Hoja ya Shossi juu ya sh. 500/- ya babu

ndugu pakajimmy,

hatukejeli wanaopata faraja huko kwa babu kutokana na magonjwa na madhaifu mbalimbali, la hasha. tunawashauri wapendwa wetu wasome na kufahamu ukweli juu ya nini yaliyo mapenzi na makusudi ya Mungu kama yalivyobainishwa ndani ya biblia na wapime na kujaribu kila roho kama inatokana na Mungu.

hivi kuna mtu huko samunge aliyepata majaribu kumshinda ayubu? mbona ayubu alikataa kumkufuru Mungu? iweje maelfu huko samunge wawe tayari kumdhihaki Mungu kwa sababu ya BP, cancer, ukimwi nk, eti kwa kupokea kikombe cha mchungaji mstaafu!

mwenye imani ya kweli na iliyojengwa kwenye neno (siyo iliyojengwa kwenye miujiza) atamtukuza Mungu hata apate mateso kiasi gani. atamtukuza Mungu hata katikati ya mateso, naam hata kama atamiminwa damu na kufa kama shahidi (martyr). imani yenu iko wapi sasa?

mimi niko tayri kuishi na majaribu ya ukimwi na mengineyo sugu lakini sio kumkufuru Mungu kiasi hicho cha samunge. ee Mwenyezi Mungu naomba nisaidie

Glory to God

.
Sii kweli hata kidogo kwamba uko radhi kufa shahidi. Kwani avatar yako inashuhudia umeanguka kwenye kamtihani kadogo tu ka Neno la Mungu la kuwataka wanawake wajifunike kwa mavazi ya staha. Ila wewe unahusudu mwanamke kujianika maumbile yake hadharani (ref U'r avatar)
Sembuse mtihani wa maradhi ya kifo.
Halafu hakuna mtu anaemwabudu babu, ni wewe tu kwa maslahi yako binafsi unataka kuaminisha watu ndivyo sivyo.
.
 
.
Sii kweli hata kidogo kwamba uko radhi kufa shahidi. Kwani avatar yako inashuhudia umeanguka kwenye kamtihani kadogo tu ka Neno la Mungu la kuwataka wanawake wajifunike kwa mavazi ya staha. Ila wewe unahusudu mwanamke kujianika maumbile yake hadharani (ref U'r avatar)
Sembuse mtihani wa maradhi ya kifo.
Halafu hakuna mtu anaemwabudu babu, ni wewe tu kwa maslahi yako binafsi unataka kuaminisha watu ndivyo sivyo.
.


nilianza kumtahadharisha mapema kwamba hii thread yake anatutafutia ban watu tukapoanza kuchangia, sasa angalia haka kademu kalivyo kanafki, avatar yake inafanana na mwanamke kahaba, makanisani kila siku wanafundisha makahaba uvaaje, sasa haka kademu kanakojifanya ni katakatifu kaliopo hapa duniani napata shida kidogo kumuelewa malengo yake.
Anyway mimi ngoja niangalie thread nyingine, hapa naona kichefuchefu tupu.
 
cha msingi tunaangalia uponyaji kama ndo ivyo mbona biblia tunauziwa jamani tena inayoandika maandiko hayo uliyoyasema,makanisani sadaka za nini tunatoa,nafkiri hujaumwa ungeenda mwenyewe na mia tano ungetoa naukaona ni ndogo
 
Dada Judith nadhani kwa hili umepotoka!!
Kwa uelewa wangu babu hauzi dawa ndio maana tunasikia hata ukitoa noti ya elfu kumi chenji ya 9,500 inarudishwa.
Watu wanatakiwa watambue kuwa yule babu hawafaanyii maombezi wagonjwa bali yeye amefanyia maombezi dawa yake aliyooteshwa na Mungu.
Cha ajabu ni kwamba huko makanisani wakienda kutembelea wagonjwa mahospitalini huwa wanaomba Mungu awaponye wagonjwa kupitia dawa wapewazo na madaktari. Tatizo binadamu tunataka kumfungia Mungu kwenye boksi wakati tunajua kuwa yeye ni Almighty God.
Kama hujawahi kuugua ama kuuguliwa na kupoteza ndugu wa karibu kwa magonjwa yanayotajwa hapa kama maradhi ya Ukimwi ni rahisi kuwa na conclusion nyepesi nyepesi.

Hakuna binadamu anayeweza kujisifu kwamba anajua njia zote za Mungu NOT even Kakobe au Mh, Dkt, Mchungaji, Mama Rwakatale. Tusihukumu tusije tukahukumiwa.

Kama kwenye makanisa kuna watu watoa huduma ambao hupata posho zinazotokana na sadaka za waumini, hili la babu kuwalipa wahudumu wake sh 200 inakuwa nongwa?? Hao kina Ndodi wanajiita wachungaji na kulipisha wagonjwa mamilioni ya shilingi mbona hauwasemi kwamba wanauza vipawa walivyopewa bure??
Kuna gharama za kutengeneza ule mchanganyiko wa dawa na kwa mtazamo rahisi hiyo 500 haitoshi hata kidogo. Ninachojaribu kuamini ni kwamba baadhi ya watu wamesikia babu anahudumia mpaka watu 4000 kwa siku which is a cool 2,000,000 wakigonga mara 30 wanaona babu anakamua 60,000,000 bila kuwa na kanisa.

Kama makanisa tunayosali, ikiwa analosali dada Judith pia, yangekuwa yanatoa majibu ya kweli na si sarakasi za kwenye Tv na show off kibao za macheni madhahabu na suti za dola 500 hao watu tunaowaona kwa babu wasingekuwepo.

Mie naamini babu kaletwa na Mungu kwa makusudi ya ku-expose unafiki uliojaa makanisani na kushindwa/udhaifu wa serikali zetu kutimiza huduma za kijamii kwa watu wake.
 
nilianza kumtahadharisha mapema kwamba hii thread yake anatutafutia ban watu tukapoanza kuchangia, sasa angalia haka kademu kalivyo kanafki, avatar yake inafanana na mwanamke kahaba, makanisani kila siku wanafundisha makahaba uvaaje, sasa haka kademu kanakojifanya ni katakatifu kaliopo hapa duniani napata shida kidogo kumuelewa malengo yake.
Anyway mimi ngoja niangalie thread nyingine, hapa naona kichefuchefu tupu.
aISEE, kweli huyu dada anatafutia watu matatizo!
Mara baada ya kujifanya Mtakatifu sana hapo juu kwenye posts zake, mi nikakimbilia kwenye profile yake kuperuzi threads alizoanzisha, nikakutana na thread at least moja ambayo inathibitisha mwenzetu huyu ni mdau mkubwa wa LILE JUKWAA almaarufu kama Marie-Rose!

Jamani, mwacheni Mungu aitwe Mungu!..Mambo ya akina Ayubu ni ya nyakati tofauti!...Tatizo na dhambi kubwa inakuja pale tunapohubiri mambo ambayo tuna uhakika hatuyawezi!
Hiyo ni dhambi kubwa kuliko kunywa dawa ya babu(kama at all ni dhambi)
 
KAMA KUNA MGONJWA ALIYEWAHI KWENDA KWA BABU AKAWA HANA 500/= KISHA AKAKATALIWA TIBA NI VYEMA TUKAPASHANA HABARI ILI TUENDELEE KUCHAMBUA...mpaka sasa sina maswali mengi kuhusu babbu
 
mimi niko tayri kuishi na majaribu ya ukimwi na mengineyo sugu lakini sio kumkufuru Mungu kiasi hicho cha samunge. ee Mwenyezi Mungu naomba nisaidie

Glory to God
Aaamen............

kwanza avatar yako imekaa kisatanic.....
 
jamani ifike wakati tuandike kama watu wanao fikiria. hivi ww (missjudy) kwa mtazamo wako unadhani sadaka zitolewazo kanisani zinapelekwa kwa MUNGU? kwa njia ipi? mbona unaongea tu kana kwamba umetoka kuamka usingizini?
Hujui kumsaidia mtu pia ni sadaka? kuna tatizo gani babu akiwapa yatima sehemu ya pato lake? au kwa kua ww hutoi pato lako kwa yatima( my assumption ungelikua mtoaji usingemshaangaa babu!!) basi imekua dhambi kwa wengine kutoa??
Hata huku bibiliani inasomeka anaye fanya kazi madhabauni ale wapi????? malizia kama unajua
hivi unadhani kubebelea maji ya dawa kuni masufuria etc ni kazi ya bure??? au babu anafanya peke yake?? na hao wasidizi wakale wapi?
usifikirie kwe urefu wa pua bwana. kama vipi mambo ya ........ waachie wenyewe...... ila usisimame mlangoni kuzuia wanaotaka kwa hoja potofu!!! nawakilisha.
 
nianze kwa kuweka wazi kuwa sina hakika na imani ya huyu ndugu yetu Mohamedi Shossi, sijui kama ni mwislamu, mkristo ama muumini wa dini nyinginezo.

aliweka wazi kuwa babu si size ya Yesu na alisema kuwa Yesu ni "world icon" na babu hawezi kulinganishwa naye hata kidogo. baadhi walimkosoa kumwita Yesu "world icon" na walikuwa na sababu zao. pia ametoa michango mingi tu mingine ila hapa nataka niungane naye na kumpongeza kwa kuhoji hiyo bei ya babu.

Mungu wetu afikie mahali apange bei!! tena ya huduma itokanayo na karama aliyotoa mwenyewe? kweli hapo pagumu kuingia akilini. tena mungu wake huyo akampa na mchanganuo wa namna atakavyozigawa hizo pesa, eti 300/- kwakanisa, yatima na wajane na 200/- za wahudumu wanaomsaidia kazi! kwa kweli naona kama hizi ni kashfa kwa Mungu wetu.

neema ya Mungu wetu ni kubwa na pana sana, na kamwe huyu babu asiichezee kiasi hiki. yeye atangaze kuwa ni mganga aliyekuja na dawa ya mti wa mrigariga, afuate taratibu za serikali za kujisajili kisheria ili serikali itambue kazi zake na aweke bei yake kama wawekavyo waganga wengine na tutamchukulia kama tunavyowachukulia waganga wengine.

hongera tena Mohamed Shossi, hoja yako ni njema na ya kweli. Mungu wetu hahitaji hata senti yetu moja. karama zake hutoa bure. michango kwa ajili ya kazi ya Bwana ni ya hiyari na kadiri mtu alivyojaaliwa kutoa.

ukishaweka bei (hata kama ni sh.10/-) maana yake ni kwamba asiye nayo hapati huduma! kumbuka madukani kuna pipi za sh.10/- na usipokuwa na hiyo sh.10/- hupati hiyo pipi. ndiyo maana ya bei. sasa babu anasema kama huna sh. 500/- kaa pembeni mwenye hela aje apate kikombe! hata akiamua kuwasamehe wengine kulipa, manake atakuwa kakiuka utaratibu wa huyo mungu wake anayedhibiti bei! sasa hii nayo bado ni huduma ya kiroho kweli kwa mujibu wa dini ya kikristo? mungu gani huyu anayepanga hesabu hivi?

tuendelee kutafakari na kuliombea kanisa

Mungu akubariki sana ndugu Mohamedi Shossi,

Glory to God!

Muulize Sheikh Yahaya ana agua kwa sh. ngapi? kisha linganisha na hiyo ya Babu
 
Nachelea kusema Miss Judith ni mlevi wa kiroho aliyekubuhu hata anashindwa kupambanua issue ya Loliondo. Inawezekana anafanya hivyo makusudi kwa maslahi yake mwenyewe (Kama tulivyoshuhudia Kakobe, Mwingira et la) ambao kwa kiasi kikubwa wamekimbiwa na waumini wao.
Hivi nani asiyejua mtaji mkubwa wa hao wanaonzisha makanisa ya kiroho kila kukicha kwamba rasilimali yao kubwa ni watu? Hivi nani asiyejua kwamba kwao somo kuu ni utoaji wa sadaka na zinapopungua lazima watafute mchawi why? Sasa mchawi wao anaonekana ni Babu hata wengine wamediriki kufunga eti babu afe (Labda wampe sumu mchana kweupe) kwa sababu eti kapunguza Mapato.
Ukiona watu wa aina ya Miss Judith wanabwabwaja hovyo bila kufanya utafiti wa kina, jua Babu kawashika pabaya.
Miss Judith rejea tena kusoma Biblia utaona njia mbalimbali za miujiza Mungu alizotumia Kuwaokoa watu wake vinginevyo umekuwa unakariri vifungu kama kasuku huku uwezo wa kuvielewa ukiwa mdogo.

