Hoja za sugu kwenye ant-virus

jouneGwalu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,687
1,767
Mnamo katikati ya mwaka 2010, EMCEE mkongwe na miongoni mwa waasisi wa HIPHOP hapa Tanzania ndugu Mbunge Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II(sugu) kwa kushirikiana na ma-EMCEE wengine wa hiphop wa hapa nyumbani ie Vinega & Kiraka, waliachia "mixed tape" iliyokwenda kwa jina la Ant-virus.
Nimeona sio vibaya nikishiriki na wanajamii kuhusu kile alichokipigia kelele sana SUGU katika mixed tape hiyo, ambacho mimi nimekiona ni kama hoja za msingi kuelekea ujenzi wa soko imara la mziki wa hiphop.
Msingi mkubwa wa kufanyika kwa kazi ile kama wenyewe (sugu, viraka na vinega) walivyosema ni kuwachana "radio ya wafu" kutokana na usimamizi wao wa kazi za kimuziki na hicho kituo cha radio kuwa zaidi ya radio ya kawaida na zaidi kujipa kazi ya wakala wa wasanii kitu ambacho kinaondoa ushindani uliosawa miongoni mwa wasanii kwa wasanii,
Katika hilo Sugu ameendelea kuwachana "cl**ds fm" kwa kuwa na kiherehere cha kujikabidhi haki ya kuwasemea wasanii, ndio maana eti “Ruge Kahaba” alikuwa anataka kuanzisha chama cha wasanii, wakati yeye (kahaba) ndio chanzo cha muziki huo kukwama, hii ipo kwenye nyimbo “I wanna kill right now” .
Pili, suala la maslahi ya wasanii. Kwasasa ni ipo wazi sana kuwa wasanii hawanufaiki na kazi zao. Katika hili Vinega wamezungumzia kuhusu malipo kwa nyimbo zinapopigwa redioni na zinapotumika kwenye matangazo mbalimbali, na uzingatiaji wa sheria ya haki miliki. Pia Vinega walizungumzia kuhusu ustawi wa wasanii katika maisha yao ya kilasiku huku wakitilia shaka nia ya wadau, wanasema “…hamtaki tujenge nyumba, mnataka tupange chumba”
Tatu ni mizengwe kwenye tuzo, mfano ni kwenye ile track ya Kiraka Coin Moko anasema “……acha nizime redio basi niwashe tv,CORA hajaenda Enika, namwona Ruge na Jaydee…..”. Kwenye hili la mizengwe pia Vinega walisema kuhusu upendeleo unaotolewa kwa kuzingatia studio ambayo msanii amerekodia badala ya uwezo wa msanii na producer husika katika ubora wa kazi.
Hoja ya kuwagawa wasanii, pia hili wamelizungumzia kwenye track “am so fly”, kwamba wasanii wanaopatiwa promo kwa muda husika na “radio ya wafu” hawaelewani (wanajengewa uadui) na wasanii waliotemwa na ambao wanaonekana kutaka kuleta fikra mpya katika uendeshaji wa soko la muziki.
Kupangia wasanii aina ya muziki wa kufanya kwa kuwaaminisha kuwa staili flani haiuzi, hii imeainishwa kwenye track “anti-virus” Kinega anasema “…..unamlazimishaje punda kunywa maji, chana wewe basi tuone kama unakipaji…”
Katika track hiyo hiyo Kinega anabainisha kuwa mtaani bado kuna hazina kubwa sana ya vipaji, kinega anaainisha “….. toka kitambo mi nachana machizi wananikubali, Jay hajatoa wimbo wa zali la mentali…….. kabla Ruge bongo hajatua…..”
Nguvu ya watangazaji kuburuza wasanii, hili limezungumziwa kwenye track kadhaa, hasa “I wanna kill” ya Sugu alizungumzia suala la watangazaji kuwanyonya wasanii kwa kuwataka watoe hela ili nyimbo zao zipigwe redioni, pia watangazaji kuongea na kuendesha vipindi vya redio vya kuwaponda wasanii ambao wao hawawapendi na kuwasifia wale ambao wao wanawapenda badala mashabiki ndio wawe mahakimu wa mwisho.
Na mwisho ila sio kwa umuhimu wake ni kituo cha radio “wafu fm” kujaribu kuwa chombo cha propaganda, na kuwa zaidi ya radio ya kawaida kwamba hapohapo inatangaza hapo hapo inajiingiza kwenye udau wa kuratibu kazi za kisanii kama tuzo na kumiliki wasanii na kikundi cha sanaa (THT) na mpaka kwenye soko kwa wahindi.
Kwa kuhitimisha, kazi ya muziki duniani bila kujali aina ya muziki ni inalipa sana kwa wasanii husika. Tunao mfano mzuri sana kwa kinachoendelea Uganda, wasanii wake wengi wamekuwa matajiri sana ukilinganisha na kabla ya kuanza kazi ya usanii mfano na Bobi Wine, japo wapo wengi sana. Sugu amekuwa katika harakati za kutaka kurekebisha hali hapa kwetu kwa wasanii wetu sema kwa sababu ya watu ambao inaonekana wananufaika na mfumo huu gandamizi wa sasa ambapo hali yake halisi ni kama nilivyoelezea hapo juu. Binafsi nakumbuka harakati za Sugu toka “HIPHOP SUMMIT”, Lakini mwisho siku sababu kama alivyosema FidQ kwenye track yake ya Propaganda “….. tunaachiana sababu hatujajuana, hatujajuana sababu tunatengana, tunatengana sababu tunaogopana……”
Kwa maana hiyo hili ni suala la wadau wote ila sana ni wasanii kwa ujumla wao, Sugu peke yake hataweza.
Pamoja na hayo bado harakati zake zinafahamika na kama aliweza kuwaweka pamoja Viraka na Vinega, nadhani atafanikiwa kuwaweka tena wasanii wote pamoja kama alivyofanikiwa kwenye "hiphop summit"
 
nakubaliana na mawazo yako as well as ideas ktk albamu ya antvirus, ila mbali na matatizo yaliyoainishwa hapo ila wasanii wenyewe ambao ni wadau wanachangia sana kupunjwa haki zao kwa sababu zifuatazo:
1. Wasanii wengine ni njaa kali kwa hiyo hawana hata muda wa kuburgain wao mradi wameckia hela mf. Kuna line moja ktk lyric za chidbenz ila ckumbuki ni song gani aliimba ''heri kidogo kitu kuliko kukosa kitu'' sasa hebu imagine msanii tena wa hiphop anakua na ideas hizo kweli tutafika.
2. Wasanii Tz wanaoimbia mziki kazi au mziki maisha ni wachache mno wengi wanaimba kupata mademu na umaarufu so wakishapata hivo na hela za bia 2 wanaridhika, aina hii wako wengi iko siku ntawachana humu ndani na tabia zao.
3. Elimu, siku hizi muziki umekuwa ni kazi ya walioshindwa shule hili si sahihi wako wasanii wachache wenye elimu na hao wanafanya vizuri hata kama sio maarufu hawaburuzwi na wale wanyonyaji
4. Ushirikiano, wanamziki hawana umoja kila mmoja anajiona bab kubwa wkt hamna kitu wangekuwa na umoja wangewza goma nyimbo zao zisipigwe bure pia kugomea show ambazo wanalipwa kiduchu na msanii wa nje analipwa mamilioni ni hayo tu
Ila pia tatizo ni Bongo flavour nafkiri nimeelewka
HipHop maisha, ramani, hiphop shule hiphop nguzo, na hao makuzi wanajua thats y wanaipiga vita wasanii wa hiphop wakikomaa ile ile mbona hali inabadilika! Achaneni na hawa masharo b ni mabwabwa, wanagawa kama bint kidawa.
 
Kwa sauti ya andiko lako, nimejua tupo pamoja katika harakati za hiphop. Zaidi nikushukuru kwa kuongezea minofu katika hoja za Sugu ambazo mi nimejaribu tu kwa kiasi fulani kuziwakilisha.....
Kitu ambacho kinaumiza sana ni kwamba misingi imeharibika sana na wanaoharibu bado ndio wanaendelea kujitangaza kama ni wadau wakuu wa muziki huo ilhali wao ndio "..... chanzo cha muziki kukwama"!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom