Hofu ya mauaji yaikumba kesi ya Wakili Mwalle • MMOJA ADAIWA KUFA BAADA YA KUTOA TAARIFA NZITO

Kowakdengo

Member
Mar 20, 2012
21
12
amka2.gif
Hofu ya mauaji yaikumba kesi ya Wakili Mwalle
• MMOJA ADAIWA KUFA BAADA YA KUTOA TAARIFA NZITO

KESI ya wakili maarufu nchini, Median Mwalle, imechukua sura mpya baada ya wakili huyo kuibua madai mazito mahakamani kuwa mmoja wa watu wake wa karibu, John Kabwe, alifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha siku chache baada ya kumpa taarifa muhimu.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi, Charles Magesa, anayesikiliza shauri la jinai namba 330/11, Mwalle alisema mtu huyo alikufa mara tu baada ya kuwa amemweleza mambo fulani muhimu na mazito kwa ajili ya kesi yake.
Hata hivyo hakueleza kwa kina kifo cha Kabwe kilitokea lini lakini alisema kuwa siku chache kabla ya kifo chake alikwenda kuzungumza naye na alimweleza mambo muhimu ambapo alishitushwa baada ya siku chache kupata taarifa kuwa amefariki dunia.
Taarifa ya wakili huyo ambayo iliwashitua watu wengi waliofika mahakamani hapo jana, aliongeza kuwa kifo hicho kimetokea huku kukiwa na vitisho vya kuuawa kwake na wale wanaomsaidia katika kesi hiyo.
Alibainisha kuwa hata baadhi ya wafanyakazi wake wamekuwa wakikamatwa ovyo na polisi na kuswekwa ndani bila sababu za msingi.
“Mheshimiwa, mfanyakazi wa kampuni yangu, Said (Kivuyo) alikamatwa akawekwa rumande kwenye kituo cha polisi siku moja, kosa lake ni kuwaandikia barua akiwataka warejeshe magari yangu ambayo waliyachukua kinyume cha sheria pamoja na simu zangu za kiganjani kama mahakama yako ilivyoamua.”
“Kijana wangu mwingine, Mruma (Yusuph) ambaye huniletea chakula magereza naye alikamatwa na kuwekwa rumande Kituo cha Kati cha Polisi siku tano,” wakili huyo alilalamika mahakamani hapo.
Aliwataja wanaotishia maisha yake kuwa ni pamoja na mawakili wa serikali, Neema Ringo , Fredrick Manyanda, polisi waliopeleleza shauri lake; warakibu wsaidizi wa Polisi (ASP) Seleman Nyakulinga na fadhili Mndeme pamoja na Ofisa Usalama wa Taifa aliyemtaja kwa jina moja la Canute.
Alisema kuwa anapata wasiwasi huo kutokana na ukweli kuwa watu wote hao kwa pamoja humfuata mahabusu kwenye Gereza la Mkoa la Kisongo akitaka kumchukua kwa hati maalumu (removal Order) wakitaka wampeleke kituo cha polisi kwa mahojiano ambapo huwa anakataa lakini anashangaa kuwa akija mahakamani siku ya kesi huwa hawatoi maombi hayo ya kutaka kumhoji.
“Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama yako tukufu iweke kumbukumbu maisha yangu yako hatarini. Wanakuja gerezani wanaomba wanichukue wakanihoji kwa siku tatu au masaa mawili. Tena wanawalaumu maafisa wa magereza kuwa kwa nini hawanitesi, kwa kuwa wanaona afya yangu haijabadilika,” alilalama wakili huyo.
Mwalle alisema kuwa kinachofanywa na maofisa hao wa serikali haamini kama ni maelekezo ya serikali bali wanayafanya kwa kusukumwa na utashi wao binafsi baada ya kubaini masuala wanayomtuhumu nayo na kumshitaki hayana ukweli hivyo wanadhani akitoka ataifungulia kesi serikali jambo alilosema hafikirii kufanya.
“Mimi siwezi kuishitaki serikali yangu ambayo imenisomesha mpaka nikawa wakili, ninachokiona mheshimiwa hakimu ni kuwa hawa kina Nyakulinga wanataka wanichukue kwa kuwa wanajua nina presha wanaweza kunifanyia jambo lolote ili presha yangu ipande nife,” alilalamika wakili Mwalle.
Aidha, alilalamikia taarifa za uongo zinazoenezwa kuwa alipokamatwa alikuwa na sh milioni 20 alizodai kuwa ni za matumizi madogo na kwenye akaunti yake alikutwa na fedha chafu shilingi bilioni 28 na akaunti nyingine shilingi bilioni 19 huku wakimhusisha na kundi la kigaidi la Al Shabab, jambo alilosema kuwa si kweli kwani katika kesi zilizopo mahakamani hapo hakuna hata moja inayohusiana na mambo hayo.
Kwa upande wake wakili wa serikali, Timon Vitalis, alimtoa wasiwasi Wakili Mwalle kwa kumweleza kuwa hawawezi kumuua kutokana na ukweli kuwa wakimchukua gerezani taarifa zitaonyesha amechukuliwa na nani na muda gani.
Hata hivyo alisema kuwa suala hilo ataliwasilisha kwenye ofisi zao ili kuwezesha haki kutendeka na Mwalle aione kutendeka ambapo alisema kama itabidi itaundwa tume ya kuchunguza suala hilo.
Hakimu Magesa alisema kwa kuwa jalada la kesi hiyo liko Mahakama Kuu kwa ajili ya kufanyiwa mapitio baada ya upande wa serikali kutoridhika na uamuzi wa kutakiwa kurejesha magari ya Mwalle, aliahirisha shauri hilo mpaka Aprili 11, mwaka huu siku ambayo Mahakama Kuu itakuwa inapitia maamuzi hayo ambapo wakimaliza ndipo litarejea kwake.
Alisema kuwa anaamini magereza wanajua utaratibu wa kuingia na kutoka mahabusu ingawa alimtaka wakili wa serikali Vitalis kupeleka malalamiko hayo kwenye ofisi zao ili yaweze kushughulikiwa.
Mawakili hao wa serikali wamekata rufaa Mahakama Kuu wakitaka ipitie maamuzi yaliyofanywa na mahakama hiyo yakiwaagiza Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DPP), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha kuyarudisha magari saba na simu za mkononi kwa wakili huyo anayetuhumiwa kupatikana na fedha chafu.
Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Magesa, ambaye alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote, mahakama yake imeridhika kuwa mamlaka hizo zilikamata magari hayo kinyume cha sheria ya matunda ya uhalifu (Proceeds Crimes Act) pamoja na vifungu namba 41 na 44 vya sheria ya mwenendo wa kesi za jinai.
Magari yaliyoamriwa na mahakama kurejeshwa kwa Mwale ni T 690 BEW aina ya Range Rover, T 643 BTS Land Rover Discovery, T 907 BTS BMW, T 118 BRS Cadillac Escalade, T 499 APX Land Cruiser, T 520 BBJ BMW, ambayo yalichukuliwa Novemba mosi, pamoja na gari T 660 BCG Toyota Chaser lililokamatwa Desemba 8, mwaka jana.
 
duh hii kesi nimeshindwa kuielewa kabisa . sasa kwani ameshtakiwa kwa makosa gani ?
 
Sijui kama huyu Mwalle anaweza akawa na pesa chafu au la, lakini nijuacho ni kwamba Nyakulinga amekuwa anatumika sana kuwabambikizia kesi vijana wengi wa kitanzania ambao wana mafanikio ya hapa na pale. Trick kubwa ambayo huifanya ni kufunga account zao za benki na kuwanyang'anya magari yao ya kifahari wakiwa na imani ya kuja kuyanyang'anya. Kuna jamaa walimbambikia uhujumu uchumi huko Mbeya, na wameshindwa kumfungulia kesi mpaka sasa. Utashangaa waendapo kumhoji mshtakiwa, akina Nyakulinga huwa wanadai mtuhumiwa awaachie wafanyakazi wake wa zamani (ambao wanatumika kumtolea mashtaka ya uongo) gari lake la kifahari. Hili jambo la ajabu, limefika mpaka ofisi kubwa za hapa jijini, lakini wala hawamsaidii kijana wa watu, japo wanajua kabambikiwa.
 
amka2.gif
Hofu ya mauaji yaikumba kesi ya Wakili Mwalle
• MMOJA ADAIWA KUFA BAADA YA KUTOA TAARIFA NZITO

KESI ya wakili maarufu nchini, Median Mwalle, imechukua sura mpya baada ya wakili huyo kuibua madai mazito mahakamani kuwa mmoja wa watu wake wa karibu, John Kabwe, alifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha siku chache baada ya kumpa taarifa muhimu.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi, Charles Magesa, anayesikiliza shauri la jinai namba 330/11, Mwalle alisema mtu huyo alikufa mara tu baada ya kuwa amemweleza mambo fulani muhimu na mazito kwa ajili ya kesi yake.
Hata hivyo hakueleza kwa kina kifo cha Kabwe kilitokea lini lakini alisema kuwa siku chache kabla ya kifo chake alikwenda kuzungumza naye na alimweleza mambo muhimu ambapo alishitushwa baada ya siku chache kupata taarifa kuwa amefariki dunia.
Taarifa ya wakili huyo ambayo iliwashitua watu wengi waliofika mahakamani hapo jana, aliongeza kuwa kifo hicho kimetokea huku kukiwa na vitisho vya kuuawa kwake na wale wanaomsaidia katika kesi hiyo.
Alibainisha kuwa hata baadhi ya wafanyakazi wake wamekuwa wakikamatwa ovyo na polisi na kuswekwa ndani bila sababu za msingi.
"Mheshimiwa, mfanyakazi wa kampuni yangu, Said (Kivuyo) alikamatwa akawekwa rumande kwenye kituo cha polisi siku moja, kosa lake ni kuwaandikia barua akiwataka warejeshe magari yangu ambayo waliyachukua kinyume cha sheria pamoja na simu zangu za kiganjani kama mahakama yako ilivyoamua."
"Kijana wangu mwingine, Mruma (Yusuph) ambaye huniletea chakula magereza naye alikamatwa na kuwekwa rumande Kituo cha Kati cha Polisi siku tano," wakili huyo alilalamika mahakamani hapo.
Aliwataja wanaotishia maisha yake kuwa ni pamoja na mawakili wa serikali, Neema Ringo , Fredrick Manyanda, polisi waliopeleleza shauri lake; warakibu wsaidizi wa Polisi (ASP) Seleman Nyakulinga na fadhili Mndeme pamoja na Ofisa Usalama wa Taifa aliyemtaja kwa jina moja la Canute.
Alisema kuwa anapata wasiwasi huo kutokana na ukweli kuwa watu wote hao kwa pamoja humfuata mahabusu kwenye Gereza la Mkoa la Kisongo akitaka kumchukua kwa hati maalumu (removal Order) wakitaka wampeleke kituo cha polisi kwa mahojiano ambapo huwa anakataa lakini anashangaa kuwa akija mahakamani siku ya kesi huwa hawatoi maombi hayo ya kutaka kumhoji.
"Mheshimiwa hakimu naiomba mahakama yako tukufu iweke kumbukumbu maisha yangu yako hatarini. Wanakuja gerezani wanaomba wanichukue wakanihoji kwa siku tatu au masaa mawili. Tena wanawalaumu maafisa wa magereza kuwa kwa nini hawanitesi, kwa kuwa wanaona afya yangu haijabadilika," alilalama wakili huyo.
Mwalle alisema kuwa kinachofanywa na maofisa hao wa serikali haamini kama ni maelekezo ya serikali bali wanayafanya kwa kusukumwa na utashi wao binafsi baada ya kubaini masuala wanayomtuhumu nayo na kumshitaki hayana ukweli hivyo wanadhani akitoka ataifungulia kesi serikali jambo alilosema hafikirii kufanya.
"Mimi siwezi kuishitaki serikali yangu ambayo imenisomesha mpaka nikawa wakili, ninachokiona mheshimiwa hakimu ni kuwa hawa kina Nyakulinga wanataka wanichukue kwa kuwa wanajua nina presha wanaweza kunifanyia jambo lolote ili presha yangu ipande nife," alilalamika wakili Mwalle.
Aidha, alilalamikia taarifa za uongo zinazoenezwa kuwa alipokamatwa alikuwa na sh milioni 20 alizodai kuwa ni za matumizi madogo na kwenye akaunti yake alikutwa na fedha chafu shilingi bilioni 28 na akaunti nyingine shilingi bilioni 19 huku wakimhusisha na kundi la kigaidi la Al Shabab, jambo alilosema kuwa si kweli kwani katika kesi zilizopo mahakamani hapo hakuna hata moja inayohusiana na mambo hayo.
Kwa upande wake wakili wa serikali, Timon Vitalis, alimtoa wasiwasi Wakili Mwalle kwa kumweleza kuwa hawawezi kumuua kutokana na ukweli kuwa wakimchukua gerezani taarifa zitaonyesha amechukuliwa na nani na muda gani.
Hata hivyo alisema kuwa suala hilo ataliwasilisha kwenye ofisi zao ili kuwezesha haki kutendeka na Mwalle aione kutendeka ambapo alisema kama itabidi itaundwa tume ya kuchunguza suala hilo.
Hakimu Magesa alisema kwa kuwa jalada la kesi hiyo liko Mahakama Kuu kwa ajili ya kufanyiwa mapitio baada ya upande wa serikali kutoridhika na uamuzi wa kutakiwa kurejesha magari ya Mwalle, aliahirisha shauri hilo mpaka Aprili 11, mwaka huu siku ambayo Mahakama Kuu itakuwa inapitia maamuzi hayo ambapo wakimaliza ndipo litarejea kwake.
Alisema kuwa anaamini magereza wanajua utaratibu wa kuingia na kutoka mahabusu ingawa alimtaka wakili wa serikali Vitalis kupeleka malalamiko hayo kwenye ofisi zao ili yaweze kushughulikiwa.
Mawakili hao wa serikali wamekata rufaa Mahakama Kuu wakitaka ipitie maamuzi yaliyofanywa na mahakama hiyo yakiwaagiza Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini (DPP), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha kuyarudisha magari saba na simu za mkononi kwa wakili huyo anayetuhumiwa kupatikana na fedha chafu.
Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Magesa, ambaye alisema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote, mahakama yake imeridhika kuwa mamlaka hizo zilikamata magari hayo kinyume cha sheria ya matunda ya uhalifu (Proceeds Crimes Act) pamoja na vifungu namba 41 na 44 vya sheria ya mwenendo wa kesi za jinai.
Magari yaliyoamriwa na mahakama kurejeshwa kwa Mwale ni T 690 BEW aina ya Range Rover, T 643 BTS Land Rover Discovery, T 907 BTS BMW, T 118 BRS Cadillac Escalade, T 499 APX Land Cruiser, T 520 BBJ BMW, ambayo yalichukuliwa Novemba mosi, pamoja na gari T 660 BCG Toyota Chaser lililokamatwa Desemba 8, mwaka jana.

kwenye RED hao ndio mungu wa hapa tanzania,wanatoa roho ya mtu mda wowote wa takao kana kwamba wao wataishi milele

yaani mtu unajisikia muruwaaaaaaaa pale unapojihusisha na kutaka kumtoa roho mwenzako
 
Sijui kama huyu Mwalle anaweza akawa na pesa chafu au la, lakini nijuacho ni kwamba Nyakulinga amekuwa anatumika sana kuwabambikizia kesi vijana wengi wa kitanzania ambao wana mafanikio ya hapa na pale. Trick kubwa ambayo huifanya ni kufunga account zao za benki na kuwanyang'anya magari yao ya kifahari wakiwa na imani ya kuja kuyanyang'anya. Kuna jamaa walimbambikia uhujumu uchumi huko Mbeya, na wameshindwa kumfungulia kesi mpaka sasa. Utashangaa waendapo kumhoji mshtakiwa, akina Nyakulinga huwa wanadai mtuhumiwa awaachie wafanyakazi wake wa zamani (ambao wanatumika kumtolea mashtaka ya uongo) gari lake la kifahari. Hili jambo la ajabu, limefika mpaka ofisi kubwa za hapa jijini, lakini wala hawamsaidii kijana wa watu, japo wanajua kabambikiwa.

hivi huyo anaishi mbinguni? si anaishi na watu? na mnaelewa kabisa kuwa hubambikia watu kesi tena vijana wanaotafuta pesa kwa ugumu?

nikupe mfano mmoja

pale chile,kama wananchi wakigundua kuwa wewe ni polisi na unatumia cheo chako kukandamiza watu na unaishi nao mitaani,wanakupa siku kadhaa tena wanakueleza live na baada ya siku hizo utajuta ukiwa kuzimu,nawapenda sana watu wa chile,sasa hivi hakuna upuuzi kama huo,haki kwa haki
 
habari hii inazidi kuniwekea hofu,ni ajabu sana kuwa afisa wa benki ambaye pia alikuwa shahidi muhimu naye amekufa kifo cha ghafla. Ni ajabu mtu haumwi,alienda kazini kawaida,baada ya mlo wa mchana ktk mgahawa flan alianza kujisikia vibaya,akaenda hosp.kupima presha akakuta very normal,akaenda kupumzika yapata sa11 ila kufikia sa4 usiku tar21 machi,akafa ghafla. Kifo chake japo hakiwezi kuhusishwa na iyo kesho ila ni kuwa kesi haitapata shahidi muhimu kama yule kwa kuwa alikuwa afisa mwandamizi wa benki
 
Pia kuna tetesi kuwa mfanyakazi mmoja wa crdb alifariki ghafla baada ya kutoa maelezo polisi.
 
Back
Top Bottom