Hodi hodi kutoka kwa Kiranga

Hivi pale mabasi yanaposimamaga na kuwaacha abiria wale Kuku na kununua samaki panaitwaje Kiranga?
Napakumbuka sana,ni njia panda ya kwenda kilwa......
 
Duh,

Nashukuru kwa kunikaribisha na kukumbushana njia ya kwetu Mkuranga mpaka daraja la ahsante Nkapa, Somanga mpaka kanda za Nangurukulu etc.
 
Duh,

Nashukuru kwa kunikaribisha na kukumbushana njia ya kwetu Mkuranga mpaka daraja la ahsante Nkapa, Somanga mpaka kanda za Nangurukulu etc.

Waswahili wamefungulia mgahawa wa "kisasa" pale. Basi sio kulalamikia bei; walikua wamezoea samaki na kuku wa bure pale Somanga, sasa wanauziwa kuku na samaki Tsh. 3000 hadi 4000 wanaona maajabu ya dunia!!

Hongera mkuu, kokote huko kiswahili+kiinglishi!
 
This really beats me-hivyo Kiranga ni mzaramo???

Hahahaha,

This really beats me, hivyo Kiranga hatakiwi kuwa Mzaramo?

Etimology/ mzizi na maana ya neno "Kiranga" unaifahamu ilikotoka?

Utashangaa vipi Mzaramo kuwa na maneno mengi?
 
Ndugu zanguni wajuvi, wadadisi na wengineo,

Mie ndugu yenu Kiranga cha Ngeda wa viunga vya bandari iso salama, Kiranga wa upande wa Mbwamaji, Kiranga wa Mkuranga,kakae Muamini na mwana wa Fundi Shomvi na Sikudhani binti Muhamedi.

Mara nilivyotoka pande za Msanga Kisiju nikaambiwa ukishangaa maajabu ya Rufiji gari kupita juu ya mto hutafika Utete wala Mpwapwa, zaidi ya hapo maendeleo siku hizi yako huku bandari iso salama kwenye majumba yaliyopandiana, nikachungulia nikaona kweli mnafaudu, hata Mbagala na Charambe tu harufu wanaisikia, na mimi nikaona niombe kugonga hodi hodi mnikaribishe mlionitangulia.Nisambe nimenyimwa maji wakati kisima chatitiri.

Salamu sana kutoka Msanga Kisiju, Kilwa Pande, Kilwa Kivinje, Kilwa Kisiwani, Songo Songo, Somanga, Muhoro mpaka pande za Sala Sala na Mkuranga.Ningewatumia pepeta na mabumunda ya motomoto lakini nimeambiwa humu naweza kutuma picha tu, na mie kamera sina, labda siku nyingine wakija wapima viwanja na midarubini yao ile nitawaomba wanipige picha niiweke muone ninavyofukuzana na ngedere na kima. Sasa niage nikimbilie kuangalia hesabu za minazi maana wakwezi na komba hawakawii kumuadhiri mwenzenu huku. Baada ya hapo mkiniona kimya mjue safari ya Mafia imewadia.

Natanguliza ungo wa shukurani

Kwa leo ni hayo tu,

Wasalaam,

Kiranga cha Ngeda Sangala Kandumbwa
Salamu kwa Ekeke, Uliza na Mlemeni!.
 
nakumbuka wakati nasoma minaki tulikuwa tunaenda msanga, masaki kwenda kufuata mihogo siku za weekend...nilikuwa na marafiki wengi wa kirazamo.. I miss them.kwao shule it was like police post, but good friends cant forget that experience.
 
nakumbuka wakati nasona minaki tulikuwa tunaenda msanga masaki kwenda kufuata mihogo siku za weekend...nilikuwa na marafiki wengi wa kirazamo.. I miss then.kwao shule it was like police post, but good friends cant forget that experience.

Hahaha,

Minaki pale pua na mdomo na kwetu. Unapokutana na watu, tisa kati ya kumi hawakupi picha halisi.

Mlifika Mwanarumango?
 
Who's that Kiranga are you talking about??? Kiranga huyuhuyu asiyeisha mapya? Hivi aliishawahi kuwa mpya humu jamvini?huwa namuona kama kitu rather than Mtu,that's Kiranga, my JF model.
 
Last edited by a moderator:
Who's that Kiranga are you talking about??? Kiranga huyuhuyu asiyeisha mapya? Hivi aliishawahi kuwa mpya humu jamvini?huwa namuona kama kitu rather than Mtu,that's Kiranga, my JF model.

yeah,,,He ha a human side in him...take time to meticulously read his posts.....ila sasa huu ndio ulikuwa upigaji hodi makini sio siku hiz bana....glad kwamba I joined the bandwagon to welcome him back in 2009....of course I am his senior in that regard...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom