Hoja za Mwalimu Nyerere kupinga serikali tatu Tanzania

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Nchi mbili zinapoungana na kuwa Nchi moja mifumo ya kawaida ya miundo ya Katiba ni miwili: Muungano wa Serikali Moja, au Shirikisho la serikali Tatu. Kwa mfumo wa kwanza kila nchi itafuta serikali yake na nchi mpya inayolizaliwa itakuwa ni nchi moja yenye Serikali moja. Katika mfumo wa pili kila nchi itajivua madaraka ambayo yatashikwa na serikali ya shirikisho na itakuwa na serikali ambayo ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yaliyobaki.

Mambo yatakayoshikwa na serikali ya Shirikisho ili yale ambayo yatashikwa na serikali ya shirikisho ni yale ambayo yakibaki katika nchi zilizungana basi kwa kweli nchi hizo zitakuwa hazikuungana kuwa nchi kuwa nchi moja bali zinaendelea kuwa nchi mbili zenye ushirikiano mkubwa katika mambo fulani fulani.


Nchi za Afrika Mashariki zilikuwa katika hali kama hiyo kabla ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Zilikuwa ni Nchi Tatu zenye ushirikiano mkubwa, lakini hazikuwa Nchi Tatu zilizoungana kuwa Nchi Moja yenye muundo wa Shirikisho. Shirikisho halisi la nchi mbili litakuwa ni Nchi Moja yenye Serikali tatu, Serikali ya Shirikisho, na Serikali mbili za nchi mbili za awali zilizoungana kuzaa nchi mpya moja.


Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmojawapo wa mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo kwa sababu ya udogo wa Zan­zibar na ukubwa wa Tanganyika. Zan­zibar ilikuwa na watu laki tatu (300,000) na Tanganyika watu milioni kumi na mbili (12,000,000). Muungano wa Serikali Moja

Ungefanya ionekane kama Tangan­yika imeimeza Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tuuhaniwe hata kwa makosa, kwanba tunaanzisha ubeberu mpya!

Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzi­bar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo. Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa Tan­ganyika ndio hasa ungeendesha SerikaIi ya Shirikisho. Kwa hiyo Tan­ganyika ingeendesha Serikali yake ya watu 12, 000, 000 na pia ndiyo ingetoa sehemu kubwa ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la watu 12,300,000.

Ni Watu wanaofikiri kwa ndimi zao wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yoyote kati ya hizo ingekuwa ndogo. Gharama ya Serikali ya Tan­ganyika isingekuwa ndogo, (waulizeni Wazanzibari), na wala ya Serikali ya Shirikisho isingekuwa ndogo. Hata bila ya gharama za mambo yasiyo ya Shirikisho. Na gharama zote hizo kwa kweli zingebebwa na Tan­ganyika.

Kwa hivyo ilitupasa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyika gharama zote hizo; na hasa kwa nini tunataka Serikali ya Tanganyika? Hivi tuna hofu ya kwamba Tanganyika, bila kuwa na SerikaIi yake, itaoekana kuwa imemezwa na Zanzibar? Hofu yetu ni kwamba tukiwa na Serikali Moja Tanganyika itaonekana kuwa imeimeza Zanzibar. Basi na tutafute mfumo ambao utaiondolea Zanzibar hofu hii ya kumezwa, bila kuibebesha Tanganyika mzigo wa kuendesha Serikalli mbili zenye uzito unaolingana.

Hivyo ndivyo tulivyofanya, na hiyo ndiyo asili ya muundo wa Muungano wa serikali mbili. Badala ya kutungua mfumo uliopo kama wapumbavu, tulitazamia hali halisi yetu ilivyokuwa, na tukabuni mfumo uliotufaa zaidi.

Mwalimu Nyerere katika Uongozi wetu na Hatma ya Tanzania



Mimi nina maswali yafuatayo
(1) Kwa wale Mnaotaka serikali Tatu, ni kwa namna mtaweza kuibeba serikali ya Shirikisho, na serikali ya Tanganyika, Kwa resources zipi?, na nguvu za kiuchumi zipi za kubeba serikali hizo mbili, za Tanganyika na shirikisho?, kwani siyo siri Atakayebeba mzigo mkubwa zaidi wa kuchangia shirikisho ni dhahiri kwamba atakuwa Tanganyika, yeye ndo ana watu wengi na uchumi wake ni mkubwa kuliko Zanzibar.
(2) Je, Serikali Tatu zina faida yoyote kwa Tanganyika, iwapo Zanzibar watataka Nchi yao, Ulinzi wao, kiti katika umoja wa Mataifa na jumuia mbalimbali za Kimataifa?.

Ninavyoona:

Tukiunda serikali Tatu, ambapo Serikali ya Shirikisho itakuwa haina nguvu kuliko serikali za Tanganyika na Zanzibar, ni dhahiri haitachukua muda kabla shirikisho lenyewe halijafa, kwa sababu Watanganyika hawatakubali, kutokana na kwamba wao ndo watabeba mzigo zaidi!.
Kwa hiyo, Laiti Wazanzibar wangeona Mantiki ya Serikali mbili, na kujikita katika kutatua matatizo ya hapa na pale, bila shaka huu ungekuwa Muundo uliobora zaidi(reasonable Union).
Hata hivyo muundo ambao ungekuwa bora zaidi ulikuwa ni wa serikali moja, ila kutokana na hofu kama Alivyoonyesha Mwalimu, za "isije ikaonekana Tanganyika kuimeza Zanzibar", basi ni dhahiri muundo wa serikali mbili ndo unafaa kwa sasa na kwa miaka kadhaa ijayo.
Serikali Tatu hazitazaa nchi moja, Tusiongopeane!. zitazaa Loose Federation ambayo itakuwa haina Tija!, kama Mzanzibari anataka kuji"identify" kama Mzanzibari na Mtanganyika anataka kuji"identify" kama Mtanganyika, sasa hiyo Federation ni ya nini?.

 

wana'JF ningependa tulijadili hili kwa sababu katika utafiti wangu (usio rasmi sana) nimegundua kuwa hii dhana ya serikali tatu ni kama vile inaeleweka vibaya, yaani sielewi elewi watu wanafikiri hili linatekelezeka vipi.

Watu wanavyoichukulia hii dhana
nimegundua kua watu huku mitaani kwetu wanavyockia kuhusu serikali 3 wanafikiria ni kuwa na:
1. serikali ya zanzibar (ambayo ipo tayari, SMZ)
2. serikali ya Tanganyika (haipo hivi sasa)
3. serikali ya muungano (kama iliyopo sasa ambayo waziri au rais anaweza kutoka sehemu yeyote ya muungano n.k.)
Maswali yangu
A) Je; huo muundo wa serikali tatu niliouanisha hapo juu ni sahihi/una manufaa kwa mtazamo wako?

B)Kama ni sahihi/una manufaa; je uoni kuwa ni hasara/gharama kuwa na serikali inayohudumia watu milioni 42 (wa Tanganyika) na wakati huo huo kuwa na serikali inayohudumia watu milioni 1 (wa zanzibar) halafu pia kuwa na serikali inayohudumia watu milioni 43 (wa Tanzania) (Assumption:TZ Population is 43million, 42 bara, 1 zenj)? mfano.kuwa na waziri wa elimu wa TZ, Tanganyika na wa Zanzibar!! is it logical??

C)Kama huo muundo sio sahihi au sio maana halisi ya ile dhana ya serikali tatu, upi ni muundo sahihi?ni nini hasa maana ya serikali tatu?

Nawakilisha wana'JF! tunahitaji kuchangia mawazo na hoja sio zaidi....ni muhimu ili huku uraiani tuweze kuwapa wananchi wetu elimu sahihi ya uraia na upembuzi sahihi wa hoja zinazozungumzwa na viongozi wetu wa kisiasa.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA!
THANKS!
 
Mwanakazi.

Kwa hapa tulipofikia hatuhitaji serikali moja wala tatu.
Mwalimu Nyerere alishatoa dawa ya Muungano tokea 1994. Alisema ikiundwa EAC na pia likiwepo azimio la kuunda EA federation basi kinachohitajika ni kuunda serikali ya Tanganyika na kuua serikali ya Muungano.

Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu. Uk 18


“Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili.” Uk 11

Serikali ya Tanganyika ilipasa kufufuliwa tokea mwaka 2000 tulipokubali kuifufua EAC, lakini zaidi sasa kwa vile tumekubali ku-fast track EA Federation.
Wakuu wetu ,they race against time kutuletea serikali moja! Na kutugawia umaskini na mgao wa umeme!

Tutakapotoka usingizini tutakuta hizo nchi nyengine wanachama wa EAC wananufaika vyema na EAC wakati sisi tunalumbana juu ya Muungano na Muundo wake.
Mwalimu aliandika kitabu chake 1994. leo ni 2011. Serikali ya Tanganyika iko wapi?

Halmashami Kuu ya Taifa iliketi Unguja ikabadili Azimio la Arusha bila kwanza kutafuta maoni ya wananchi. Na walikuwa na haki kufanya hivyo, maana sera ni yao. Ubaya wao ni kwamba jambo lenyewe walilifanya kwa hila na 'janja janja", na mpaka sasa wanaendelea kudanganya wananchi kwamba sera ya CCM bado ni Ujamaa na Kujitegemea. Uk 18

Hizi hila na ujanja wa CCM unaonekana katika kila kitu, kujivua gamba, kupambana na ufisadi, kwenye chaguzi, sera ya muungano wa kutoka serikali mbili kuelekea moja, tatizo la umeme kuwa historia, “maisha bora kwa kila mtanzania”, katika issue ya katiba mpya….orodha ni ndefu!!!


Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
 
Muungano hauwezi kuimarishwa kwa upande mmoja kutwaa madaraka ambayo ni ya pande mbili za Muungano huo. Muungano hautalindwa kwa Siasa na kuwaita wale wanaoukosoa au kuukataa kabisa kuwa ni wahuni au maadui wa Muungano.

Ila, hata hao wanaojiita wapenzi na watetezi wa Muungano wanakiri kuwepo kwa kasoro nyingi ndani ya Muungano na hata kufikia kuziandikia na kuzifanyia vikao. Muungano utalindwa kwa kuwekewa misingi madhubuti iliyo wazi ambayo itasimamiwa na Katiba inayokubalika na ambayo itatokana na ridhaa za washiriki wa Muungano kwa kupata uhalali kutoka kwa wananchi husika ambapo washirika watakuwa ni equal partners with equal say ndani ya Muungano huo.

Muungano madhubuti hauwezi kusimama wala kulindwa na sera za Chama. Muungano madhubuti ni ule utakaolindwa na wananchi wa pande zote kwa ridhaa, hiari na kuamini wanafaidika kwa kupata fursa na haki sawa ndani ya Muungano huo
 
Wana jf naomba mnisaidie, hivi juzi nilikuta wanafunzi wanajadili kuhusu muungano na mfumo wa serikali tatu mmoja akauliza hivi tukiwa na serikali tatu ile ya zanzibar ya tanganyika na ya muungano sasa hiyo ya muungano makao makuu yake yatakuwa wapi na je nani atakubali makao makuu yakae kwa mwenzake?

Naomba kuwasilisha
 
Mwl. Nyerere alitaka shirikisho lenye serikali tatu - Joseph Mihangwa

"MUUNGANO huu unatubana mno…..na Muungano ni kama koti tu, likikubana unalivua”. Haya ni maneno ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar na mwasisi wa Muungano, hayati Abeid Amani Karume aliyoyatamka mwaka 1968, miaka minne kabla ya kifo chake akionyesha kukerwa na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kauli hii haikumfurahisha Baba wa Taifa la Tanzania [la Tanganyika na Zanzibar?], Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyetaka Muungano ulindwe kwa nguvu zote, tofauti na Karume alipoonekana kuchoshwa na Muungano kutokana na kile alichokiita “kupelekwa puta kwa Muungano unaokiuka makubaliano”.

Tangu mwanzo, Karume alielewa kwamba, alilazimika kuingia Muungano kwa shinikizo na ghiliba. Aliwahi hata kutishia kutohudhuria sherehe za kubadilishana “Hati za Muungano” na kutangazwa rasmi kwa Muungano huo, mjini Dar es Salaam Aprili 26, 1964.

Na kwa sababu hizo hizo, aliendesha Zanzibar atakavyo, kana kwamba haikuwa sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati Nyerere alizidi kuimeza Zanzibar kwa kuongeza mambo ya Muungano kwa imla, kutoka 11 ya mwanzo hadi 16 wakati wa kifo cha Karume.

Uhasama kati ya viongozi hawa wawili ulifikia hali ya kutisha kuelekea kipindi cha kifo cha Karume kiasi cha wawili hao kutoongea ana kwa ana kwa zaidi ya mwaka mmoja. Mawasiliano yao yalikuwa kupitia wapambe wao, Bhoke Munanka kwa upande wa Nyerere, na Aboud Jumbe kwa upande wa Karume. Kisa? Mfarakano juu ya Muungano!

Kuna wakati Mwalimu Nyerere [mwaka 1968], alikuwa karibu kusalimu amri. Akiandika katika gazeti la “The London Observer” la Aprili 20, 1968, alisema kwa kulalama: “Kama umma wa Wazanzibari, bila ya kurubuniwa kwa hoja za nje, na kwa sababu zao wenyewe, wataona Muungano si wa manufaa kwa uhai wao [na kuamua kujitoa], sitawapiga mabomu kuwalazimisha waendelee na Muungano”.

Yote haya yalitokana na kutekeleza Muungano wenye muundo tata. Wakati Karume aliamini aliingia Muungano wenye Shirikisho lenye Serikali tatu – Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali Kuu ya Muungano, Nyerere kwa upande wake, alitaka Muungano wenye Serikali mbili – Serikali ya Muungano [ambayo pia ndiyo Tanganyika] na Serikali ya Zanzibar, lengo likiwa kuelekea Serikali moja kwa sababu maalumu kama tutakavyoona baadaye.

Na hiyo ndiyo sababu ya kuongezwa kwa mambo ya Muungano kinyemela, kinyume na matakwa ya Mkataba wa Muungano wa Aprili 22, 1964.

Siku moja kabla ya Karume kuuawa Aprili 7, 1972, aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Salim Rashid, alikwenda kumuaga kwamba alikuwa anajiuzulu kazi serikalini. Karume alimsihi asifanye hivyo na kumhakikishia kwamba [yeye Karume] alikuwa anakusudia kuvunja Muungano siku chache baadaye. Hata hivyo [Karume] hakubahatika kuifikia siku hiyo kuweza kutekeleza alilokusudia, kwa sababu ya kifo.

Wachambuzi wa mambo ya siasa za Muungano wanaamini kwamba, kama Karume angeishi mwaka mmoja zaidi ya 1972, Muungano huu ungevunjika haraka, kwa adha na kwa hali ya kutisha. Lakini pamoja na hayo, kifo chake hakikuzika mzimu wa kero za Muungano tangu hapo hadi leo, mambo yameendelea vile vile.

“Tunang’ang’ana kujadili Muungano kijuujuu bila kugusa Mkataba wa Muungano. Kwa nini hatujadili Mkataba wa Muungano? Hii ndiyo hati pekee inayohalalisha Muungano na ni msingi na chimbuko kuu la Katiba. Kwa nini tumefanya kujadili Mkataba wa Muungano kuwa dhambi?

Migogoro, mikanganyiko na mitafaruku yote juu ya Muungano inatokana na kukataa kujadili Mkataba huo ambao ndio “Cheti cha kuzaliwa cha Muungano”. Ni maneno ya Rais wa awamu ya pili Zanzibar, Aboud Jumbe akihoji Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu [NEC] ya CCM iliyomwita kumhoji na hatimaye kumvua nyadhifa zote za uongozi kwa kuhoji muundo wa Muungano, Dodoma, Januari 24 – 30, 1964: Soma Mhtasari wa Kikao hicho, ukurasa 116 – 117].

Jumbe, kama Karume, alikuwa ameanza kubaini jinsi utekelezaji wa Muungano ulivyopelekwa puta bila kuzingatia Mkataba wa Muungano kwa mtizamo wa Muundo wa Serikali mbili kuelekea Serikali moja, na kuzua hofu miongoni mwa Wazanzibari kwamba “nchi” yao ilikuwa inamezwa taratibu na Tanganyika.

Na hiki ndicho kilichomsukuma Jumbe kutumia haki yake ya kikatiba kutaka kuhoji kwenye Mahakama Maalumu ya Katiba kupata ufafanuzi juu ya Muundo sahihi, ridhaa inayopatikana kwa kila Mtanzania chini ya ibara ya 125, 126 na 128 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya 1977.

“Awali ya yote, niweke wazi kuwa, chini ya Mkataba wa Muungano, uhusiano wa kisiasa uliokusudiwa ni wa Shirikisho. Mkataba wa Muungano haukufuta Tanganyika wala Katiba na Sheria za Tanganyika”, alisema Jumbe kwa kutoa changamoto kwa NEC ya CCM iliyomwita kumhoji.

Akaendelea, “Ule ukweli kwamba Tanganyika ilikabidhi mambo yake kwenye Muungano, haimaanishi kwamba Tanganyika ilikufa. Huu ulikuwa mpango wa muda tu kusubiri Katiba ya Muungano”,

Kwa hili, bila shaka, Jumbe alikuwa ananukuu ibara ya 5 ya Mkataba wa Muungano na kifungu cha 8 (1) cha Sheria ya Muungano, Namba 22 ya 1964, vinavyotamka kuwa; “Kuanzia siku ya Muungano na kuendelea, Sheria za Tanganyika na Sheria za Zanzibar zitaendelea kuwa na nguvu katika nchi hizo kwa mambo yote yasiyo ya Muungano”,”.

Mwalimu akacharuka, akasema: “Sasa mkanganyiko wa mawazo umezuka. Makamu [Makamu Mwenyekiti wa CCM - Jumbe] anasema kuna Serikali tatu; mimi nasema mbili. Ni suala la Mkataba wa Muungano. Na kesi imeandaliwa kwenda Mahakamani kwa Serikali ya Mapinduzi kuishitaki Serikali ya Muungano kwenye Mahakama [maalumu] ya Katiba. Ukuu wa Chama. Kwa kosa gani Serikali ya Zanzibar iishitaki Serikali ya Muungano?..... Makamu, jiuzulu sasa hivi”, Mwalimu akamwagiza Jumbe kikaoni.

Jumbe akajiuzulu [kwa shuruti?] nyadhifa zote za Chama na Serikali kwa dhambi ya kuhoji Muundo wa Muungano. Na kuanzia hapo akawekwa chini ya Ulinzi nyumbani kwake “Mji mwema” kwa miezi mingi.

Mwalimu alikuwa muumini wa Serikali tatu.

Kama tutakavyoona baadaye, tangu mwanzo, Mwalimu hakuwa muumini wa Serikali mbili, bali wa Shirikisho. Kwake Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulivyo, ulikuja kama ajali tu.

Ulitokana na shinikizo la nchi za Magharibi enzi za vita baridi, zikimtumia Nyerere “aimeze” Zanzibar ndani ya tumbo kubwa la Tanganyika baada ya Shirikisho la Afrika Mashariki kushindwa ili isiangukie mikononi mwa Wakomunisti kufuatia Mapinduzi ya Kikomunisti Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Mwanzoni, Nyerere alikuwa mpinzani mkubwa wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, pale wazo hilo lilipowasilishwa kwake na Balozi wa Marekani, Februari 1964; na tena Machi 7, 1964 na Naibu Waziri wa Nchi wa Marekani [Mambo ya Afrika], Jimmy Trimble. Lakini taratibu, alianza kuona hatari mbele yake kwa Zanzibar ya Kikomunisti [hakupenda Ukomunisti mwanzoni] kuwa mlangoni mwa Tanganyika, huku nchi za Magharibi nazo zikimshinikiza achukue hatua juu ya jambo hilo.

Alianza kutambua udhaifu wa Serikali yake na wa nchi zingine za Kiafrika dhidi ya hatari kutoka nje. Si hivyo tu, tangu mwaka 1960 kabla ya uhuru, alihofia Zanzibar kuwa karibu na Tanganyika akatamka wazi wazi akisema: “Kama ningekuwa na uwezo wa kukisukuma kisiwa kile [Zanzibar] hadi katikati ya bahari ya Hindi, ningefanya hivyo. Sitanii. Nina hofu [kwamba], huko mbele kitakuja kutuumiza kichwa”.

Juhudi zote za Nyerere kuona Shirikisho la Afrika Mashariki [EAF] likiundwa, zilikuwa ni kuhakikisha Zanzibar inamezwa ndani ya Shirikisho, na pale Shirikisho hilo liliposhindwa, akaona njia pekee ya kuondokana na hofu yake [na sasa kwa kupewa nguvu pia na Marekani na Uingereza ambazo nazo zilikuwa na hofu ya Ukomunisti kuenea Afrika Mashariki kupitia Zanzibar] ni kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika.

Kuhusu Muundo wa Serikali mbili alioendeleza, tofauti na Serikali tatu za Mkataba wa Muungano, unalenga Serikali moja kwa kuongeza taratibu [kinyemela] mambo ya Muungano ili hatimaye Zanzibar ijikute imenyang’anywa mambo yote kuwa chini ya Serikali ya Muungano ambayo ndiyo Tanganyika pia. Ugomvi wa Karume na baadaye Jumbe juu ya Muungano umejikita hapo. Na hivi karibuni, Rais wa Zanzibar, Dakta Mohamed Shein, amewakemea wote wanaodhani Zanzibar siyo nchi yenye mamlaka kamili waache uzandiki huo.

Nyerere alisalimu amri kwa shinikizo


Vitisho na shinikizo la Marekani na Uingereza vilimfanya Mwalimu akubali Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kukidhi matakwa ya Mataifa hayo. Vitisho vipi?. Kwanza, alikuwa bado na kumbukumbu yenye hofu jinsi alivyonusurika kupinduliwa na Jeshi lake mwenyewe, Januari 20, 1964; na jinsi alivyookolewa na Jeshi la Waingereza ambao ndio pia walioshinikiza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Na hata kama angekataa kuungana, Uingereza na Marekani, chini ya mpango wa kivita ulioitwa “Zanzibar Action Plan” [ZAP], zilikuwa tayari kuivamia Zanzibar kijeshi, kama Karume angekataa Muungano.

Uhakika ni kwamba, majeshi ya Uingereza, chini ya Kamanda wa Jeshi la Anga – “Royal Air Force” [RAF], Brigedia Jenerali I. S. Stockwell, na Kamanda wa Jeshi la Ardhini nchini Kenya, Brigedia Jenerali I. H. Freeland, yalipewa Amri [Joint Operation Instruction] Namba 2/64 kuvamia, huku yakitarajia upinzani na kipigo kutoka Jeshi la Zanzibar [Zanzibar Liberation Army – ZLA] chini ya Uongozi makini wa Kanali Ali Mahfoudh, na pengine kwa msaada kadhaa wa silaha kali kutoka China na Urusi.

Pili, Mwalimu bado alikuwa akikumbuka kwa hofu, kuuawa kwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Kongo, Mwanamapinduzi Patrice Emery Lumumba, na Rais Sylivanus Olympio wa Togo, waliouawa kikatili chini ya kile kilichoitwa “mchezo mchafu wa nchi za Magharibi dhidi ya Viongozi wanamapinduzi barani Afrika”.

Kwa hili, Nyerere aliona lazima achukue hatua haraka badala ya kusukumwa na kujiweka rehani kwa ugomvi wa mataifa makubwa ya Magharibi na Mashariki. Na hii ilikuwa Baraka pia kwake kumaliza “hofu” yake juu ya Zanzibar huru.

Muungano huo, ambao ulibuniwa baada ya kuvunjika kwa mpango wa EAF mjini Nairobi, Aprili 10, 1964, ulikuwa njia pekee ya kumzuia aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje wa Zanzibar wa wakati huo na Mkomunisti, Abdulrahman Mohamed Babu na mawakala wenzake wa Wachina [Chicoms] na Warusi, asidhibiti na kuhodhi madaraka ya Serikali ya Mapinduzi Visiwani.

Kuna dhana isiyo kweli kwamba Machi 1964, Mwalimu na Karume walikutana Ikulu Dar es Salaam ambapo Mwalimu alipendekeza kwa Karume juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na eti kwamba Karume alikubali mara moja akisema: “Ita waandishi wa magazeti; waambie kwamba sisi tuko tayari sasa hivi”.

Dhana hii imepotoshwa. Maneno ya Mwalimu yalikuwa hivi: “Tazama, nimewaeleza wazi wazi Waziri Mkuu [Jomo] Kenyatta na Waziri Mkuu [Milton] Obote kwamba, wao wakiwa tayari kuunda Shirikisho la Afrika Mashariki, sisi [Tanganyika] tuko tayari. Na sasa nakwambia na wewe [Karume, kama nilivyowaambia Kenyatta na Obote], kwamba Zanzibar mtakapokuwa tayari kuunda Shirikisho [hilo], sisi [Tanganyika] tuko tayari”.

Ukweli ni kwamba, alichomwambia Karume ni juu ya uundaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki na si Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ingekuwaje hivyo wakati muda huo Nyerere alikuwa akifukuzia Shirikisho la Afrika Mashariki kuliko kitu kingine chochote, hadi juhudi hizo ziliposhindwa Aprili 10, 1964 na kugeukia Zanzibar?

Nani anasema Mwalimu alitaka Serikali mbili?


Tumesema, Mwalimu tangu kale hakuwa muumini wa Muungano wenye Serikali mbili ila kwa Tanganyika na Zanzibar kwa lengo maalumu. Kwenye Mkutano wa nchi huru za Afrika mjini Cairo, Julai 1964, alionyesha wazi wazi kutopendelea Muundo huo aliposema, “Muundo wa Serikali moja [Unitary System of government] haufai kwa Afrika kwa sasa; Muundo bora ni ule wa Shirikisho la Nchi”.

Akitetea hoja hiyo baadaye, aliandika makala ndefu kwenye Gazeti la “Africa Forum” [Vol.1 No. 1] mwaka 1965 akisema: “Mfumo bora ni ule wa Shirikisho lenye Serikali Kuu ya Muungano na Serikali za nchi zinazoungana, kila moja ikiwa na Mamlaka juu ya Mambo yasiyo ya Muungano”. Msimamo wake huo ameurudia pia katika Kitabu chake: “Uhuru na Umoja” [Freedom and Unity] ukurasa 300 – 304.

Na hivyo ndivyo alivyoamini Mzee Karume. Akitoa taarifa kwa Serikali yake kwa simu ya maandishi [telegraph], aliyekuwa Balozi wa Marekani nchini Zanzibar kabla na baadaye kidogo kufuatia Muungano, jasusi la CIA, Frank Carlucci, Aprili 23, 1964 alisema, “Karume ametia sahihi [Aprili 22, 1964] Hati [Mkataba] ya Muungano akiamini kwamba ameingia Mkataba wa kuunda Shirikisho lenye Serikali tatu”.

Na siku za karibuni kabla ya kifo chake, baada ya kuchoshwa na kero za Muungano zisizoisha, Mwalimu alitambua utata wa Muundo wa Serikali mbili alisema muundo huo yafaa ujadiliwe kuondoa utata hata kama yeye alikwishatoa msimamo wake wa Serikali mbili.
Ukweli Mwalimu alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa, kama isingekuwa kwa “mambo fulani fulani” juu yake, asingemvua Jumbe madaraka kwa kuhoji Muundo wa Muungano.

Je, hawa wanaojifaragua, hivi sasa, kwamba kujadili Muundo wa Muungano nje ya Serikali mbili ni kumsaliti Mwalimu, wanatoa wapi ujasiri huo kuuhadaa umma? Kama ni kumsaliti Mwalimu, tusemeje juu ya hao hao waliohujumu Azimio la Arusha na Ujamaa; waliobinafsisha mali za umma bila kujali ili kuwapa ulaji mawakala wa ubepari? Je, si wasaliti, hao hao wanaokigeuza Chama cha Mwalimu [CCM] kichaka na kimbilio la mafisadi wasiotaka kujivua gamba?.

Sio siri tena kwamba Wazanzibari wengi hawapendelei Muungano wa Serikali mbili au moja, mbali na wanaotaka uvunjwe. Lakini Wahafidhina wa siasa za makundi, kwa unafiki mkubwa, wanajifanya kutoliona hili.

Ni hao hao waliopinga mchakato wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Visiwani, wakiwamo Wajumbe wa NEC ya CCM, mpaka Rais wa wakati huo, Amani Abeid Karume akatishia kuwaumbua.

Uhafidhina huo na unafiki wao wa kutaka kuona migogoro na kero za Muungano zikiendelea ndio unaofanya waishi kwa gharama ya amani na umoja wa Kitaifa wa nchi yetu.

Sasa, ifike mahali waambiwe wazi wazi, waache demokrasia na mawazo ya wananchi juu ya Muundo wa Muungano wautakao yatawale badala ya ubinafsi wao. Na tunaposhinikiza mambo dhidi ya matakwa ya wengi tunatafuta nini, na nini hatima ya yote haya?
 
Angalia kiambatisho - picha hii inawasilisha ujumbe wakutosha kuliko maneno nitakayoandika. Hapo ni Jaws Corner Zanzibar.
 

Attachments

  • Muungano.jpg
    Muungano.jpg
    593.2 KB · Views: 637
Waarabu tuna usemi unaonena. ''NI RAHISI SANA KUWADANGANYA WATU. LAKIN NI VIGUMU SANA KUWAAMBIA WATU KUWA WAMEDANGANYWA''

Na vile vile Mwimbaji mashuhuri wa Reggae Robbert Nesta Marley (mmarufu kama Bob Marley) kwenye wimbo wake wa "Redemption song" alisema YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOMETIMES BUT YOU CAN'T FOOL ALL THE PEOPLE ALL THE TIME"

WaTanzania mumeamua kuiga tabia ya “ujanja” wa mbuni wa kuzika kichwa mchangani, eti kukwepa janga. Labda tujikumbushe kidogo kwa hili.

Mdahalo wa kwanza juu ya mfumo na muundo wa Muungano ulianza kwa njia ya maoni juu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1983/84. Hapo, kwa mara ya kwanza ilibainika kuwa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakiongozwa na Rais Aboud Jumbe, na wale wa Serikali ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mwalimu Julius Nyerere, walikuwa na mitazamo tofauti inayokinzana juu ya Muungano.
Jumbe na timu yake walitaka Muungano uwe na Serikali tatu kwa maana ya Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar (iliyopo sasa) na Serikali ya Muungano yenye kushughulikia mambo ya Muungano tu, ambayo yameainishwa katika Ibara ya 6(a) ya Katiba ya Muungano (Articles of Union) na kifungu cha 8 cha Sheria ya Muungano (Acts of Union) Namba 22 ya 1964, na hatimaye ibara ya 4 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977.
Jumbe alikwenda mbali zaidi kwa kuandaa Hati ya Maombi ya kuhoji na kutaka ufafanuzi kwenye Mahakama Maalum ya Kikatiba juu ya muundo sahihi wa Muungano kwa kutumia ibara ya 125 ya Katiba.
Tofauti hizi kati yake na Mwalimu hazikwisha salama kwa Jumbe kuthubutu kukanyaga mahali “patakatifu” bila kuvua viatu. Jumbe alilazimishwa kuachia ngazi zote za uongozi wa nchi kuanzia Urais wa Zanzibar, Umakamu wa Rais wa Muungano, na nafasi zote za kichama Januari, 1984.

Utata mwingine huu uliibuka tena kwa nguvu mpya zaidi wakati Wabunge 55 (maarufu kama G55) wa Bunge la Muungano, walipowasilisha bungeni mwaka 1993, hoja ya kutaka kuundwa/kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika kwa kukasirishwa na hatua ya Zanzibar kujiunga na OIC kama nchi huru nje ya Muungano, Desemba 1, 1992.
Ukweli, Bunge lilikuwa limekwisha kupitisha kwa kauli moja, Azimio la kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika Agosti 24, 1993 kwa maana ya kuwa na Serikali ya Muungano inayoundwa na Serikali hai zenye Mamlaka huru, za Tanganyika na Zanzibar, kama vile tu alivyotaka Rais Jumbe mwaka 1983.
Hata hivyo, Azimio hilo lilipigwa rungu zito na Mwalimu Nyerere na likavunjika.. Na kama ilivyokuwa kwa Jumbe, hapa napo mambo hayakuisha salama; safari hii Waziri Mkuu wa wakati ule, John Malecela (hongera kwa kutimiza miaka 75) na Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba, walipoteza nyadhifa zao kwa sababu ya ama kunyamazia au kuunga mkono hoja / Azimio la G 55.

Suala langu hapa Je kulikuwa na Siri gani kwa St Nyerere kukataa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano wenu wa Tanzania?


Kifupi naweza kusema mumeamua kuiga tabia ya “ujanja” wa mbuni wa kuzika kichwa mchangani, eti kukwepa janga.

 
Na lingine linalofanana kabisa na hayo ya Post Na1 na 2, Je kwanini tunazing'ang'ania Pemba na Unguja zilizo mbali kidogo, na kuna separation ya bahari, kwanini tusiungane na nchi kama Burundi Rwanda au Uganda, ambazo in reality tumeungana nazo kabisa kwenye ardhi?
 
Waarabu mna vituko sana,
Unaonaje hizo kelele ukienda kuzipigia kwenye kaburi la NYERERE kule BUTIAMA?

Buji Buji,

Si unajua kwenda kuliangalia Kabuli la St Nyerere ni lazima ulipe kiingilio. Sasa mimi sina pesa za Kiingilio.

Na siwezi hata siku moja kutoa pesa yangu ili kwenda kuona Kabuli. Hata nilipotembelea Agra (UP) kule India, kuona Taj Mahal sikulipa kiingilio.

lakin ni suala la msingi sana hususan kwa WaDanganyika.

 
Mwalimu aliwakumbatia wazanzibar kwa shinikizo la CIA (USA) kwa kuwa mwarabu alikuwa na urafiki/njama na former KGB ya iliyokuwa USSR (RUSSIA). Mgongano ya kimaslahi/Territory ndio chimbuko la yote na aliyekuwa middleman/negotiator ni KENYATTA (RIP).
 
Uamsho @work...
Mwanakijiji mbna ameshapa njia ya kujtenga

Remote,

Ahali yangu usikurupuke.
Nimeonyesha na kubainisha harakati mbili kuu kabisa zilizonywa kupitia vyombo sahihi kabisa vyenye mamlaka ya nchi yenu Tanzania. Lakin zote Nyerere alipinga katakata kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika.

sasa tulipenda kujua kutoka kwenu Je kuna Siri gani aliyokuwa nayo kuhusu Serikali ya Tanganyika nje ya Muungano?

nakushauru nisome vizuri sana kwenye bandiko langu, kisha kama utakuwa na jibu basi Bismillah

 
Mwalimu aliwakumbatia wazanzibar kwa shinikizo la CIA (USA) kwa kuwa mwarabu alikuwa na urafiki/njama na former KGB ya iliyokuwa USSR (RUSSIA). Mgongano ya kimaslahi/Territory ndio chimbuko la yote na aliyekuwa middleman/negotiator ni KENYATTA (RIP).

Kwani kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano wenu kungeathiri nini uwepo wa Zanzibar na Tanzania?

 
Swali jingine linalofanana na hilo ni hili: Kwa nini Mwalimu alikataa pendekezo la Sheikh Karume la kuunda serikali moja tu?

teh teh teh... WildCard, wengine wanasoma mambo nusu nusu tu ili kukidhi haja zao. Wanasahau nchi hii Nyerere alikuwa raia kama mwingine yoyote ila tu alikuwa amepewa dhamana ya uongozi. Na hatima ya nchi hii haiko kwenye mikono ya Nyerere bali iko kwenye mikono yetu sote kama raia.
Sasa kelele kuhusu muungano na Nyerere zinasaidia nini wakati kama hatuutaki muungano uwezo wa kuukataa uko kwenye mikono yetu na sio Nyerere aliyekufa miaka 13 iliyopita?
 
Last edited by a moderator:
Hivi tulitakiwa tusonge mbele kuelekea NCHI moja au turudi nyuma kurejesha Tanganyika na hatimae tusambaratike kama Yugoslavia au USSR? Zanzibar tayari ni NCHI hata hivo. Ni kiti cha UN tu hakijarudi kwa ujinga wa Maalim Seif na Jussa kuyasemea haya kusikohusika badala ya kupeleka haraka hoja kwenye BUNGE la JMT ambako ndiko masuala ya Muungano yanakojadiliwa na kutolewa uamuzi kama wale G55 walivyofanya wakati ule.
 
Back
Top Bottom