Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

wewe si ulitaka kujua nashiriki ibada wapi? nimekujibu na niambie imekusaidia nini? ndio tatizo la watu wasio na uelewa wa maandiko, hurukia na kudandia chochote wanachoona kinaweza kuwasaidia.

sasa point hapa ni kuwa kutoza fedha (fixed amount) iwe ndogo au kubwa kwa huduma sio ukristo. sasa wewe unayeamii kuwa unajua vyema tuthibitishie kimaandiko kuwa kwa kutoza fixed amount kama bei kwa huduma yake bado he is in line with the scriptures. suala la kuwa hakuna malalamiko sio la msingi. huwezi kujua labda yapo ila hayajaripotiwa na vyombo vya habari. kutosikia jambo haina maana kuwa HALIPO! tambua hilo ndugu

Glory to God

huna hekima ya ki Mungu ndugu kama ungekuwa na hekima usingemtusi binadamu mwenzakona kumuona mwizi tapeli na hana tofauti na waganga wengine, huyo Mungu tofauti na Mungu tunaemwamini sisi na usitake kujifanya unalijua neno kwa kujifunza kwa miezi michache na nina uhakika hii post yake umetumwa sio mawazo yako maana umeonyesha udhaifu hata ktk kuiteyea bado hujakua kiroho ndugu yangu tamani kulijua neno la Mungu na mapenzi yake usiongozwe na mawazo na hisia za wakina Mwingira maana hata Yesu angekua anatukana kama wewe na wenzako sijui kama kuna mtu angeokoka akijibu kwa hoja sio kwa kejeli na matusi kama wewe
nilitaka kujua dhehebu lako nilidhani wale wale waumini wa makanisa ya kiroho kumbe ni mlutheri() ubarikiwe kwa uaminifu wako
POLE SANA KWA KUTEGEMEA SUPPORT YA SHOSSI LAKINI NAONA KAINGIA MITINI
 
huna hekima ya ki Mungu ndugu kama ungekuwa na hekima usingemtusi binadamu mwenzakona kumuona mwizi tapeli na hana tofauti na waganga wengine, huyo Mungu tofauti na Mungu tunaemwamini sisi na usitake kujifanya unalijua neno kwa kujifunza kwa miezi michache na nina uhakika hii post yake umetumwa sio mawazo yako maana umeonyesha udhaifu hata ktk kuiteyea bado hujakua kiroho ndugu yangu tamani kulijua neno la Mungu na mapenzi yake usiongozwe na mawazo na hisia za wakina Mwingira maana hata Yesu angekua anatukana kama wewe na wenzako sijui kama kuna mtu angeokoka akijibu kwa hoja sio kwa kejeli na matusi kama wewe
nilitaka kujua dhehebu lako nilidhani wale wale waumini wa makanisa ya kiroho kumbe ni mlutheri() ubarikiwe kwa uaminifu wako
POLE SANA KWA KUTEGEMEA SUPPORT YA SHOSSI LAKINI NAONA KAINGIA MITINI

haya mkuu na wewe umesikika, nashukuru kwa maoni na kunitakia baraka

ubarikiwe sana na Bwana

Glory to God
 
babu amekuwa mpweke sana .... anafanya kazi usiku kucha na kikubwa ni kwamba babu hana mke ..... nadhani ingekuwa ni project nzuri sana kama ungeungana na babu pale loliondo ili apate faraja

nafikiri kwa jinsi unavyomtetea, wewe ndiye unayemfaa zaidi

amani iwe nawe

Glory to God
 
Miss Loliondo

Hahaaa haa mkuu, umenifanya nianze siku kwa tabasamu na kicheko kikubwa saaaaaaaana... baada ya ghadabu na hasira ya hii thread

The Following 2 Users Say Thank You to LAT For This Useful Post:
MANYANZA (TODAY)
 
Hahaaa haa mkuu, umenifanya nianze siku kwa tabasamu na kicheko kikubwa saaaaaaaana... baada ya ghadabu na hasira ya hii thread

The Following 2 Users Say Thank You to LAT For This Useful Post:
MANYANZA (TODAY)

huyu mama anajifanya yeye ni miss ... no problem
 
Sasa mbona ukiugua malaria na maladhi mengine unaenda hospitali??? si ukae na imani yako ili usimkufuru Mungu??. Mi nadhani wengine hapa ni lazma mdiscourage watu wenye imani za kweli ili kulinda maslahi yenu kwani mashirika yanayojihusisha na vita juu ya ukimwi yatakua na lipi la kufanya ss endapo babu ataponya asilimia kubwa ya watu???..... na utambue kuwa hata huko Rwanda kuna mabinti walishawahi tokewa na bikira maria na kuambiwa watoe ujumbe kwa nchi kuwa watubu dhambi zao kwani nchi inanuka damu ...na kitu hiyo ilikuja tokea baada ya miaka kumi tangu walipotoa taarifa hizo...lakini ieleweke ia kwamba ktk imani wapo watakao amini na ambao mioyo yao itakua migumu sn, hili linaonekana hata kipindi na nuhu na rutu...Tunaona hata Yesu mwana wa Mungu alikua akitibu kwa maelekezo pia ingawa ni mwana wa Mungu aliyekua hata na uwezo wa kusema/kukugusa tu na ukapona lakini utaona anamwambia kipofu achukue tope apake machoni na ataweza kuona

Namalizia kwa kusema hivi NABII HAKUBALIKI KWAO NA KWA SABABU YA UOVU WETU HATA IMANI YETU IMEKENGEUKA
ndugu pakajimmy,

hatukejeli wanaopata faraja huko kwa babu kutokana na magonjwa na madhaifu mbalimbali, la hasha. tunawashauri wapendwa wetu wasome na kufahamu ukweli juu ya nini yaliyo mapenzi na makusudi ya Mungu kama yalivyobainishwa ndani ya biblia na wapime na kujaribu kila roho kama inatokana na Mungu.

hivi kuna mtu huko samunge aliyepata majaribu kumshinda ayubu? mbona ayubu alikataa kumkufuru Mungu? iweje maelfu huko samunge wawe tayari kumdhihaki Mungu kwa sababu ya BP, cancer, ukimwi nk, eti kwa kupokea kikombe cha mchungaji mstaafu!

mwenye imani ya kweli na iliyojengwa kwenye neno (siyo iliyojengwa kwenye miujiza) atamtukuza Mungu hata apate mateso kiasi gani. atamtukuza Mungu hata katikati ya mateso, naam hata kama atamiminwa damu na kufa kama shahidi (martyr). imani yenu iko wapi sasa?

mimi niko tayri kuishi na majaribu ya ukimwi na mengineyo sugu lakini sio kumkufuru Mungu kiasi hicho cha samunge. ee Mwenyezi Mungu naomba nisaidie

Glory to God
 
Hiyo biblia unaisoma vibaya sana mdau, Mungu anahimiza viwango na kiasi na usishangae kumpa mchanganuo 'babu' wa namna gani aitumie pesa inayotolewa kwa huduma
 
.........
sasa point hapa ni kuwa kutoza fedha (fixed amount) iwe ndogo au kubwa kwa huduma sio ukristo..........

Judith kuna kitu nadhani unakosea hapa.
Yaweza kuwa andiko la "mmepata bure toeni bure" ndio basis ya argument yako. Swala la kujiuliza hapa babu alichopata bure ni kipi????
Kwa haraka tunaweza kusema ILE NDOTO anayodai kuoteshwa na Mungu haina monetary value ktk kuipata zaidi ya neema ya Mungu.
Lakini uchimbaji wa mizizi, uchotaji wa maji, uchemshaji wa dawa, wahudumu n.k unagharama in monetary value. Huyo Mungu ametupa akili na hekima tuzitumie ingawa ametutaka tusizitegemee. Kama kutoza sh 500 ndio hekima iliyomuongoza babu hakuna kosa la kimaandiko.

Ingawa umewataka wachangiaji ku-disapprove hoja yako kwa maandiko wewe sijaona kuweka andiko lolote linalomzuia babu kutoza sh 500. Binafsi sina uhakika na dawa anayotoa babu lakini sitotenda haki kuisema negatively kwa vile isije ikawa kwa kufanya hivyo ukawa unashindana na Mungu mwenyewe.

Hapo kale kuna jemedari mmoja alipona ukoma baada ya kuambiwa na nabii Elisha akaoge/dip mto Jordan mara saba na akapona. Mtumishi wa Elisha akaona isiwe noma akamkamua mchuzi yule jemedari na akajipa laana maana aligeuza uponyaji wa Mungu kuwa biashara. Hii inakuonyesha hapakuwa na gharama yoyote aliyoingia nabii zaidi ya kusema neno.

Narudia kusema "Tusimfungie Mungu kwenye boksi" maana anaitwa ALMIGHTY GOD, njia zake hazichunguziki. Enzi za mitume, kina Petro waliponya watu kwa kivuli tu, Paulo alitumia leso zikaponya watu. Kabla yao hapakuwa na andiko ku-support utendaji wa namna hiyo wa Mungu. Na kama Mungu wako is a Living God basi kubali kwamba "He is able to do immeasurably more than all we ask(pray) or Imagine according to His power..." Eph 3:20,21

Hapa Tanzania kuna mhubiri mmoja anaitwa Mwakasege - The last time I attended his meetings at Diamond Jubilee had to part with sh 500. Tuliambiwa ni kwa ajili ya gharama za ukumbi and it was understandable. Je Mwakasege alikuwa anauza kipawa alichopewa bure???
Kusema kwamba kuna watu hawana sh 500 hivyo hawatapat huduma ni kujaribu nadharia ambayo haipo na hatuwezi kujadili kisichokuwpo unless una ushahidi wa mtu aliyekosa huduma kwa kukosa sh 500.

Mimi ni mkristo lakini ni aina ya mkristo ambaye siruhusu hisia za wachungaji kuwa ni msimamo wa Mungu na hivyo uwe msimamo wangu. Kina Kakobe au Mwingira wanaomsema babu kuwa anafanya kazi ya shetanibado hawawezi wakatoa andiko kuthibitisha hilo na wengi wa "wakristo" wameamini maneno yao bila kuhoji.

Mwisho wa siku si wote watakaokwenda kwa babu watapona na kutopona hakutakuwa na maana kwamba ile ni dawa ya shetani, maana sote tunajua si wote waliohudhuria mikutano ya Yesu walipona kama ambavyo wapo wanaopona na wasiopona wakija makanisani kwenu kuombewa.

Hitimisho langu: Hakuna kosa kimaandiko linalomzuia babu kutoza a fixed amount.
 
asante sana mpendwa kwa kuniia moyo maana mashambulizi ni kutoka kila kona. hata hivyo kwa neema ya Mungu sikatishwi tamaa na lolote. nitasimama kidete kutetea imani yangu ya kikristo ISICHAKACHULIWE na yeyote

ubarikiwe sana mpendwa na tuzidishe maombi

Glory to God

Ubarikiwe.
Umesema wewe ni Mluteri.
Unakwenda kanisani kila jumapili?
Unatoa sadaka? Ya Jengo? ya Sare za kwaya? ya Gitaa la kwaya? Unanunua Biblia pale uliyo nayo inapochakaa? Unatoa fungu la Kumi? Unanunua Kitu Siku ya Mavuno? Mkungu wa Shilingi Laki Moja, labda? Kuku wa Shilingi Alfu Hamsini, Labda??
Hela zote hizi Zinakwenda Wapi???
Umeishawahi kuumwa na kwenda Hospitali zinazomilikiwa na Makanisa? Ulitibiwa Bure?

Kama umeishawahi ku-sadaka yote hayo niliyoorodhesha hapo juu Kwa nini leo Uionee Nongwa sana shilingi 500 anayopewa Babu???????
 
baadhi ya wakristo wenzangu na baadhi ya wanaJF mnanishangaza sana.

kuchezea neema ya Mungu nilikosema ni kutokana na kuweka bei kwa uponyaji huo utokanao na karama ya Mungu. ukiweka bei ina maana kuwa asiyekuwa na 500/- hapati huduma! Narudia tena Mungu ninayemfahamu hawezi kutoza hata senti moja!, kama babu anahitaji ku-cover some overheads au kusaidia wenye shida na kanisa anapaswa kuitisha michango ya hiyari ambapo kula mtu atachangia kutokana na uwezo wake na katu asiwapangie kiasi fixed cha kuchangia na kukifanya kuwa sharti la kupata huduma hiyo ya uponyaji. huo ndio ukristo ninaoujua mimi.

suala kuwa KKKT wameunga mkono si hoja. wapi imeandikwa kuwa KKKT wakiunga mkono basi jambo hilo lazima liwe limetoka kwa Mungu? hujasikia makanisa yakitawaza mashoga kuwa wachungaji? wake up my friend. shetani anaweza kutumia hata vingozi wetu wa kiroho, ndiyo maana nasema ni lazima kuijaribu kila roho kama inatokana na Mungu kwa kutumia maandiko matakatifu. kitu chochote kilicho kinyume na maandiko hata kama kimeungwa mkono na serikali, KKKT, wakazi na Loliondo, Arusha na sehemu mbalimbali za Tanzania na hata dunia nzima na hata huyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha ama mkoa mwingine wowote, lazima kikubaliane na maandiko ndugu yangu. ukubwa wa jeshi la wanaokubali, haukifanyi kuwa kitakatifu. tafakari tena ili uwe great thinker wa kweli.

Glory to God

Ni lazima ushangazwe na sisi maana hata rekodi yako ya kutunga thread haifanani hata kidogo na utakatifu unaohubiria na unaotaka babu afanye. Ulituletea thread yenye mbinu za utongozaji tena kwa mwanaume na mwanamke, leo hii useme unafahamu vizuri maandiko na utakatifu wake????? :smash::smash::smash::smash:
Acha kuutukana utakatifu na maandiko yake

Isitoshe naona unarudi kule kule ambapo ulishindwa kujibu maswali ya wengine!
Wewe ulisema ni mlutheran, ambapo tunaambiwa tuwe tunatoa 10% ya vipato vyetu, je hiyo amepanga nani??? Au nayo ametumia shetani kwa watu wa Mungu??? Na hapo pia ni kuchezea neema ya Mungu sio, maana imepangwa utoe 10%???
Biblia zinauzwa kwa kila mtu kutoa hela yake????? Je huu ndio U-great thinker unaoujua wewe??? Huoni ulutherani wako una utata mtupu?? Unapingana na mambo ambayo yanafanyika na kunenwa kila siku huko lutheran???? Uko wapi U-great thinker hapa????

Halafu naona umekomaa na watu kushindwa kutoa hiyo 500/-, hebu nipe statistics zinazoonyesha wangapi walienda kwa babu wakashindwa kutoa hiyo hela????? Huyo mtu ambaye hana Tshs 500/- kutibiwa magonywa sugu, hata kama anatoka kijijini anaishi vipi kupata huduma zenye gharama za kutisha kila sehemu?? Mbona huwanyooshei vidole akina Kakobe, Mwingira na wenzake ambao kila kukicha msisitizo wao mkubwa ni kutoa michango, tena hata kwa mtu mmoja sio hiyo 500/- na ni kila siku ukienda kwake unatoa?? Uko wapi U-great thinker wako hapa???

Maandiko yanasemaje kuhusu michango kwenye huduma za Mungu??? Halafu linganisha na hiyo 10% unipe jibu kama nayo imetumiwa na shetani au la??? Lete U - great thinker wako kwa hili niuone???

Na hata ukitazama rekodi yako ya michango hapa JF haifanani kabisa tena hata kidogo na maelezo yako ya kutaka kuhubiri utakatifu
 
nianze kwa kuweka wazi kuwa sina hakika na imani ya huyu ndugu yetu Mohamedi Shossi, sijui kama ni mwislamu, mkristo ama muumini wa dini nyinginezo.

aliweka wazi kuwa babu si size ya Yesu na alisema kuwa Yesu ni "world icon" na babu hawezi kulinganishwa naye hata kidogo. baadhi walimkosoa kumwita Yesu "world icon" na walikuwa na sababu zao. pia ametoa michango mingi tu mingine ila hapa nataka niungane naye na kumpongeza kwa kuhoji hiyo bei ya babu.

Mungu wetu afikie mahali apange bei!! tena ya huduma itokanayo na karama aliyotoa mwenyewe? kweli hapo pagumu kuingia akilini. tena mungu wake huyo akampa na mchanganuo wa namna atakavyozigawa hizo pesa, eti 300/- kwakanisa, yatima na wajane na 200/- za wahudumu wanaomsaidia kazi! kwa kweli naona kama hizi ni kashfa kwa Mungu wetu.

neema ya Mungu wetu ni kubwa na pana sana, na kamwe huyu babu asiichezee kiasi hiki. yeye atangaze kuwa ni mganga aliyekuja na dawa ya mti wa mrigariga, afuate taratibu za serikali za kujisajili kisheria ili serikali itambue kazi zake na aweke bei yake kama wawekavyo waganga wengine na tutamchukulia kama tunavyowachukulia waganga wengine.

hongera tena Mohamed Shossi, hoja yako ni njema na ya kweli. Mungu wetu hahitaji hata senti yetu moja. karama zake hutoa bure. michango kwa ajili ya kazi ya Bwana ni ya hiyari na kadiri mtu alivyojaaliwa kutoa.

ukishaweka bei (hata kama ni sh.10/-) maana yake ni kwamba asiye nayo hapati huduma! kumbuka madukani kuna pipi za sh.10/- na usipokuwa na hiyo sh.10/- hupati hiyo pipi. ndiyo maana ya bei. sasa babu anasema kama huna sh. 500/- kaa pembeni mwenye hela aje apate kikombe! hata akiamua kuwasamehe wengine kulipa, manake atakuwa kakiuka utaratibu wa huyo mungu wake anayedhibiti bei! sasa hii nayo bado ni huduma ya kiroho kweli kwa mujibu wa dini ya kikristo? mungu gani huyu anayepanga hesabu hivi?

tuendelee kutafakari na kuliombea kanisa

Mungu akubariki sana ndugu Mohamedi Shossi,

Glory to God!

Pia fahamu kwamba njia za Mungu (nakushauri uwe unaanza na herufi kubwa kila unapoandika jina la Muumba wako) hazina cha kuwa great thinker wala thin thinker, sisi sote ni mali yake. Hata babu nae ni mali ya Bwana.
Mbele za Mungu hakuna anaefanana nae kwa kufikiri wala kumkaribia. Uwe great thinker wa JF, mimi nisiwe sote tuko sawa mbele za Mungu.
Kwa imani yako kwamba huenda babu anafanya kazi za shetani, fanya maombi basi ili babu aanguke na ashindwe ktk kazi zake, kuja hapa hapa kumpongeza Shossi hakusaidii kumzuia babu asifanye kazi yake (ambayo wewe unaiona kama ya kishetani)

HAKUNA BINADAMU ANAEWEZA CHUNGUZA NJIA ZA MUNGU WETU
USIHUKUMU USIJE UKAHUKUMIWA
 
Kwanza kwa kurekebisha tu, mchanganuo wa pesa ya babu.

TZS 200- Wasaidizi wa babu(wachimbaji,walinzi,wachanganya dawa)
TZS 200- Kanisa
TZS 100- Babu

I will be back
 
Hoja ya Miss Judith ni ya msingi lakini watu wanajaribu kuipotosha.
Hatukatai kama babu anatibu.
Hatukatai kwamba ameshawasaidia wengi sana na anaendelea kuwasaidia.
Binafsi hata mimi kama ningekuwa mgonjwa ningeenda kupata tiba kwa babu kwani ugonjwa sio mchezo ukikupata utaangaika kila kona kadri ya uwezo wako.
Lakini swala la Mungu kukwambia upange bei flani ili uwaponye watu ndio HOFU kubwa, Mungu wa aina gani huyo?
Wangapi wanakosa hata hiyo sh 500 ambayo kwa wadau humu inaonekana kwao sio kitu.
Ina maana Mungu anatumia ile formular ya 'mwenye nacho...?'
Kwanini isiwe kila mtu atoe kulingana na uwezo wake?

Narudia tena, sisemi tiba ya babu haifai, noo ila naungana na Miss Judy kuwa swala la kupanga pesa ya malipo ndipo panapotia hofu kwamba Mungu hawezi kupanga bei kwani anajua kuwa wapo watu wanaumwa na hawana pesa, je hao wasipate tiba ya Mungu?
 
Ivi unajua mgonjwa wa figo anahitaji kiasi cha shilingi 1m kila baada ya wiki mbili ili aweze kusafisha damu?mshukuru saana Mungu kwa afya uliyonayo,na tena ukatubu kwa hiyo kauli yako.
Ugonjwa siyo mchezo.Kuna wanaopona na kuona kama wangetoa 2m badala ya 500/
 
Hoja ya Miss Judith ni ya msingi lakini watu wanajaribu kuipotosha.
Hatukatai kama babu anatibu.
Hatukatai kwamba ameshawasaidia wengi sana na anaendelea kuwasaidia.
Binafsi hata mimi kama ningekuwa mgonjwa ningeenda kupata tiba kwa babu kwani ugonjwa sio mchezo ukikupata utaangaika kila kona kadri ya uwezo wako.
Lakini swala la Mungu kukwambia upange bei flani ili uwaponye watu ndio HOFU kubwa, Mungu wa aina gani huyo?
Wangapi wanakosa hata hiyo sh 500 ambayo kwa wadau humu inaonekana kwao sio kitu.
Ina maana Mungu anatumia ile formular ya 'mwenye nacho...?'
Kwanini isiwe kila mtu atoe kulingana na uwezo wake?

Narudia tena, sisemi tiba ya babu haifai, noo ila naungana na Miss Judy kuwa swala la kupanga pesa ya malipo ndipo panapotia hofu kwamba Mungu hawezi kupanga bei kwani anajua kuwa wapo watu wanaumwa na hawana pesa, je hao wasipate tiba ya Mungu
?

Kaka
Hapo ambapo wewe unaona kuna utata basi ni bora ungeanza kujiuliza hizo 10% za kipato chako zilizotamkwa utoe kanisani alipanga nani?? Mungu au Binadamu???
Kama alipanga binadamu, mbona haitui-challenge makanisani kama hii 500/- ya babu??
Biblia ina tangaza na kueneza neno la Mungu, lakin inauzwa kwa fixed price, tafakari????!!!
Kanisani huko huko tuahimizwa kutoa sadaka ya jengo na sare za wanakwaya ambapo tuaambiwa ni lazima zifike kiasi fulani, tafakari????!
Tunaenda ktk mahospitali ya makanisa, tunachangia fixed amount kupata huduma fulani, tafakari?????!!!

Baada ya kutafakari hayo yote, then uje kwenye 500/- ya babu ili utibiwe magonjwa sugu
 
Nadhani kukosa 500/ sio ishu.ishu ipo kwenye nauli ya kufika huko
 
Hoja ya Miss Judith ni ya msingi lakini watu wanajaribu kuipotosha.
Hatukatai kama babu anatibu.
Hatukatai kwamba ameshawasaidia wengi sana na anaendelea kuwasaidia.
Binafsi hata mimi kama ningekuwa mgonjwa ningeenda kupata tiba kwa babu kwani ugonjwa sio mchezo ukikupata utaangaika kila kona kadri ya uwezo wako.
Lakini swala la Mungu kukwambia upange bei flani ili uwaponye watu ndio HOFU kubwa, Mungu wa aina gani huyo?
Wangapi wanakosa hata hiyo sh 500 ambayo kwa wadau humu inaonekana kwao sio kitu.
Ina maana Mungu anatumia ile formular ya 'mwenye nacho...?'
Kwanini isiwe kila mtu atoe kulingana na uwezo wake?

Narudia tena, sisemi tiba ya babu haifai, noo ila naungana na Miss Judy kuwa swala la kupanga pesa ya malipo ndipo panapotia hofu kwamba Mungu hawezi kupanga bei kwani anajua kuwa wapo watu wanaumwa na hawana pesa, je hao wasipate tiba ya Mungu?


Ndibalema, Hivi kitabu kikuu kabisa cha Kikristo cha Biblia ambacho yote tunayonukuu na kubishania hapa kinatoka kwayo kwa nini kimepangwa bei ya kukinunulia kutegemea na sehemu inaponunuliwa?? Kwa nini kila Mtu asikinunue kulingana na Uwezo wake tu?? Kitabu cha Nyimbo za Kikristo je? Tenzi za Rohoni? Wa mia tatu, Apewe. Wa alfu Mbili anunue na wa Alfu, Sita Saba naye pia anunue kwa bei hiyo??
 
Back
Top Bottom