Hoja ya Zitto Kabwe dhidi ya Pinda sasa yaimarika!

Tanzania inatisha unavaa koti hili likichafuka unabadili unarudi kwenye ulingo. Hizi ndiyo siasa zetu, kinachotakiwa ni mabadiliko ya kweli kwenye eneo la Makatibu wakuu, Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa na Wamashirika ya umma wakiendelea basi kwenye siasa itabaki kubadili makoti nasi tukaendelea kuumia. HOJA YA ZITTO IMEIMARIKA. Mimi nilitegemea mabadiliko yataanza na kuwawajibisha waliotajwa kutuhujumu.

[MENTION]Anadetus[/MENTION].......tz ni ubabaishaji mwingi maneno maneno matupu hayavunji mfupa..................lakini siye tunaamini maneno matupu ambayo hayatupeleki popote pale..........
 
Exactly! Wao walichakachua kura za maoni za wabunge wakapitisha watu wao wakijua kabisa, waziri ni lazima awe mbunge. Sasa kama una-wabunge wa aina ya Lusinde, Maji Marefu, Vicky Kamata etc utawapata wapi mawaziri wachapakazi? JK wala asilalamike eti amejitahidi ooh please! JK & Co walijua wanachokifanya au la, hawakuweza kuona mbali zaidi ya urefu wa pua zao. Utasemaje umejitahidi kutafuta mawaziri wakati ulianza na wabunge ambao ni below standard? Ukishakuwa na wabunge wababaishaji umeshaji-limit kabisa kwenye kuchagua mawaziri wanaofaa. Ndio yanakuja haya yakumwapisha mtu the same day na uwaziri juu. In general, hawa watu hawako serious kabisaa; awamu hii imezidi ubabaishaji.

Unstoppable tunachohitaji kwenye katiba mpya ni kukataa wabunge kushika wadhifa zaidi ya ubunge tu.....huu uwaziri bandia utakuwa umefikia kikomo.............
 
Last edited by a moderator:
Mkuu suala la 2015 siwezi kuliongelea, lakini kwa elimu hii ya demokrasia inavyozidi kusambaa watu wanataka mabadiliko. Haijalishi amebanwa nani au katetewa nani, kwa historia niliyonayo na demokrasia(japo siyo kubwa) kuna uwezekano mkubwa watu wakafanya mabadiliko.

Morinyo uko kwenye mstari ugumu wa maisha ndiyo utatufumbua macho na kutaka kujua kiini cha matatizo yetu yot tena.....lol
 
Last edited by a moderator:
very well presentation and content quite true. Naunga mkono hoja. It is time kuendelea na hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. sababu zote ushazitoa. na kama rais anashauriana na waziri mkuu kabla ya kuunda baraza la mawaziri, na kama waziri mkuu tuliyenaye anajua hoja ya msingi iliyolalamikiwa na wabunge kwenye kikao kilichopita, na bado akamshauri rais kuendelea/kuwahamisha mawaziri waliolalamikiwa, basi kwa uhakika waziri mkuu huyu hatufai! na kama atajitetea kuwa alimshauri rais ila rais hashauriki, basi aidha yeye ajiudhuru kwa hiari yake au bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na rais, mambo yote yawe hadharani...wenye nchi yao tuingie ikulu mapema kabla ya 2015!

Manumbu hawa watu wangelikuwa wanatufuatilia tunachosema kwenye mitandao baadhi ya o nafsi zingeliwasuta na kuachia ngazi bila ya kusubiri kudhalilishwa vile............
 
Last edited by a moderator:
Ukiangalia jamaa anachokifanya ni kuwa kama alisema ni upepo tuu na utapita na kweli utapita
hakuna alilolifanya la kudhihirisha anaumizwa na ufisadi uliofanyika
Nyalandu wizara yake inatuhumiwa badala ya kumuondoa unamuhamisha wizara
bado sera ya kulindana inafanya kazi sana hapa bongo
[MENTION]
Mr Rocky[/MENTION]..........................aluta ndiyo kwanza continua...............
 
Kelele na malalamiko kwa sasa hayatasaidia kitu, poa kutegemea hoja za Zito na wabunge wengine kuhimiza uwajibikaji haitaendelea kutusaidia. Cha msingi sisi kama watanzania wenye uchungu na nchi yetu na tuanataka tuwe na aina ya viongozi tunaowataka sisi, tuelekeze ngungu zetu kwenye katiba mpya na kuamua namna ambayo tunataka viongozi hawa wawe wanapatikana. Kwa mawazo yangu mimi viongozi hawa wanaoendesha mustakabali wa nchi yetu wasiwe wanachagulia na mtu mmoja (raisi) kwa matakwa yake; lazima wapatikane kwa utaratibu wa kupigiwa kura, iwe na wananchi au na wabunge wenyewe. Na hata hawa wabunge wa viti maalum nao waaangaliwe. Pia habari ya raisi kuteua wabunge wengi kiasi hicho nadhani pia liangaliwe.

Mkwai umejieleza vizuri lakini kumbuka katiba mpya tayari imekwishachakachuliwa kwa kutuwekea watu bomu ambao hata hatujui wamewapata vipi.................na wamejiwekea mabunge mawili ya kutumalizia.....huku wakidai kura ya maoni ndiyo itatupa madaraka ya kuamua kile wao wanakitaka siye sisi.......kwa hiyo katiba mpa haitakuwepo bali marekebisho ya katiba tu............
 
Last edited by a moderator:
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom