Hofu yatanda kufuatia kumwagwa sumu kwenye Mto Ruvu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
HOFU kubwa imetanda kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake na wale wakazi wa Mkoa wa Pwani kufuatia sumu iliyomwagwa na wavuvi katika mto Ruvu kwa lengo la kuvua samaki.
Taarifa hizi zilithibitishwa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASCO), Mary Lyimo jana jijini Dar es Salaam.



Lyimo amesema kuwa, tukio hilo limefanywa na wavuvi haramu ambao walikwenda katika mto huo na kufuta eneo lililotulia katika mto Ruvu na kisha kumwaga sumu kwa nia ya kuua samaki.

"Hawa wavuvi haramu walikuwa wakitafuta samaki katika mto Ruvu kisha wakaenda katika eneo lililotulia na kumwaga sumu kwa nia ya kutaka kuua samaki," amesema afisa uhusiano huyo.

Amesema kuwa baada ya DAWASCO kupata taarifa kuhusiana na kuwepo taarifa hizo walilazimika kwenda umbali wa Kilomita 70 kutoka kwenye mtambo wa Ruvu.

Amesema kuwa baada ya kufika eneo hilo ambalo ni mbali na maji yanayotumiwa wananchi walilazimika kupima na kubaini kuwepo kwa umwagaji wa sumu.

Amesema kuwa walibaini kuwa sumu iliyomwaga haina madhara kwa binadamu isipokuwa inauua samaki tu.

Alithibitisha na kusema kuwa baada ya kupima sumu hiyo walibaini kuwa haina madhara kwa binadamu isipokuwa inaua samaki tu.

Hata hivyo amesema kuwa endapo mkazi yeyote atapata madhara kuhusiana na utumiaji wa maji hayo anashauriwa kufika katika ofisi hizo.

Amesema kuwa kutokana na hofu hiyo baadhi ya watu wamekamatwa na wanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Mlandizi.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absolom Mwakyoma amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa watu wanne wanashikiliwa na polisi kufuatia tukio hilo linalowafanya wananchi kutokuwa na imani na nchi yao.

Kamanda huyo amesema kuwa watu hao walikamatwa jana wakiwa na samaki wanaodhaniwa na sumu pamoja na maji.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Saidi Hucha (42), Hassan Shabani (22), Salumu Mohamed (23) na Alfan Sima (19) wote wakazi wa Mlandizi.

Amesema kuwa samaki na maji vimechukuliwa kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupimwa.

Taarifa zaidi juu ya sakata hili litawajia na majibu yatakayotoka kwa mkemia mkuu


http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3284350&&Cat=1
 
Back
Top Bottom