Hizi ni Nusu Fainali Kali Zaidi za UCL

Observer2010

Senior Member
Oct 29, 2010
195
44
Tukiwa tunaelekea ule wakati ambao binafsi nauita ni peak ya michuano ya UCL, napenda kuwakumbusheni nusu fainali kali zaidi ambazo nimewahi kuziona live katika miaka ya karibuni. Hii ni kwa mujibu wangu binafsi nikiwa kama International Observer.

Manchester United vs Juventus Turin 1998/1999


Wakati Juventus Turin ikionekana ndio club bora zaidi kwa wakati huo ikiwa na viungo walio magwiji kabisa katika historia ya soka Zinedine Zidane na Edgar Davids, walikuwa wanapewa nafasi kubwa kusonga fainali na kuwa mabingwa. Game ya kwanza ilianzia Old Trafford, goli la Antonio Conte likatenganisha timu mbili, huku muda ukielekea ukingoni kabisa, Ryan Giggs akasawazisha dakika za majeruhi na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Mechi ya marudiano Italia ilikuwa ni kama ishamalizika, huku timu za Uingereza zikiwa hazijawahi shinda katika ardhi ya Italia kwa miaka zaidi ya arobaini, magoli ya haraka ya Filipo Inzaghi yakawa ni kama yamemaliza mchezo. Roy Keane akafufua matumaini kwa header baada ya kona ya David Beckham, Dwight Yorke anaequalize kwa diving header kabla ya Andy Cole kupiga msumali wa mwisho na kufanya matokeo kuwa 2-3. Wonderful semi final. Man U wanasonga fainali kwa agg ya 4-3.

FC Bayern Munich vs Real Madrid 2000/2001

Real Madrid wakiwa ndio mabingwa watetezi, ilikuwa ni club inayotisha zaidi katika miaka hii. Ikiwa chini ya Vicente Del Bosque, ilikuwa ni club yenye kutandaza soka la hatari. Louis Figo akiwa ndio katoka kusajiriwa tokea Barca kwa rekodi ya dunia, Raul Gonzalez akiwa ndiye anaongoza mashambulizi hakika ilikuwa ni club bora sana. Game ya kwanza ndani ya Santiago Bernabeu, Giovanne Elber anawashangaza maelfu ya mashabiki wa Madrid kwa goli pekee la dakika ya 55. Dunia nzima ikiamini bado Madrid wana nafasi ya kusonga mbele wakikumbuka msimu wa 1999/2000 jinsi Madrid walivyoigaragaza Man U ndani ya Old Trafford. Game ya pili ndani ya Olimpiki Stadium Munich, Elber dakika ya 8 anafungua hesabu, dakika ya 18 Louis Figo anasawazisha na kurudisha matumaini kwa Mabingwa watetezi, dakika ya 34, Jens Jeremies akiwa yard 25, anaunganisha faulo ya Memet Scholl kwa a wonderful strike na kufanya matokeo kuwa hadi mwisho Bayern 2 Madrid 1. Hii hakika ilikuwa ni brilliant semi final.

FC Barcelona vs Chelsea FC 2008/2009

Huku dunia nzima ya wapenda soka ikijaribu kuaminishwa na maneno ya Morinho kuwa Barca inabebwa, CFC wanaenda Camp Nou wakiwa na matumaini ya kufuta makosa ya msimu uliopita ili waingie tena fainali na Man U. Game ya kwanza Camp Nou, Drogba anakosa nafasi za wazi kadhaa, Barca wakionekana wamebanwa na Chelsea, hadi dakika ya 90 matokeo yanakuwa 0-0.
Game ya pili ndani ya Stamford Bridge, Chelsea wanaanza na kasi, goli kali sana toka kwa Michael Essien, left footed long range strike inafanya matokeo yawe 1-0. Dakika 90 zikiwa zimeisha, na za nyongeza zikiwa zinaelekea kuisha, Dani Alves anakimbia kwa kasi wingi ya kulia, anapiga cross golini kwa Chelsea, Captain John Terry anapiga kichwa, mpira unadondoka miguuni mwa Samuel Etoo kwenye line ya upande wa kushoto ya 18 yard box, Etoo anacontrol mpira ila unakuwa km unamshinda unamkuta Michael Essien, anajaribu kuondoa hatari, anauparaza mpira unaenda mguuni mwa Messi, Messi anadrible kidogo na kumpelekea Andres Iniesta, sekunde zinakuwa zimeisha, huku refa akisubiri kumaliza mpira. A wonderful strike toka kwa Andres Iniesta, akiwa just nje ya 18, unafanya matokeo kuwa 1-1, CFC wanaondolewa kwa away goal. Hii ilikuwa ni a fantastic semi final.

Hapa sijazipanga kwa namba wala kwa ubora ila nimezipanga kwa miaka, ila wadau mnakaribishwa kwa maoni. Huu ni mtazamo wangu tukiwa tunaelekea kwenye nusu fainali ya UCL. Natumaini baada ya hapa nitatoa pia tathmini ya fainali 3 kali zaidi ktk UCL nilizowahi kuziona.

Cheerz !!!
 
nusu fainali kali zaidi zilipigwa msimu wa 2002-2003.

real Madrid vs Juventus
Manchester UTD VS AC Milan.

Nusu fainali hizo tulishuhudia 1st legg Madrid wakiwafunga Juve jumla ya magoli 2-1.
Na AC Milan klabu yenye mafanikio zaidi ulimwenguni ikiwacharaza Manchester UTD kwa jumla ya Goli 1-0 ggoli lililowekwa kimiani na mshambuliaji Hernan Creapo.

2nd Legg tulishuhudia Manchester wakipanda ndege mpk ktk mji wa Milan barabara ya Turati ktk uwanja wa Sansiro ambako matokeo yakawa kama ya 1st Legg kwani Manchester wakalala tena kwa goli 1-0 goli lililofungwa na Hernan Crespo.
Haikuishia hapo Madrid nao wakafanya safari mpaka Torino kwa wajukuu wa hayati Bibi Lavecchia Signora na Dunia ikashuhudia Wageni hao wakipokea kipigo kilichopelekea kufukuzwa kwa Kocha na fagio hilo pia likamkumba Nahodha wa klabu hiyo.
Mpaka mwisho wa mchezo Juventus 3-1.
Magoli ya Juve yaliwekwa kimiani na Alexander Peter, David Trezeguet na pavel Nedved.


Fainali ilizikutanisha AC Milan na Juventus.
Naomba break nikatafute Miraa na PK then i promise i'll be back
 
duu jamani Elber alikuwa kunguru kama tegete,lakini sijawahi ona bayern kama ile mlio zaliwa jana pole yenu maana hehehe hatari,angalia mchezaji kama jens jeremies,memet sholl huyu alikuwa anapiga mashuti hakuna mfano,mkuu umemsahau striker janka hatari mrefu..,jamani Roberto Karlosi mpaka raha,Luis Figo,mendieta gaizak.
 
duu jamani Elber alikuwa kunguru kama tegete,lakini sijawahi ona bayern kama ile mlio zaliwa jana pole yenu maana hehehe hatari,angalia mchezaji kama jens jeremies,memet sholl huyu alikuwa anapiga mashuti hakuna mfano,mkuu umemsahau striker janka hatari mrefu..,jamani Roberto Karlosi mpaka raha,Luis Figo,mendieta gaizak,hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha.
 
mmmh kama nausoma ushuzi atakaokuja nao Gang chomba.
Manake ye Milan kwanza, hao wengine watafuata...
Ila kiukweli mwanzoni mwa miaka ya 2000 soka la ulaya ngazi ya vilabu lilikuwa na msisimko sana.
Nyota walikuwa wengi, marefa pia walikuwa marefa kweii kweli.
Naikumbuka Valencia yenye Santiago Canizares, Joselyn Angloma, abedeo carboni, mauricio peregrino na roberto fabian ayala.
Huku Deportivo la Coruna wakiwa na watu kama Song'oo, manuel pablo, capdevila, donato gama da silva, mourdin naybet, mauro silva, djalma feiltosa fotso ''Djalminha''.
Barca walikuwa mdebwedo na timu yao ya akina Oscar Bonano, michael reiziger, sergi barjuan, nadal, abelado.
Madrid walikuwa na cesar, salgado, roberto carlos, airto karanka na Fernando hierro.


Juve walikuwa na Buffon, thuram, gianluca pessoto, mark iuliiano, alesandro bilindelli, paolo montero na nguli cirro ferrara.
Lazio wakawa na Peruzzi, negro, favalli, couto na mihajlovic.
Milan naomba nimwachie mwenye timu yake manake kaaga anakwenda saka mirungi ila kaahidi atarudi.
 
Angloma alikuwa namba 2 ya valencia alimkwatua Patric Kluvert refa mzee Corina alicheka sana,basi akawaambia peaneni mikono wakapeana na mpira ukaendelea.
 
haha jamani wewe shifta na wa-ukenge mnamkumbuka oliver kani na samuel kuffor na Rivaldo?Halafu hata kombe la mataifa ya Africa msisimko haupo kabisa tofauti na zama za akina patrik mboma, pius ndiefi kifupi kama ngasa,sunday oliseah,victor ikpeba,uhondo ulikuwepo.
 
Back
Top Bottom