Miss Judith, badala ya kuikandia Dawa ya Loliondo, ningekuona wa maana kama ungetumia juhudi kubwa kujua uwezo wa dawa yenyewe kwa kufanya research kubaini waliopona maana hapa issue siyo Babu, issue hapa ni wagonjwa kupona.
MUNGU AKUNUSURU USIJE PATA MAJARIBU.
 
mnh watu badala ya kudiscuss issue aliyoleta Judith mnamshambulia yeye?!!!!...tunaona huyu dada alivyowashika pabaya mpk mnakimbilia petty issues kama avatar yake shame on you great thinkazz!:smash:
 
Hizi threads kuhusu babu ni nyingi na wanaozileta, kwa bahati mbaya, hawana hoja mpya! Ingependeza kama moderators wangeangalia namna ya kuziunganisha na kuondoa irelevant posts (naona kuna watu wanatukanana tu humu!).
 
Poleni sana wote mnaomshabikia babu.

Nawaona mmekimbilia avatar yangu kana kwamaba avatar ndiyo inayoakisi mwili na roho yangu.

Jamani avatar ni avatar tu na si zaidi ya hapo. Mi ni msichana mrembo sana mwenye umri wa miaka 26, figure namba 8, maji ya kunde na ni bikira. Sijawahi kuingiliwa na mwanaume awaye yote maungoni mwangu. Nimeyashinda majarinbu yote haya ya maisha ya leo kwa sababu ya nguvu zitokazo katika neno la msalaba. Signature yangu inasema kuwa mwili wangu ni mali ya Mwenyezi Mungu na mimi ninauchukua siku zote na kutembea nao kama dhamana tu. Nautunza na naamini siku moja Mungu atataka hesabu ya matendo yote niliyoutendea mwili wangu hadi siku ile aliyaomua kuniita.

Back to the pint, nataka kuwaasa kuwa:

1.
Mungu hakutuita katika furaha na anasa peke yake, bali pia katika shida na mateso na anataka tumuabudu na kumuamini katika hali zote hizo ili utumishi wetu usije kulaumiwa.

2.
Muijiza si ishara pekee kuwa Mwenyezi Mungu anatupenda na yuko katikati yetu. Mungu amedhihirishwa kwa NENO lake na imani yetu chanzo chake ni kusikia na sio KUONA MIUJIZA!

3.
Sadaka na mafungu ya kumi yaliwekwa enzi za makuhani walawi. Siku zetu hizi tunapswa kutoa kwa moyo na kwa kadiri tunavyojisikia mwenyewe. Hivyo mungu anayepanga kiasi cha kutoa ni mungu tofauti na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Mwisho nawaomba toeni ushahidi wa maandiko ama leteni sababu za kibiblia zinazohalalisa uganga huo wa babu, ama vinginevyo tubuni dhambi na kumrudia Mungu.

Mungu awabariki nyote

Glory to God
 
Nimeishiwa maneno wazungu wanasema i run out of word!!!!
Yaani nguvu zote zimeniisha kabisa.

Sitii neno hapa kabisa!!! Nasoma tu comment


unaitisha mpenzi. hebu tia hata neno moja tu ili nijue mdogo wako nimepotea wapi nipate kurudi. si unajua tena nyie ndio dada zangu?

please nipeni maono yenu, nafaidika sana na michango yenu wapenzi.

please!
 
unaitisha mpenzi. hebu tia hata neno moja tu ili nijue mdogo wako nimepotea wapi nipate kurudi. si unajua tena nyie ndio dada zangu?

please nipeni maono yenu, nafaidika sana na michango yenu wapenzi.

please!

Natamani kuchangia kila nikianza kuandika nadelete ngoja nitarudi baadae maana nguvu zimeniisha kabisa
 
Back
Top Bottom