Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
na Asha Bani
IKIWA mapambano ya kudai katiba mpya yanaendelea, jumuiya na taasisi za Kiislamu Tanzania zimesema katika madai yao kutakuwepo na mapendekezo ya kuishinikiza serikali kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Katibu wa Jumuiya hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema watapita katika kila taasisi ya Kiislamu nchini kwa lengo la kukusanya maoni kama ilivyoahidi lakini ni muhimu kuwepo na hoja ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo ya Waislamu.
"Suala la Mahakama ya Kadhi kwa ujumla ndilo muhimu lakini pia ni muhimu kukusanya mambo mengi ambayo naamini yatakuwa na misingi mizuri, kikatiba suala hilo haliwezi kukwepeka lazima liwepo pia," alisema Ponda.
Aidha, alisema wao kama Waislamu wa jumuia tofauti tofauti wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kusema ataunda tume ambayo itakuwa na uwakilishi wa watu wote.
Sheikh huyo alisema hata hivyo kutakuwa na mkutano wa jumuia mbalimbali za Kiislamu utakaofanyika Januari 8 katika ukumbi wa Tanzania Muslim Solidarity Trust Fund ukiwa na lengo la kufanya mchakato wa kupata watu ambao wao wanaamini watafaa katika kuwawakilisha pindi mchakato utakapoanza.
Alisema baada ya kuyapata majina yatakayowawakilisha watawasilisha majina hayo serikalini kama yatakuwa yanahitajika na kwamba Waislamu hao ndio watawafaa katika kuwawakilisha.
Alisema katika mkutano huo pia BAKWATA wamealikwa kuudhuria na wameamua kufanya hivyo ili kuwatoa unyonge Watanzania ambao wanafikiri BAKWATA peke yao ndio wanaostahili kufanya kazi za jamii nzima ya Waislamu.
"Utaratibu huu tunaamini kwamba utamsaidia rais kwa kuwa sisi ndio watu ambao tuna mtandao wa namna ya kuifikia jamii ya Kiislamu ambapo pia itarahisisha kazi za tume na miongoni mwa kazi zetu ni kwenye misikiti kwenye jumuia na kwingineko, tutafika kote," alisema Ponda.