa kwa mazungumzo yake lakini zaidi kwa kijitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania. Katika kitabu hiki Nyerere alichambua hoja mbalimbali zilizotolewa kuhusu Tanganyika na kwanini zilikuwa ni hoja dhaifu japo zilikuwa zinavutia na yeye peke yake aliweza kunyamazisha kelele za “Tunataka Tanganyika”.
Ukweli ni kuwa hoja zile za kwenye kitabu kile bado zinasimama na hadi leo hajatokea mwanasiasa Tanzania (awe mzee au kijana) ambaye amewahi kuzionyesha upungufu wake ama wa kihistoria au wa kimantiki.
Nyerere hakutumia nguvu kuzima hoja alitumia hoja kuzima nguvu! Leo hakuna hilo.
Tunashuhudia Visiwani Zanzibar leo hii mwamko wa kuitaka “nchi yao” ukipamba moto lakini mwamko huo unaenda sambamba kabisa na madai ya kuibebesha lawama Tanganyika na Watanganyika. Kwamba ni Tanganyika ndiyo sababu ya kudumaa na matatizo ya Zanzibar na si yale tu ya kiuchumi bali hata ya kimaadili.
Kinachoshangaza na kuchekesha, hajatokea kiongozi yeyote ambaye amewahi kusimama na kujibu hoja hizi zaidi ya kuzidharau, kuwapiga mkwara na sasa inaonekana hata kujaribu kujibu hakutajaribiwa tena kwani FFU na vyombo vingine vya usalama ndio vitazima hoja kwa nguvu! Wanasiasa wetu wameshindwa!
Ndiyo maana binafsi naamini kuwa kwa vile viongozi wetu wameshindwa kujibu hoja za uamsho hakuna sababu tena ya kutumia vyombo vya usalama kutawanya watu.
Kama mashehe na viongozi wengine (kama kina Raza na Seif Sharrif) wanaamini kuwa Muungano haufai na wako upande wa Uamsho watoke na wawe wa kwanza kutaka Wazanzibari waamue wenyewe kupiga kura ya maoni. Ni kuchezea watu akili leo kina Seif wanasema ati “Watu wazungmzie Muungano” wakati kinachozungumzwa si “Muungano” tena bali ni “utengano”.
Kina Seif, Raza na viongozi wengine wa Wazanzibar wawe wa kwanza kusimama na kutaka “Utengano” kama wanavyofanya watu wa Uamsho. Lakini wasifanye hivyo wakiwa kwenye vyombo ambavyo wao waliapa kulinda Katiba Muungano! Haiwezekani!
Kama kuna Mwakilishi yeyote au Mbunge yeyote ambaye anataka Zanzibar ijitenge atakiwe kuachia ngazi kwanza ili awe mpigania “uhuru” wa Zanzibar. Hawawezi kuwa kwenye vyombo vya Muungano au kuapa kulinda Muungano halafu pembeni wanataka utengano! Ni matumaini yangu watakuwepo wabunge mahiri ambao watawaambia hili waziwazi kwamba tumechoka kutishiwa nyau! Kama Wazanzibari na viongozi wao wanataka kutoka kwenye Muungano hawahitaji tena mihadhara wala mikutano, wanahitaji tu kujiuzulu nafasi zao katika Muungano au zile ambazo waliapia kutii Katiba ya Muungano halafu waamue kutoka kwenye nafasi hizo.
Na wanaweza kwenda mbali zaidi na kutunga sheria (huko Zanzibar) ambayo itawatakataza Wazanzibar kushika ajira yoyote kwenye vyombo vya Muungano. Kina Jussa wanaweza kuleta mswada wa aina hiyo ili kuwazuia Wazanzibar kukubali cheo au wadhifa wowote kwenye vyombo vya Muungano ikiwa ni ishara ya kuukataa Muungano huo.
Lakini pamoja na sheria hiyo wale wanaotaka Muungano uvunjwe wawashawishi wawakiilshi wanaokutana Zanzibar ambao wengine wamesema hawataki kuburuzwa au kutishwa, watunge sheria ya kura ya maoni ili kabla ya mwisho wa mwaka huu Wazanzibari wapige kura ya kutoka kwenye Muungano au la. Muda wa kuzungumzia “muundo wa Muungano” umepita! Sasa tunataka watu waamue “uwepo wa Muungano”.
Kwa sisi wa Bara na wale ambao tunaamini tunawapenda sana Wazanzibari ambao ni ndugu zetu kiasi kwamba hatuwezi kuwang’ang’ania tunaendelea kutia msisitizo Let Zanzibar Go!
Iacheni Zanzibar iende. Wanaofikiria kuwa kuvunjika kwa Muungano kutavihamisha visiwa vya Zanzibar kutoka vilipo waendelee hivyo hivyo. Zanzibar ikitoka kwenye Muungano haitajisogeza mbali na Tanganyika na kwa mtu yeyote mkweli anajua kabisa kuwa huwezi kuishi kwenye taifa kubwa na lenye nguvu ya kila hali kama Tanganyika bila nchi yako kupata shida. Wazanzibari hata watoke kwenye Muungano wataendelea daima kukaa kwenye kivuli na uangalizi wa Tanganyika. Huu ni ukweli.
Kwa vile tunalijua hili hatuna shida hata kidogo kwa Wazanzibari kujitoa. Hivi ndugu katika familia akiamua kujitenga na familia itakuwa na maana kwamba damu ya familia yake haipiti kwenye mishipa yake? Wazanzibari hata wajitenge kesho (ingekuwa afadhali) bado watabakia kuhusiana na Watanganyika.
Sultani Jamsheed na serikali yake walijaribu kuwafukuza watu wa Bara ambao waliona ni tatizo kwao lakini mwisho wa siku ni wao waliofukuzwa.
Leo hii wanaoeneza chuki dhidi ya Watanganyika wasipoangalia wao ndio watavikimbia visiwa vya Zanzibar kwani wapo Wazanzibari ambao wanajua historia yao ilivyofungamana na Tanganyika. Hawa wamekaa kimya wanawaangalia. Watakapoamka historia inaweza kujirudia tena. Watawala wafikirie.
 
Muandishi mtowa Mada nakala yako mzuri na yenye msisimuo lakini kuna Mambo mawili tu uniweke sawa Jee Sultani Jemshini na Ali Hassan Mwinyi,Jumbe,Karume Yupi ni Mzawa wa Zanzibar na yupi ni mgeni wakuja sio wa Kuzaliwa ?.a.
B . Jee Seif Sharifu na Jussa na Raza wanahusika vipi na kiapo cha Katiba ya Muungano wakati wao ni wajiriwa wa Katiba ya Zanzibar isio ya Muungano ya 1984?.
 
Kwani zaidi ya muungano nini tena wanataka achieve ?kwani wale watoto wanaorandaranda beach ni issue ya muungano?Au mtaji wao kuleta fujo baadaye? Mbona mateso kwao yameanza kabla ya muungano?Na maisha duni kwa waislam ni dunia mzima,kuanzia India,china, Ulaya, US, na kwingineko?
 
Bora kuwa maskini wa mali kuliko kuwa maskini wa akili, Hivi ni lini bara wamewazuia kujitoa kwenye muungano?
 
wakiijua kweli na kweli kuwaweka huru waatacha.Shida wanaogopa kweli.
 
Lula Mwananzela.

Kumbuka kuwa uandishi ni taaluma tena ni taaluma makini sana sio ya kudakia dakia na kujaza chuki miongoni mwa jamii. Kumbuka kuwa Mwandihi ni yule anaye anayefanya utafiti kabla kuandika makala.

Makala yako ujafanya uchunguzi wala utafiti wowote bali imeongozwa zaidi na hisia na chuki zako dhidi ya jumuiya hii na kutaka kufitinisha jamii za Kiznz.

Pole sana
 
Back
Top Bottom