HOJA na VIOJA vya VC-UDSM

Kule kwetu Tandahimba neno "Mukandara" maana yake ni Choo. Sijui ndiyo hicho hicho mnaizungumzia hapa au kitu kingine?
 
Jana ulifanyika Mkutano baina ya Makamu Mkuu wa Chuo-UDSM almaarufu kama VC,Prof.Rwekaza Sympho Mukandara na wafanyakazi wote wa chuo hicho. Washiriki,ambao ni wafanyakazi,walitoa hoja mbalimbali ambazo zilikumbana na majibu ya vioja vya Makamu Mkuu huyo wa chuo.

1.Hoja: Nyumba ya Makamu Mkuu wa Chuo ambayo haikaliwi na mtu yeyote lakini inalindwa na kukarabatiwa kwa gharama kubwa iwekwe mikononi mwa Mhadhiri au Mfanyakazi mwingine ili aweze kuitumia.Hii ni kwasababu Prof. Mukandara anaishi kwenye Hekalu lake kule Makongo Juu.

Jibu-Kihoja LA VC: Nyumba ile kwasasa inatumika kama ukumbi wa 'Functions' mbalimbali.

2. Hoja: Nafasi za kiutawala kuanzia na Makamu Mkuu wa Chuo na Manaibu wake sasa zishikwe na watu wenye weledi wa uongozi na uzoefu uliotukuka badala ya Maprofesa ambao wameshindwa kuonesha ufanisi wao.

Jibu-Kihoja la VC: Acha kazi hapa UDSM ukaipate kwenye Chuo na namna uitakayo.



3. Hoja: Responsibility allowance(imenishinda kuitafsiri kwa Kiswahili) ziwe zinatolewa kwa wafanyakazi wa kada ya chini badala ya wa juu kwakuwa wachini ndio wanaolundikiwa kazi na Wakuu wao.

Jibu-Kihoja la VC: Hiyo haiwezekani

4. Hoja: Kwanini mishahara ilipandishwa kiholela na Chuo ikiwa Hazina hawana taarifa na sasa inashushwa?

Jibu-Kihoja la VC: Kaiulizeni Serikali....sisi tulifanya hivyo kwa nia njema kabisa.

Wana-JF pimeni na mjionee wenyewe...

Mkuu kama haya umeandika hapa jamaa alisema, then jamaa anadharau sijapata kuona and there must be something which give him that power!!
 
Back
Top Bottom