dm2000inter
Member
- Oct 27, 2010
- 29
- 10
Ama kweli CHADEMA imeishika pabaya CCM. Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Moshi mjini,Bernadette Kinabo leo amepiga marufuku sherehe za mahafali ya sekondari ya Majengo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi kwa sababu itaipa ujiko Chadema. Taarifa za maofisa usalama zinadai mkuu wa shule hiyo aliitwa leo saa 3:00 asubuhi na Kinabo na kuambiwa afute Graduation hiyo iliyokuwa ifanyike Jumamosi ya Tarehe 30.10.2010 hadi uchaguzi utakapomalizika. Inaelezwa kuwa mkuu wa shule hiyo alielezwa wazi kuwa maagizo hayo ni maelekezo toka ngazi za juu. Taarifa ni kwamba Academic Master wa shule hiyo, Pantaleo Minja anagombea Udiwani kata ya Majengo kwa tiketi ya Chadema na ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kushinda. Shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 2,800 na wanafunzi 1,600 wamejiandikisha kupiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura. Uamuzi huu wa serikali umechochea hasira ya wazazi na wanafunzi kwa kuwa baadhi ya wazazi walishakodisha kumbi kwa ajili ya kuwapongeza watoto wao, kutoa order za cake na kadha wa kadha. Swali la kujiuliza ni je Uamuzi huu wa msimamizi umekisaidia CCM au ndio umekimaliza zaidi kisiasa?Jibu unalo kwa kichwa....:sad: