Hoja binafsi

Revolution

JF-Expert Member
Feb 28, 2008
790
549
Salamu nyingi sana ziwafikie wanachama wote wa jamiiforums,

Nimekuwa mwanachama wa mtandao huu wa kijamii tangu mwaka 2008 na nikiri ya kwamba nimejifunza mengi sana mazuri na nimeelimika sana kwa maoni, taarifa na michango mbalimbali za wanachama. Pia nimekuwa nikivunjwa mbavu na baadhi ya jokes za wanachama, kwa ujumla JF ni zaidi ya mtandao wa kijamii kwangu.

Trend ya uchangiaji na ukosoaji kwa kuheshimiana, kuheshimu mawazo na fikra za members, kuheshimu utashi, imani, itikadi na mielekeo ya mirengo ya wanachama ilikuwa ni nzuri sana kwa kipindi kile nilipojiunga (ninaamini hali ilikuwa hivyo kabla sijajiunga pia). Kadri siku, miezi na miaka ilipozidi kusogea na ndivyo wanachama walivyoendelea kujiunga kwa kasi kubwa (ninaamini kasi hii kubwa ilikuwa inatokana na msukumo wa vuguvugu la hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, wananchi wengi kupanuka kimawazo na kwa kiasi fulani ukuwaji wa demokrasia nchini kwetu pamoja na ukuwaji mkubwa wa sekta ya technohama bila kusahau umaarufu wa JF uliokuwa unasambaa mitaani na kila kona kila kukicha).

Ukuwaji wa JF umekuja na changamoto nyingi lakini mojawapo ambayo ni lazima wanachama pamoja na moderators wa mtandao huu tuikemee ni hili suala la kukashfiana juu ya imani zetu, hili suala litazidi kudidimiza umaarufu wa JF na litaweza kabisa kuondoa malengo ya kuwepo mtandao huu. Ninapendekeza moderators wajaribu kuzuia threads ambazo kwa namna moja wataona zina lengo la kukashfu, kuaibisha au kutania imani yoyote inayohusu mambo ya dini na kuabudu.

Kuamua ni kuchagua na wakati wa kuchagua ni sasa.

Naomba kutoa hoja.
 
Mawazo yako mazuri ila kumbuka katika msafara wa mamba na kenge wamo. Wanaokashifu, wanaotukana, wajinga hawawezi kukosekana pamoja ni kwamba mtandao huu ni kwa watu wenye busara.
 
Back
Top Bottom