HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

Nakubali, Membe ndiye chaguo bora kwa CCM. Atasaidia sana 'kuleta mageuzi' ya kweli.
Thanks mkuu FJM for joining the team!. Hivi sisi Watanzania, mbona huwa hatujiulizi, sisi ndio tuna wakimbiaji mahiri since time immemorial, kina Filbert Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamis Shanga, Nzael Kiyomo, Juma Ikaangaa etc, etc, Wakenya walikuwa nyuma yetu!. Sasa Wakenya ndio machampioni wa mbio ndefu!, Watanzania..kwishney!, Hivi kuna mnao jiuliza Wakenya wanatushindaje?!. Wakenya wanatushinda kwa ku file, runners na run mates ambao ni wasindikizaji!, wanaitwa "pace makers"!, hawa kazi yao huwa ni kukitimka mbio ili kuwachanganya na kuwachosha opponents washindwe ku-maitain constancy pace! ili the true runner wetu aweze kumaitain his pace, and win the victory!. EL could make a good "pace maker so du Membe!".
P.
 
Rais hatoki tena miji ya mwambao...safari hii ni zamu ya nyanda za juu, kaskazini na ziwa jitihada za kuumiliki u-rais mwambaoni safari hii hazita weza lbd kwa force.
 
Sidhani kuwa CCM inachukiwa kwasababu ya Rais fulani, kinyume chake Rais amebaki kuwa anapendwa na CCM inachukiwa.Chuki dhidi ya CCM si kutokana na watu au haiba zao, si kutokana na sera, ni kutokana na mfumo uliokiuka maana nzima ya chama, kanuni, taratibu na sheria n.k.
Chuki dhidi ya CCM ni kutokana na chama kupoteza umiliki wa wananchi kwa kundi dogo lenye nia tofauti na ile ya CCM.

Uchaguzi wa 2015 hautaongozwa na sura au kashfa za mtu mmoja mmoja. Utaongozwa na dira ya kitaifa na mtazamo.
Kikubwa zaidi ni kuchoshwa kwa wananchi na kundi teule kuiweka nchi ilipo kwa miaka 50.

Hakuna kiongozi aliye ndani ya CCM au serikali yake anayeweza kuja na hadithi tofauti.
Membe kama walivyo wengine hajaweza kusimama katika masilahi ya taifa.
Hajakwepa kashfa kwasababu anaposhindwa kuueleza umma nini kimetokea kwa kujificha nyuma ya bunge na serikali hana maadili, uthubutu au utashi wa kisiasa.

Lakini hatuhitaji kiongozi wa uchumi na siasa tu, tunahitaji kiongozi atakayewaunganisha Watanzania na kurudisha Tanzania isiyo na makundi ya kikabila au kidini. Membe ameshindwa mtihani huo kwa kuanzia.

Naamini kuwa ili CCM ijirudishie hadhi ni lazima mgombea wa 2015 atoke nje ya 'system' iliyopo.
Na sidhani kuwa ni suala la nani atakuwa rais, bali chama gani kinaweza kututoa hapa tulipo!
Nimeipenda sana hii post. Kingekuwepo kitufe cha like
ningekugongea like
 
Huwa nakukubali sn ila kwa hili sikubaliani nawe hata kidogo, membe ni kiongozi asiye na subila na uwezo wake wa kiutendaji ni mdogo pia kashifa nyingi zilitakiwa zmezuiliwa na ofisi yake hasa hawa wawekezaji wanaohujum nchi toka nchi za ulaya. Huyu membe hafai kabisa kuwa rais hta ktk nafasi ya uwaziri imemshinda
 
MM naomba nichakachue thread yako kama inavyoendelea kuchakachuliwa.
Mara nyingi natatizika sana kila ninaposoma habari za fulani ni best candidate.
Hapa ndipo nakubaliana na Mkandara kuwa elimu ya uraia bado ni tatizo kubwa sana.

Wenzetu wanaojua kuchagua viongozi huangalia kigezo kimoja hadi kingine:
Maadili ya mtu, misimamo yake kisiasa, anasimamia nini, mahusiano na wenzake, mahusiano na chama chake, ushiriki katikashughuli za kijamii, maadili yake, mahusiano kati yake na wananchi, mtazamo wake kuhusu nchi, historia ya utendaji wake, maamuzi aliyowahi kuayafanya huko nyuma, uthubutu katika kusimamia anachokiamini n.k.

