Hizo kazi maalum za Prof. Mark Mwandosya ni zipi?

Madhara ya Katiba mbovu inayompatia fursa rais kuteua mtu yeyote na idadi yoyote ya mawaziri wakati mwingine kadri anavyoshauriwa au kadri ya maslahi na matakwa ya mke wake au hata watoto wake.

Mbona Dj mbowe kateua idadi ile ile ya mawaziri sawa na mawaziri wa CCM, Kwahiyo Dj Mbowe alishauriwa na JOYCE MUKYA au!??.

Mmeshindwa kuonyesha mfano!. Wote ni ukoo wa panya!
 
Nawashangaa mawaziri wa Kike wa CCM. Yaonesha kuwa "wanabebwa" na usawa wa kijinsia na wanashambuliwa sana na ugonjwa wa Lisuisis, ambao huwapata pale Wabunge makini wa Ushindani wanapotoa hoja ama kuhoji jambo kwa manufaa ya Umma. dalili za ugonjwa huu ni kuhamwa na akili, kutetemeka wanapojibu ama kutoa hoja na wanapojikwaa hivi si Spika, naibu wake ama mwenyekiti anayeyeweza kuthubutu kuwarudisha kwenye mstari.
 
Madhara ya Katiba mbovu inayompatia fursa rais kuteua mtu yeyote na idadi yoyote ya mawaziri wakati mwingine kadri anavyoshauriwa au kadri ya maslahi na matakwa ya mke wake au hata watoto wake.

Ni kweli,kama vile dk Silaa anavyoshauliwa na mama Junior.Maana kuna wakati mama Junior anajibu hoja za kisiasa kwa niaba ya haWALA wake.
 
Sio Kweli Kazi Maalum zinaweza Kuwaiti ht USA wapo mfano SPECIAL ENVOYS na ht UN wapo Ninyi Hamjui Anachofanya URAIS NI TAASISI Hivyo Rais Hawezi Fanya Kazi Zote lazima awe na MTU wa Kumsaidia Wakati mwingine Tusikosoe tu ILI tuonekane Tumesema au Wajuaji Saana TAIFA LA MANUNG'UNIKO

Mmmmh, bado majibu yana ukakasi! Mtu wa kumsaidia ndo nini? Kila Waziri anamsaidia Rais na huo ndo ukweli. Mawazi wa Utumishi,Mahusiano, Utawala bora wako Direct kwa Rais, sasa hao hawatoshi? Achilia mbali kurugenzi mbalimbali pale State House. Lakini pia kila mtumishi wa Umma anamsaidia Rais pia.
 
Wizara hii imeanza zamani. Hata Rashid Kawawa wakati wa JK original alishawahi kuwa Waziri wa Wizara hii, pamoya na Mganga Kingunge wakati wa Mwinyi.
 
Mbona Dj mbowe kateua idadi ile ile ya mawaziri sawa na mawaziri wa CCM, Kwahiyo Dj Mbowe alishauriwa na JOYCE MUKYA au!??.

Mmeshindwa kuonyesha mfano!. Wote ni ukoo wa panya!

Wewe kweli Chimpumu, wala hujui maana ya neno kivulli kwenye baraza mawaziri. Kwa hiyo ulitaka idadi ya Mawaziri isiwe sawa na vivuli vyao! Vivuli viwe vichache.....
 
Sio Kweli Kazi Maalum zinaweza Kuwaiti ht USA wapo mfano SPECIAL ENVOYS na ht UN wapo Ninyi Hamjui Anachofanya URAIS NI TAASISI Hivyo Rais Hawezi Fanya Kazi Zote lazima awe na MTU wa Kumsaidia Wakati mwingine Tusikosoe tu ILI tuonekane Tumesema au Wajuaji Saana TAIFA LA MANUNG'UNIKO

Mkuu, usilinganishe tanzania na UN au USA, tanzania bado ni changa sana kiuchumi kiasi cha kua na waziri ambae kazi zake zingeweza kufanywa na wizara zilizopo chini ya ofisi ya raisi. ni kazi gani hizo maalum ambazo haziwezi kufanywa na wizara nyingine?
 
Badala ya kujibu hoja ya Mkosamali kuhusu kazi maalum ya mh. Mwandosya yeye amemjibu Mkosamali kuwa amekufuru. Na kaongezea msemo kuwa hujafa hujaumbika. Je, hili ndo jibu alilopaswa kujibiwa na waziri huyu? Je kuuliza swali ni kukufuru?

Huyu Celina atakuwa mchepuko wa Mwandosya, basi wagonjwa na walemavu wote wawe mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu ili tuwape hela ya kujikimu
 
Kwa kweli ktk awamu ambazo kumekuwa na wanawake bungeni hii ni ya aina yake. Ni kama walienda kupiga vigelegele na makofi na ivo hawaitaji kutumia akili wala busara hata kidogo, maana hata hayo makofi yanakopigwa, utajiuliza hili nalo lahitaji kupigiwa makofi!!!!! Kusema kweli wanawake wengi bungeni haswa wa chama chetu tawala wameonesha udhaifu mkubwa wakiongozwa na SPIKA WAO MAKINDA. Sioni mwanamke mwenye uwezo wa kushika madaraka muhimu nchi hii
 
Jamani haya maneno tunayoyatoa humu hayawezi kuwa ya great thinkers hata kidogo tunaudharilisha huu mtandao hatuna tofauti na walevi wa gongo. Ni ushauri tu.
 
Tunao mawaziri wengi ambao kwa majirani zetu ktk EAC hawawezi teuliwa hata Ukuu wa Wilaya. Heri kaongea huo ujinga hapa nchini,waulize Watanzania walioko ktk Mashirika ya UN,Taasisi za Kimataifa na Balozi zetu jinsi gani wengi wa Mawaziri wetu na Watendaji wa Serikali wanavyo tia aibu wakienda ktk Mikutano,Semina na Makongamano ya Kimataifa nje ya nchi.
 
Kombani: "Katiba iliyopo inatosha, hakuna haja ya Katiba mpya". Kwa mtu kama huyu, hakuna kitu upstairs!

Alikuwa sahihi. Siku 65 zimekatika nothing done.
Siku ya 57 UKAWA wamekimbia kwenda ZANZIBAR kuidai Tanganyika bila TANU.
Ukawa wametangaza hawarudi bungeni.
Na bila two third hakuna kitu.
The Woman was right and she is still right.
 
Wanawake mnadhalilishwa na wanawake wenzenu waliopo bungeni maana hawaakisi ile asilimia hamsini inayotakiwa bungeni na vyombo vingine vya nchi.
 
Daaah,wakuu nimesisimka mwili mzima juu ya haya majibu,huyu mama kamdhalilisha sana mzee Mwandosya

Hata mimi sijaamini km huyu mama kakosa busra kiasi hicho. Kwamba mzee wa watu kumbe amepewa cheo cha fadhila na hakuna kazi yoyote anayofanya. Kwa mfano kwa kawaida waziri siyekuwa na kazi maalumu huwa na umuhimu kwenye serikali mseto ili asaidie katika kura ya maamuzi. Lakini katika serikali zinazoofuata mfumo wa kijamuhuri waziri wa aina hiyo hana umuhimu. Hata hivi kombani alishindwa tu kusema mwandosya ni mshauri wa rais katika mabo fulani fulani? "Hujafa hujaumbika" ina maana mwandosya sasa kawa mlemavu kabisa anayehitaji msaada nasiyetakiwa kuulizwa tunamlipa kodi zetu kwa sababu gani?
 
Back
Top Bottom