Hoja ya Madaraka Nyerere kuhusu barabara ya Serengeti

Kila siku watu wanakufa kwa ajali za barabarani je utakubaliana na hoja kuwa ni wakati muafaka nchi hii ikaacha kabisa kujenga barabara na kutumia magari ya moto ili kulinda maisha na mali za wananchi? Kwa ufupi hoja yako haina mashiko.

Tata nakubaliana na wewe kuwa kila siku watu wanakufa kwa ajali za barabarani, hoja yangu ni kuwa pale Mikumi sababu kubwa huwa ni magari yanapojali kukwepa wanyama wavukao barabara, japo hifadhi imejaribu kuweka matuta lakini trend bado inakuwa kila siku
 
Jana nilimsikia mwanamazingira flani wa kenya aidha BBC au VOA jioni akifurahia uamuzi wa kutoweka lami katika barabara hiyo. Kilichoniudhi sana ni kitendo cha kuizungumzia TZ kama mtu mwenye mamlaka (authority) vile ya kutuamulia tufanye nini. Alikuwa anapendekeza barabara mbadala ambazo zinaweza kuwekewa lami na kwamba tukikubali options hizo eti nchi kadhaa zitatufadhili!
 
"
HTML:

Nakushauri ndugu yangu siku nyingiine ukitaka kujibu hoja ya kitaalamu uwe na takwimu na mifano hai sio kukurupuka na kukosoa hoja za msingi ambazo tayari zimeshafanyiwa tafit na wataalamu waliobobea.

Hivi ile lami ya mikumi - Iringa, imeathiri kwa kiwango gani wanyama pori? au wale wa Serengeti ni very special?
 
Jana nilimsikia mwanamazingira flani wa kenya aidha BBC au VOA jioni akifurahia uamuzi wa kutoweka lami katika barabara hiyo. Kilichoniudhi sana ni kitendo cha kuizungumzia TZ kama mtu mwenye mamlaka (authority) vile ya kutuamulia tufanye nini. Alikuwa anapendekeza barabara mbadala ambazo zinaweza kuwekewa lami na kwamba tukikubali options hizo eti nchi kadhaa zitatufadhili!

Unajua Masa Mara kule Kenya ni kiduchu kwa Serengeti yetu.......hii barabara ingepunguza mivuko ya wanyama na kuuwa utalii Kenya
 
Tumeishasahau tulipojivika joho la utaifa wakati wenye nia njema wakituasa tusinunue rada ya BAE. Kwa jeuri tukasema pesa tunazo za kununulia kwa hiyo wasituingilie uhuru wetu wa kujiamulia. Wajukuu zetu watakapoenda huko huko Ulaya kuangalia hawa wamyama na ndege tunaosema hawana faida zetu, tusijifanye kuwa tulirubuniwa.

Amandla........
 
naunga mkono hoja ya ujenzi wa barabra ya lami hata ndani ya serengeti. siamini wanyama watashindwa kuvuka mita 10 za hiyo barabara. si kweli
 
Labda nimuulize mtoa hoja, pale Mikumi pundamilia wengi na hao nyumbu hufa? Nauliza kwa sababu kuna barabara ya lami pale ya miaka mingi
 
Kulinganisha ukubwa na wingi wa wanyama wa hifadhi ya Mikumi na Serengeti ni ujuha....Kwanini msipige makelele serekali hii ijenge reli za kisasa na muachane na barbara zinazoangamiza mamia ya watu kila siku...inchi zinazojua kupiga mahesabu ni bora kulinda wanyama wanaoingiza pato kubwa kuliko kuvuruga mfumo wa maisha ya wanyama kwa barabara ya lami ili hali kuna mbadala wa kuunganisha Arusha na Mara...Wanadamu ni viumbe wabinafsi sana wanatamani dunia hii wangeishi wao tu tena milele
 
-- Kilichojificha nyuma ya pazia katika hili: Hoteli nyingi zenye hadhi ya kitalii jijini Nairobi zinamilikiwa na Kampuni za KIjerumani na Kiisrael sasa wegeni wengi wanafikia hoteli hizo wakidanganywa kuwa Tanzania hamna miundo mbinu bora ikiwemo hoteli na barabara viwanja vya ndege.
-- Ujenzi huu wa barabara utaendana na ujenzi wa hotels na viwanja vya ndege vya kisasa, kwa mantiki hii, hii ni threat kwa mahotel haya makubwa pale Nairobi kwani italazimika watalii waje moja kwa moja Tanzania.
-- Wakenya kwa kudhaminiwa na hayo mataifa ya nje wanajidai kupinga ujenzi huo wa barabara wakati wenyewe barabara ya lami ninakatiza mbuga ya masai mara.
-- Hata mlima Kilimanjaro wanautangaza kama ni wao, watalii wengi wa kuja mlima KIlimanjaro wanafikia Nairobi, hela kubwa wanaacha kule hapa kwetu wanakuja kumalizia chenchi, hata pembezoni mwa barabara ya Namanga kwenda Nairobi kuna shule nyingi, mahospitali, maduka na hata kile chuo kikuu cha waislam vyote vinaitwa kilimanjaro kuonyesha kwamba ni mlima wao
-- Kuna chama fulani cha siasa hapa nchini kishapata fedha kutoka Ujerumani ili kutetea kutojengwa kwa barabara hiyo ya Musoma - Arusha, hakuna uzalendo ulafi na uchu wa madaraka tu!
-- Tunapaswa kuwa wazalendo kwa kuipenda nchi yetu, ikijengwa barabara, hoteli nzuri na viwanja vya ndege pato letu litaongezeka, shida tunashabikia hata hatujui kinachendelea nyuma ya pazia.

Karibuni tujenge uzalendo!
 
Back
Top Bottom