Hizi ndizo ndege mpya za Jet ambazo zinategemewa kuagizwa hivi karibuni

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Leo katika hotuba ya uzinduzi wa ndege mpya aina ya Bombardier Q400; Rais Magufuli ametamka kuwa Serikali yake ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili mpya za injini ya Jet.

Ndege hizo moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 240. Ndege hizo si nyingine bali ni Airbus A320 na Airbus A330-200. Embu tuzitazame hizo ndege kiundani zaidi:

Airbus A320
Ndege hii ina uwezo wa kubeba kati ya abiria 150 hadi 180 katika mpangilio wa madaraja matatu. Ina uwezo wa kwenda hadi umbali wa 6,500 km kwa kasi ya 871 km/h bila kutua na inatumia injini aina ya CFM56-5 au IAE V2500-A5.

BEI: Bei ya hii ndege ni US $98.0 milioni

Screenshot (11).png


A320_Cabin_IFE_HG_08.jpg


CE-A320_AIB_N.299-15_L_1.jpg


csm_A320neo_PW_Airbus_neo_livery_V10_300caa4fa9.jpg


Airbus A330-200
Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 247 katika mpangilio wa madaraja matatu. Ina uwezo wa kwenda hadi umbali wa 13,450 km kwa kasi ya 913 km/h bila kutua na inatumia injini aina ya PW4000, Rolls-Royce Trent 700 au GE CF6-80E1.

BEI: Bei ya hii ndege ni US$231.5 milioni

Screenshot (10).png

csm_A330-200_GE_AIRBUS_V10_300dpi_963a61aa6d.jpg


Interior-AIRBUS-A330-200-1.jpg
 
Hii nchi ya ajabu Sana.....! Viongozi wa Tanzania wanapenda maendeleo ya Vitu badala ya Maendeleo ya Watu.

Angalia mfano...Dawa Hospitalini hakuna na watu wengi walipata madhara...mpaka watu wamepiga kelele

MSD wanaidai serikali na walipewa pesa pungufu......Sasa maiti ndo zitapanda hizo ndege?

Pili: Kule kagera watu wanataabika....hawajapata msaada.

Harambee iliitishwa na michango ikatolewa mingi...sasa kigugumizi cha kupeleka hiyo misaada ni nini?

Wapeni RED CROSS wapeleke hiyo misaada chap.....

Wafanyakazi serikalini wamepoteza morali, mishahara kiduchu

Mfumuko wa bei upo juu
 
Hiyo Bombadier CS300 maelezo yake yako wapi ? Naona umetaja ndege mbili tofauti ila maelezo ninayoyaona ni ya Airbus pekee

Mkuu Bombardier CS300 haitatufaa kwa sababu yenyewe ina uwezo wa kubeba abiria kati ya 100 hadi 150 na si zaidi ya hapo.
 
Tutakula nyasi !!! maana kupanga ni kuchagua kama kweli hela zote hizo zikipelekwa huko mambo mengi yatadolola
 
Back
Top Bottom