Hoja: Regional vs. National Oposition Political Parties

Nsololi

JF-Expert Member
Mar 8, 2007
298
80
Ndugu Wana JF,

Napenda kuleta mbele yenu hoja hii ya vyama vya kisiasa vilivyoanzishwa kufuatia mfumo wa vyama vingi uruhusiwe mwaka kikatiba nchini TZ mwaka 1992.

Hivi kweli vyama vyetu hivi vina nguvu ya pesa ya kutosha kujieneza nchi nzima na vikawa effective kushindana na chama tawala kilichojilimbikizia mapesa kibao na bado wanaendelea kuchota BOT????

Hivi hakuna haja ya vyama hivi kuangalia strategically ni maeneo gani wanahitaji kuweka nguvu ili ku-maximize mafanikio yao???

Najua kuna watu wataleta hoja ya ukabila au ukanda (hasa wana CCM) lakini tukielewa kuwa itakuwa ni mbinu ya kisiasa tu. Lakini ni vyema ifahamike kuwa duniani kote vyama vya kisiasa vinakuwa na maeneo ambako wanaamini kuwa wana guvu na huko huwekeza zaidi na kutambuliwa waziwazi kuwa eneo fulani ni ngome ya chama furani.

Ni vizuri ikafahamika kuwa hakuna sababu kiutendaji vyama vya kisiasa kama Chadema, CUF, TLP, UDP na vingine kujitanua nchi nzima wakijua kuwa resources zao ni ndogo sana kufanikisha shughuli zao.

Kwa mfano Chadema kwa haraka haraka wanatakiwa kuelekeza nguvu zao katika mikoa ya Kilimanajaro, Mara, Arusha, Kagera na Kigoma, Dar na maeneo mengine wanakoamini kuwa wanaweza kufanikiwa; CUF wakaelekeza nguvu zao Zanzibar, ukanda wote wa Pwani, baadhi miji ya mikoa wanakoamini wana influence ya kutosha kama Bukoba mjini; TLP wakaelekeza nguvu zao mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Mara, Kagera, Dar, n.k.; UDP wakaelekeza nguvu zao katika maeneo ya Shinyanga na Mwanza; na vyama vingine wakaangalia ni maeneo gani wanahitaji kuweka nguvu zaidi.

Pia ni muhimu wakaendeleza utaratibu wa kuachiana majimbo kulingana na nguvu za kichama katika maeneo tofauti.

Ni imani yangu kuwa ni kwa njia hii kwa taratibu vyam vinaweza kujiimarisha na kuweza kufanikiwa kuwa na idadi kubwa ya wabunge, vinginevyo miaka nenda miaka rudi wataendelea kuwa idadi isiyo ridhisha.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom