Hizi tabia zinakera sana

Wananikera sana watu wanaopenda kuchanganya lugha za Kiingereza na Kiswahili. Nashawishika kuamini kuwa watu wa aina hiyo hawawezi kuongea kwa ufasaha kwa kutumia moja ya lugha hizo na hivyo kulazimika kuzichanganya.
NN kuna sehemu ulikereka na meno yaliyo na irregular alignment ulikereka in eng na kiswahili, kuchanganya sio majivuno bali ni misamiati tu, ss naona unakereka na kitu ambacho post za nyuma umekichanginyi..
 
1. Utakuta mtu anatembea barabarani huku anavuta sigara hajali kuwa moshi wa hiyo sigara yake unakera watu
2. Mtu anatembea barabarani anatema mate au anapenga kamasi hovyo hovyo kila mahali bila ustaarabu
3. Mtu anakupa business card siku unamtafuta ukipiga namba za simu zilizoko kwenye card hapatikani
4. Hawa wamachinga wanaouza vitu wakitumia kispika saa zote kikisema 'dawa ya mende, mchwa, mba na mapunye inapatikana hapa' kinarudiarudia kwa kweli kinaleta kero
Na mengine mengi yenye kero katika jamii yetu, Hii inakera sana

nenda uarabuni uone
 
inakera sana pale mtu anapokupigia simu, akaona hupokei, hajui upo busy au hujasikia, anaanza kupiga mfululizo kama mara 7 hivi, jamani ukipiga mara moja ukaona haijapokelewa si uache, mwenye simu akikuta miss call kama wewe ni wa muhimu si atakupigia,hii inakera sana
 
Watu wanaojichokonoa puani kutoa makamasi yaliyokauka. Unakuta mtu anajichokonoa mbele ya watu halafu wala hanawi mikono. Na hata kutumia tissue paper hawatumii. Ndiyo maana sipendi kusalimiana kwa kushikana mikono kwa sababu hujui hiyo mikono ya huyo mtu unayesalimiana naye ilikuwa wapi!!
 
sawa kabisa.....watu wengine wanaingia msalani....wakishajiswafi hawanawi na sabuni, hii tabia imekithiri sana uswazi
wamama wengi utakuta anamuosha mtoto baada ya kujisaidia halafu anaenda kukamua nazi.....ndio maana huwa sipendi kula nyumbani kwa watu
 
Watu wanaojichokonoa puani kutoa makamasi yaliyokauka. Unakuta mtu anajichokonoa mbele ya watu halafu wala hanawi mikono. Na hata kutumia tissue paper hawatumii. Ndiyo maana sipendi kusalimiana kwa kushikana mikono kwa sababu hujui hiyo mikono ya huyo mtu unayesalimiana naye ilikuwa wapi!!
na wanaoweka mikono kwenye mapu.. na kwenye ku..
 
na wanaoweka mikono kwenye mapu.. na kwenye ku..

Wee acha tu aisee. Kuna watu wana tabia ya kupenda kujishika shika huko chini.....

Kama alivyosema Preta, hata mimi kula kwa watu aisee huwa ni ngumu sana.....hata kula kwenye migahawa sipendi. Yanayofanyika huko kwenye majiko ukiyaona waweza kuzimia...
 
wengine wanaokera ni mafundi....wakati unampa kazi anakuwa mstaarabu sana....lakini wakati unadai kazi yako anakupiga kalenda....na kwenye simu hapatikani......hii inakera sana
 
Tabia nyingine mbaya ni hii ya kugawanya gazeti.....mtu umenunua gazeti lako anakuja mtu anakwambia umpe ukurasa wa katikati....sipendi hii tabia
 
Duh! umenichekesha aisee....Unakuta mtu anaachia ki "silencer".........anachafua kabisa hali ya hewa
... Halafu anajitia kuwa wa kwanza kuhamaki na kudai kuwa aliyefanya hivyo ameoza utumbo wakati yeye mwenyewe ndio kaoza utumbo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom