HODI, HODI -- naingia JF:

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Hodi, hodi: nami nimeingia baada ya kuangalia mapambano baina ya haramu na halali (evil and virtue).

Nimekuja kuongeza nguvu upande ule wa haki -- upande wa halali, upande wenye matumaini na neema.

Nionyesheni mafisadi -- na wale wapambe zao wanaowalamba miguu kwa vipande thelathini -- niwanyuke very hard.

Hawa wapambe hawana hoja, kazi yao kuvurugavuruga tu mada.

Watanzania tuendelee kuwasakama hawa na dalili zinaonyesha sasa hivi wanarudi nyuma, kwani daima haki hatimaye hushinda.

Wameanza kuonyesha woga mkubwa wa kushindwa, ndiyo maana sasa wameingilia umafia, wa kutaka kuwaua viongozi waliotukuta, waliojitolea shingo zao kwa ajili ya wengi.

Mwakyembe, Kubenea, Mengi, Dr Slaa, Sitta, Anne Kilango, Selelii, Kimaro, Lembeli, Shellukindo, Ole Sendeka na wengine wengi, jueni kwamba Watanzania wengi (majority) wako nyuma yenu -- hilo msihofu.

Sijui nianze na nani?
 
Mmh mkuu mbona umewajia kwa kasi ivo? Tafadhal angalia watu wasije kimbia nchi
 
Back
Top Bottom