Hizi rufaa za NECTA huwa kiini macho?

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
29,041
10,686
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini rufaa mbali mbali za wanafunzi wa kidato cha 4 na 6 pale NECTA. Lakini kwa miaka kadhaa naona matokeo yao ya rufaa kuwa vile vile (matokeo hayabadiliki). Ni kweli wako makini hivyo?
 
Hilo ndo jibu mkuu, ni mara chache sana wanakosea

hili ndilo tatizo la wabongo mkifaulu mnaona wenzenu vilaaza hata kama wameonewa lkn ukweli wote unaonekana vyuo mkikutana na waliopitia diploma wanawakimbiza kishenz mi najua bongo uonevu 2 watto wa wakubwa wakiappeal wanbadilishiwa na kupangiwa shule nzuri
 
Una uhakika na usemacho????kwa taarifa yako mtu akiappeal na maks 5 zikaongezeka wale wote walio sahihisha hilo somo huandika barua ya maelezo kwanini walimkosesha. sasa nani hupenda kufanya hivyo??? na kwa nini wakukoseshe kwa makusudi???? Ukipata majibu ya maswali hayo ndo uje tena, nikupe taarifa zingine.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini rufaa mbali mbali za wanafunzi wa kidato cha 4 na 6 pale NECTA. Lakini kwa miaka kadhaa naona matokeo yao ya rufaa kuwa vile vile (matokeo hayabadiliki). Ni kweli wako makini hivyo?

What is the basis of your doubts?
 
Una uhakika na usemacho????kwa taarifa yako mtu akiappeal na maks 5 zikaongezeka wale wote walio sahihisha hilo somo huandika barua ya maelezo kwanini walimkosesha. sasa nani hupenda kufanya hivyo??? na kwa nini wakukoseshe kwa makusudi???? Ukipata majibu ya maswali hayo ndo uje tena, nikupe taarifa zingine.
Kwani wanaosahihisha hizo rufaa ni wale wale wa;iosahihisha mwanzo?
 
Unategemea mwalimu alietoka kigoma aje asahihishe kwa hiyo buk20??? huchukua waalimu wale walio sahihisha na walio karibu.

Ninaamini wasahihishaji wanakuwa wengine,hivyo inategemewa kuwa na changes.
 
Wanajichanganya sana hao NECTA.. Majibu ya essay huwezi kusahihisha mara mbili na majibu yakawa ni yaleyale...!Maana yake wanawalia watu hera tu!
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini rufaa mbali mbali za wanafunzi wa kidato cha 4 na 6 pale NECTA. Lakini kwa miaka kadhaa naona matokeo yao ya rufaa kuwa vile vile (matokeo hayabadiliki). Ni kweli wako makini hivyo?

Tatizo unao uelewa mdogo kuhusu rufaa. Rufaa haina maana unapokata rufaa inatakiwa ibadilike. Aidha, unapokata rufaa unaonesha kutoridhika na usahihishaji wa awali. hivyo, basi NECTA utafuta wasahihishaji wapya waje wachunguze kwa makini usahihishaji wa awali. Anayekata rufaa ina maana anao uhakika wa alichokiandika bila error ya aina yoyote. umejibu maswali kwa ufasaha na kutetea hoja zote kwa lugha fasaha na inayoeleweka.
Kumbuka ni uchunguzi wa kina, kwa hiyo katika rufaa yoyote lazima wahusika watoe maamuzi yatakayoonesha umeonewa au haukuonewa. ikiwa umeonewa haki itafanyika.
 
we unategemea nini wanafunzi wanaenda na headphone shule full time ziko maskioni then wewe unakuja kukata rufaa. cha msingi watu wasitake ushindi wa mezani someni mwanzo mwisho ili mfaidike na maksi mtakazopata.
 
Tatizo unao uelewa mdogo kuhusu rufaa. Rufaa haina maana unapokata rufaa inatakiwa ibadilike. Aidha, unapokata rufaa unaonesha kutoridhika na usahihishaji wa awali. hivyo, basi NECTA utafuta wasahihishaji wapya waje wachunguze kwa makini usahihishaji wa awali. Anayekata rufaa ina maana anao uhakika wa alichokiandika bila error ya aina yoyote. umejibu maswali kwa ufasaha na kutetea hoja zote kwa lugha fasaha na inayoeleweka.
Kumbuka ni uchunguzi wa kina, kwa hiyo katika rufaa yoyote lazima wahusika watoe maamuzi yatakayoonesha umeonewa au haukuonewa. ikiwa umeonewa haki itafanyika.

Unajichanganya wewe,umepitia rufaa ya wanafunzi 200 halafu hakuna hata mmoja ambae matokeo yamebadilika.Huoni kuna kasoro hapo?
 
Hapa ni uelewa mdogo unaomsumbua mtoa hoja na baadhi ya wachangiaji. Ukweli ni kuwa mtahiniwa akikata rufaa, hutafutwa wasahihishaji wengine wasahihishe karatasi yake/zake na kutoa maamuzi ya kuonewa kwake au la. Kinachotokea ni kuwa vijana wengi huwa hawakufanya vizuri lakini kwa vile waliwaaminisha wazazi kuwa wao ndo wenyewe, ikitokea wameshindwa mitihani yao hulalama nyumbani kuwa wameonewa na kwamba lazima wakate rufaa!!! Na inapotokea rufaa imeshindwa, huwaaminisha wazazi na jamaa zao kuwa wameonewa. Lakini ukweli sivyo, huwa wamechemsha ile mbaya!!!

Wangeacha kula hela ya watu ya ngama,maisha yanabana.
 
hapa ni uelewa mdogo unaomsumbua mtoa hoja na baadhi ya wachangiaji. Ukweli ni kuwa mtahiniwa akikata rufaa, hutafutwa wasahihishaji wengine wasahihishe karatasi yake/zake na kutoa maamuzi ya kuonewa kwake au la. Kinachotokea ni kuwa vijana wengi huwa hawakufanya vizuri lakini kwa vile waliwaaminisha wazazi kuwa wao ndo wenyewe, ikitokea wameshindwa mitihani yao hulalama nyumbani kuwa wameonewa na kwamba lazima wakate rufaa!!! Na inapotokea rufaa imeshindwa, huwaaminisha wazazi na jamaa zao kuwa wameonewa. Lakini ukweli sivyo, huwa wamechemsha ile mbaya!!!
no, big no mate...
 
Back
Top Bottom