Hizi ndizo kura alizopata Mhe. Regia Mtema alipogombea Ubunge Morogoro 2010

kwa kweli ninapata utata sana ninapotafakari mazingira ya ajali ya dada regia..... A. Kipande cha barabara kablaya ruvu darajani kimenyooka sana na hasa kama unatokea dsm unaona magari hata yaliyo mbali kwani uko mlimani....ilikuwaje aovateki ilihali kuna gari linakuja? kwa wanaosoma maandiko na kuyatafakari katikati ya mistari.... gari lilibingirika mara 7 na kumwacha ubongo wazi... Rejea logic ya kiimani iliyo katika namba 3 na 7 mazingira baada ya ajali eti alifariki dunia peke yake? kesi yake ya kupinga ubunge ilikuwa pazuri na pengine kumweka pabaya mbunge wa sasa kwani pamoja na mengi alimkashifu majukwaani kuwa ni kiwete hataweza kuongoza! Upon udhibitisho wa hili jamaa angejifutia milele kibali cha kugombea..... Tumeona ya shelembi, halafu sasa regia.....
umesema
 
Jamani, sitaki kuhusisha uchawi na msiba wa dada huyu ila naomba nielezee kidogo mazingira wanayoishi na imani za wanasiasa wetu.

Siasa za TZ kwa asilimia kubwa zinaongoza kwa uchawi, kisha rushwa ndiyo inafuata. Kabla mtu hajagombea anaenda kwa waganga, wanalala huko, wanalala uchi, wanawanga wanaambiwa wamepewa kinga na ushindi. Mpinzani wake akijua kaedna Handeni Tanga yeye anaenda Sumbawanga. Basi ni full kulogana.

Hii yote inatokana na kutokujiamini - kiimani na kiuwezo. Mtu hana mbele wala nyuma ataupataje ubunge asipologa na kutumia hela kuhonga? Mtu wa kijiweni kwa mfano. Na hapa tusiseme CCM, ni vyama vyote!

Ukijua siri zao utashangaa. Hawasafiri mpaka waulize mashetani, hawali mpaka waulize mashetani, hawaendi vikao vizito mpaka waulize mashetani.

Hawa ni wasomi na tunategemea watuletee maendeleo majomboni mwetu. Maendeleo ya mashetani? Au maendeleo gani, ya damu na kafara?

Unaamini uchawi?
 
Mwalimu kumbuka sisi ni waafrika !
Uchawi ni IMANI tu kama zilivyo imani za DINI. Wanaomini DINI wanaamini na UCHAWI upo. Kwao kila tukio, janga, maafa, magonjwa, kifo,..., kuna mkono wa mtu! Neema za Ubunge zimechangia kifo cha mpendwa wetu Regia.
 
Uchawi ni IMANI tu kama zilivyo imani za DINI. Wanaomini DINI wanaamini na UCHAWI upo. Kwao kila tukio, janga, maafa, magonjwa, kifo,..., kuna mkono wa mtu! Neema za Ubunge zimechangia kifo cha mpendwa wetu Regia.

Kila aaminie dini lazima aamini na uchawi pia?

Neema zimechangiaje?
 
Lazima mkubali kadari za Mola.
Kama aliweza kumuumba atashindwaje kumchukua. Tunaamini kila kilichoumbwa basi lazima kitakufa.
Na yeye ametangulia sisi tupo nyuma yake. Ni vizuri kumuombea kwa Mola amlaze pahala panapostahikhi na sio kutafutana uchawi.

 
Kila aaminie dini lazima aamini na uchawi pia?

Neema zimechangiaje?
DINI zote mpinzani wake mkuu ni uchawi na uganga wa kienyeji. Neema zimechangia kwa kuwa ka-mkoko haka kalikommaliza alikavuta kwa kutumia ule mkopo usio na riba aloopewa na BUNGE letu tukufu.
 
Wandugu, huu ni wakati wa kulia, kuomboleza na kumwombea dua mpendwa wetu Regia (Mungu Ampe Malazi Mema), na wala sio wakati wa kutafuta mchawi. Imeandikwa katika vitabu kuwa kila nafsi itaonja mauti. Mungu ndie Muumbaji, Mungu ndie muondosahji. Hakuna pameandikwa kuwa baada ya kuumba Mungu kaweka mawakala wa kumsaida kazi ya kuondoa watu kwenye uso wa dunia.

Tuwe na tahadahri na maoni yetu mengine. Badala ya kuwafariji wafiwa tunawaongezea machungu ya kuondokewa na mtoto wao. Tujirejeshe katika nafasi yetu ya ma Great Thinkers na sio ma Great Pumba.
 
MOROGORO
WILAYA YA KILOMBERO
KILOMBERO
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
MTEKETA RAJABU ABDUL
CCM
43,459 48.86
MTEMA REGIA ESTELATUS
CHADEMA
38,550 43.34
ZAINABU IBRAHIMU HIMILI
CUF
4,469 5.02
ABDU ALLY MNOLA
UPDP
299 0.34
SPOILT VOTES2,165 2.43
TOTALS 88,942 100

Takwimu hizi ni za oungo wa mchana. Maafisa wa UWT waliomnyang'anya ushindi ndiyo nafsi zinawasuta ndiyo maana wameona wazitoe ili kudanganya waTz. Shame on you UWT mnaoangamiza taifa la Tz. Lakini mjue siku yenu iko jikoni mbinguni na adhabu yenu. Siwapendi hawa jamaa!!!!!
 
MOROGORO
WILAYA YA KILOMBERO
KILOMBERO
Candidate
Political Party
Number of Votes
Percentage Votes
MTEKETA RAJABU ABDUL
CCM
43,459 48.86
MTEMA REGIA ESTELATUS
CHADEMA
38,550 43.34
ZAINABU IBRAHIMU HIMILI
CUF
4,469 5.02
ABDU ALLY MNOLA
UPDP
299 0.34
SPOILT VOTES2,165 2.43
TOTALS 88,942 100

MwanaJF Jiwe la Ukwara hebu twambie dhamiri ya kutoa tkwimu hizi ili tueeweje?; maana huyu mama si ndiye yule ambaye hawa jama wabaya UWT walimnyang'anya ushindi baada ya kupewa certificate? Hebu tuwekw sawa hapa!!!!!
 
Kwa haya matokeo 2015 chadema wakipata mgombea type ya Regia,lazima watalichukua hili jimbo
 
Huyo anaitwa PAPA MTEKETA mtoto wa Lipangalala mjini Ifakara..AWIJE BAMBOO

Hizi kura ni za UWT kujaribu kusoma upepo!!!!!!!!!!!!!!! Lakini Mungu yupo. Takwimu hizi ni uongo wa mchana; hazina ukweli wowote. Huyu marehemu alinyang'anywa ushindi mchana kweupe!!!!!!!!!!!! Waliofanya maovu haya nawaasa wasiende kwenye msiba huu Ifaka au la mizimu ya Regia italipa kisasi kwao na familia zao wote!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hizi ni kura za ushindi kwa vigezo vifuatavyo
1.mgombea mwanamke
2.mgombea mlemavu
3.mwanasiasa mchanga
4.mwanasiasa wa upinzani
 
na yeye aliyesebabisha ivi tuone aishi milele, au japo miaka 100 tu afaidi! na kama ni kweli jamaa wamemsababishia ajali, basi Mungu awape laana mwaka huu wote. hawa wazee wazee ndo wanaongoza kwa uchawi hapa Tanzania, hivi vijana sa ivi tunakuja juu katika kila nyanja sio siasa peke yake, basi watatumaliza!. Mi sielewi hapa nilipopata kazi alikuwepo mzee, ila baada ya mimi kuanza kazi basi kaondoka hata hakuaga wala kukabidhi ofisi!
 
Wandugu, huu ni wakati wa kulia, kuomboleza na kumwombea dua mpendwa wetu Regia (Mungu Ampe Malazi Mema), na wala sio wakati wa kutafuta mchawi. Imeandikwa katika vitabu kuwa kila nafsi itaonja mauti. Mungu ndie Muumbaji, Mungu ndie muondosahji. Hakuna pameandikwa kuwa baada ya kuumba Mungu kaweka mawakala wa kumsaida kazi ya kuondoa watu kwenye uso wa dunia.

Tuwe na tahadahri na maoni yetu mengine. Badala ya kuwafariji wafiwa tunawaongezea machungu ya kuondokewa na mtoto wao. Tujirejeshe katika nafasi yetu ya ma Great Thinkers na sio ma Great Pumba.

Avator yako imefanana na comment
 
Ndg wadau wa JF, wakati nyie mnajadil uchawi na iman nyngne. Mi hapa nawaza na kuwazua, Je rafiki yangu kpenzi Regia amepokelewa wapi? Je yuko jehanum or paradiso? Hk n kitendawl knanisumbuaga mara nyng, hasa napotokea kupotelewa na watu wa karibu na mashuhur km regia wangu! Itakua ni furaha iliyojee km Regia atakua yupo kifuan mwa Baba, paradiso akfutwa machoz mara bada ya tabu za kuwapgania waTz, lakn upande wa pil ni majuto na simanz endapo atakua yupo jehanam. Lait km 2ngekua na access ya kupaona hapo alpo kwa sasa! 2ngejua aidha 2endelee kulia au nas 2taman kwenda huko aliko. Ndg zangu kwa kifo hk cha ghafla hua knanfanya niwaze, je! ingekua ni mim hapa sa hv nngekua wapi? Na kumbka no point or chanc 2 turn back! Regia ma frnd ulikuwa safi kupokelewa huko paradiso? Ulikidh vigezo? Ndg zangu 2rudi nyuma 2jiweke tayar, coz bada ya rafki ye2 zamu ni yangu mim hapa au wewe unayesoma comment hii! 2kumbuke kua 2natembea tayar 2kiwa ni marehemu! Tujiweke SAFI na 2we tayar in any time and at any point!
Bwana alitoa na BWANA ametwaa jina lake Libarikiwe!
 
Back
Top Bottom