Tunatakiwa twende mbali zaidi ya hapa pa kusema fulani atatusaidia.
Labda nitoe mifano kidogo, ni Membe aliyetuambia kuwa tumeibiwa katika Radar, ni Membe aliyekataa kutuambia nani ni wezi. Alichotaka ni ku-score political point kuwa pesa zimerudi! Sasa huyu mtu kimaadili unamweka kundi gani?
Nina nani miongoni mwetu anayejua misimamo ya Membe kuhusu masuala ya kitaifa?

Mfano wa pili, ni Lowasa huyu aliyetuambia hakuna wizi Richmond, ni Lowasa huyu aliyejiuzulu kwa dhambi anayosema hakuitenda, ni Lowasa huyu anayesema alifanya hivyo kuilinda serikali, ni Lowasa huyo asiyetuambia nani alibofoa Richmond hadi leo tunapata hasara. Ushujaa wa kusema huyu ni best candidate unakuwa katika misingi gani?
Ni nani anayeweza kunishawishi kuhusu uadilifu wa Lowasa hadi apewe ofisi kubwa kiasi hicho?Ni nani anayeweza kutumia vigezo ilivyoweka kumpa pasi Lowasa japo 60%?

Kama ni suala la kusema tu fulani anafaa basi mimi nasema Sophia Simba anafaa kama best candidate.
Msiniulize kwa vigezo gani kwasababu lengo ni kutaja tu.
 
hapa mzee unajikosha tu, lakini within the context, we know who you are and what you actually meant katika andiko lako la kwanza, kuna watu walikuwa wanakusubiri kwa hamu sana provided that you have started showing your hidden agenda, the saga is with you wait a bit. TANZANIA Si Kiongozi, ama Tajiri, ama Mchambuzi nguli( mwanakijiji), ama CCM ama UPINZANI, ama Masikini ambaye ni wa kumwamini wengi wao wanahubiri , kuishi na kusema wasichokiamini ndani ya mioyo yao.

Ooh boy...! haya unajua kilichomo moyoni mwangu. Kadizooo
 
Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
I wish tungekuwa na nafasi ya kupush vya kutosha, basi tungetumia nafasi hiyo kujihakikishia kuwa CDM inachukua nchi ifikapo 2015. Ni kweli Membe ni mzuri, lakini hakika Membe hana ubazu hata kidogowa kuzichanga na EL. Hakika mziki utakuwa mzito zaidi endapo EL atasimama kuliko akisimama Membe. Sijawahi kum-beza hata kidogo EL
 
Mzee Mwanakijiji hajasema kwamba Membe anafaa kuwa Rais bali anafaa kuwa Mgombea Urais kupitia CCM kuliko wenzie wote wanaotajwa. Kama kushinda au kushindwa hilo ni suala jingine kabisa linalohitaji mjadala wake!!

Brilliant mind!!! Post yangu ya awali kwa makusudi kabisa haijasema Membe anafaa kuwa Rais wa Tanzania au mgombea yeyote wa CCM kuwa anafaa kuwa Rais wa Tanzania...
 
Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?

"Nikisema nitagombea urais nitapakwa matope puani na machoni hadi nitashindwa kuchukua na hizo fomu… kuna watabiri wa ajabu na uongo ambao wamezuka kuwatabiria watu. Hata usipoomba wanapata jina lako wanakuchukulia fomu na kukupigia kura na kukwambia wewe utapata asilimia fulani… mtu anakwambia hivyo wakati hata hujatamka wala hujachukua fomu" - source Membe mwenyewe.

Haya bana. Naona kuna mwingine kule kaanzisha thread ya kumetetea Dr. Migiro kugombea urais kwa kuwa eti hana kashfa, si fisadi na hana doa. Na wewe hapa unasema Membe hana kashfa. Kama kigezo cha kugombea urais Tanzania ni kutokuwa fisadi, kutokuwa na doa au kashfa si hata wewe Mwanakijiji unaweza kuchukua fomu fasta na kugombea? Au una kashfa?

Siyo kweli kuwa kama Membe "hataoteshwa" kugombea urais, basi ndio itakuwa mwisho wa CCM. Tatizo sio mgombea. Tatizo ni system ya chama chenyewe na Watanzania kwa ujumla. CCM inaweza kumweka mgombea yoyote hata kama ni fisadi, ana doa au kashfa na akashinda vile vile. Sababu ni kwamba kwa sasa Watanzania wengi sana hawana mpango wowote wa ku-replace system ya sasa na system mpya.

CCM wataweka mtu yoyote na kushinda simply because most Tanzanians are sad, but not angry with what is going on in their own country. Soma posts kibao hapa JF na kule facebook nyingi zinaanza na "Ee Mungu wetu tusaidie kuondoka na hili tatizo". Ni full maombi tuu. "Usually when people are sad, they don't do anything. They just cry over their condition. But when they get angry, they bring about a change." – Malcolm X.
 
Mkuu Bajabiri, hii inaitwa "negation"!, kukanusha kitu ambacho ni facts!.
Huwezu kukanusha hard facts ili tuu ku ji please nafsi yako!.
  1. CCM ni chama cha siasa chenye usajili wa kudumu, na ndicho chama klilichopata certficate of registration as Nambari One Tanzamnia political Party!. This is a fact, you can't deny it!, unless ni kujifurahisha!.
  2. CCM ndicho chama tawala Tanzania kwa sasa, uwe ulikichagua or not, CCM ndicho kinachotawala and this is a fact!, you can't deny it unless unajifurahisha!.

Mkuu Bajabiri na wengine, tujenge utamaduni wa kuwa wakweli toka kwenye nafsi zetiu kwa kuzikubali hard facts
kuwa CCM ni chama, kipo, ndicho chama tawala!, sasa suala la kuendelea kuwepo baada ya 2015, au kuendelea
kutawala baada ya 2015, hivyo ndio debatable subject subject based on political probabilities!.

P.

pasco mi nakuelewa sana,pamoja na kuwa chama cha kwanza kusajiliwa,pamoja na kwamba ndo kimeunda serikali,lakini kwa sasa ccm kimepoteza uhalali wa kuiongoza tanzania,na sababu ni wale waliomo ndani ya CCM,
hata kiwe kna miaka 200 kwa ukongwe,hakuna msafi tena pale CCM,ndo maana hata minyukano yao yote wana ccm imekaa kimaslah yao binafsi
 
Mkuu napendekeza ccm wamsimamishe white hair au bibi kiroboto

Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
 
Ukiangalia sana
kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye
anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia
chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa
aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na
mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki
kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia
inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential
candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya
kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa
ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?

Ka akigombea Membe urahisi coz sio urais basi hata tlp watachukua nchi
 
MM naomba nichakachue thread yako kama inavyoendelea kuchakachuliwa.
Mara nyingi natatizika sana kila ninaposoma habari za fulani ni best candidate.
Hapa ndipo nakubaliana na Mkandara kuwa elimu ya uraia bado ni tatizo kubwa sana.

Wenzetu wanaojua kuchagua viongozi huangalia kigezo kimoja hadi kingine:
Maadili ya mtu, misimamo yake kisiasa, anasimamia nini, mahusiano na wenzake, mahusiano na chama chake, ushiriki katikashughuli za kijamii, maadili yake, mahusiano kati yake na wananchi, mtazamo wake kuhusu nchi, historia ya utendaji wake, maamuzi aliyowahi kuayafanya huko nyuma, uthubutu katika kusimamia anachokiamini n.k.

Tunatakiwa twende mbali zaidi ya hapa pa kusema fulani atatusaidia.
Labda nitoe mifano kidogo, ni Membe aliyetuambia kuwa tumeibiwa katika Radar, ni Membe aliyekataa kutuambia nani ni wezi. Alichotaka ni ku-score political point kuwa pesa zimerudi! Sasa huyu mtu kimaadili unamweka kundi gani?
Nina nani miongoni mwetu anayejua misimamo ya Membe kuhusu masuala ya kitaifa?

Mfano wa pili, ni Lowasa huyu aliyetuambia hakuna wizi Richmond, ni Lowasa huyu aliyejiuzulu kwa dhambi anayosema hakuitenda, ni Lowasa huyu anayesema alifanya hivyo kuilinda serikali, ni Lowasa huyo asiyetuambia nani alibofoa Richmond hadi leo tunapata hasara. Ushujaa wa kusema huyu ni best candidate unakuwa katika misingi gani?
Ni nani anayeweza kunishawishi kuhusu uadilifu wa Lowasa hadi apewe ofisi kubwa kiasi hicho?Ni nani anayeweza kutumia vigezo ilivyoweka kumpa pasi Lowasa japo 60%?

Kama ni suala la kusema tu fulani anafaa basi mimi nasema Sophia Simba anafaa kama best candidate.
Msiniulize kwa vigezo gani kwasababu lengo ni kutaja tu.

mdau nazifatilia comment zako,unafafanua vizuri sana,,,,,,membe jimbo limemshinda nchi ataiweza?????
Membe anasema tayari anamaadui,na aliahidi kuwatatja,je si kwamba ataendeleza siasa za jk za visasi????
Kwenye Color hakuna cha kuongeza,hawa wanaowapigia kelele akina membe na Lowassa ni waramba nyayo tu,,,baadae wapewe U-DC
 
Sawa wacha niseme kwamba tuna mawazo tofauti juu ya hili (ndio demokrasia yenyewe hiyo) labda hatujaelewana na tunaongelea vitu viwili tofauti! Tukubali kutofautiana!
Mkuu wangu nimekuelewa sana na nimewahi kusema wanawake jinsi wasivyopenda kumpa support mwanamke mwenzao nadhani ilikuwa mada fulani aloileta marehemu Mpiganaji na mbunge wetu wa viti maalum. Hilo lipo wazi wala halina Ubishi isipokuwa pale Umoja wa wananwake unapohusika ama kushirikishwa hasa ktk siasa zetu nimegundua kwamba wana nguvu kubwa sana ya ushawishi maana JK mwaka 2010 alikuwa ktk hali mbaya sana kisiasa. Na nachelea kusema kwamba mwaka 2010 CCM walikuwa ktk hali mbaya zaidi na uwezekano wa kushndwa vibaya ulikuwa wazi lakini mbinu zao za kutumia mgawanyiko wa wananchi ktk makundi ya kijamii ulitumika kama kawaida yao hasa pale wanapobanwa kona..Hivyo, mbegu walobakia nayo ni AshaRose maana ktk Udini na Ukabila wameshindwa kukivuruga CDM -Tujiandae kwa hilo..
 
Kwa Kanuni ya ushindi: Mshindi ni Mshindi, CCM kupata 50.1% dhidi ya Chadema 49.9%, CCM ni mshindi. Membe au mgombea mwingine yeyote atakayesimamishwa na CCM, hasa wale wote ambao tayari wapo masikioni mwa Watanzania watapita kwa urahisi sana dhidi ya Chadema chini ya kanuni hii ambayo Chadema kwa sababu tusizojua hawaonekani kuwa na jitiada zozote za kuifanyia kazi. Vinginevyo katika siasa za Tanzania kuelekea 2015 zinazotawaliwa na "innocent until proven guilty, lakini muhimu zaidi, guilty only if you dont have money to buy justice, any publicity is good publicity, iwe ya ufisadi, kukamatwa ugoni n.k;
 
Mzee Mwanakijiji,
Sintopendekeza mtu isipokuwa kwa manufaa ya taifa na japokuwa Membe ni kichwa, muweza ukiachana na habari za Ufisadi wake maana huko CCM hakuna msafi kihivyo. Wayahudi walilaaniwa tena na Mungu mwenyewe lakini bado wanaitawala dunia.

Hivyo pamoja na utetezi wako bado nakuhakikishia kwamba CCM wataweza tu kushindana ikiwa watamsimamisha Asha Rose Migiro na hii itatokana na WANAWAKE kutumia kauli mbiu ya TUKIWEZESHWA TUNAWEZA. Itakuwa sio swala la chama bali wanawake against the rest...Na amini maneno yangu watu hawatatazama tena nyuma wala kutazama uwezo wa AshaRose isipokuwa ni mageuzi ambayo kwao yatawalemaza akili..

Kwa upande wa ushindani na hasa Chadema wanatakiwa kuanza mapema sana kumtafuta na kumwandaa mgombea japo kwa siri lakini nawatahadharisha mapema - KAZI IPO 2015 wajipange mapema na vizuri sana laa sivyo itakuwa aibu maana elimu ya Uraia haijazama vichwani mwa wananchi hivyo SHIDA na MATATIZO yanatangulia Mapenzi yao..

Mkuu Mkandara: Tafadhali angalia hapo nilipoweka red!! Kwa kutumia hiyo kauli mbiu inaashiria ufanisi bora? Hili la kusema kuwa wanawake wakiwezeshwa wanaweza bado ni kitendawili kwa hapa Tanzania. Wanawake watendaji wamewezeshwa kielimu na kwa semina elekezi lakini mazingira ya kazi si rafiki kwao. Je wanawake walio madarakani wamewezaje kuwakomboa wananchi kutokana na mateso ya umaskini, ujinga na maradhi. Tuchukulie mfano wa wabunge, viongozi wanawake kwenye mawizara, wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wa wilaya hivi wameonyesha utendaji uliotukuka tofauti na wanaume wenye nafasi kama hizo? Swali moja tu je, ubadhirifu wa mali ya umma haupo kwenye sehemu ambazo wanawake wanaongoza? Bila kubadilisha mfumo uliopo hata wanawake wakipewa nafasi zote za uongozi bado ni tabu na shida tu.
 
Back
Top Bottom