Hizi kero maofisini usiombe

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,105
2,499
1. Upo rum mmoja na mwenzio, anaweka AC juu kupita uwezo wa mwili wako kuhimili ile baridi kali.
2. Upo rum mmoja ofisini, mwenzio wageni ni vidosho tu kwa kwenda mbele.

3. Ile unafika asbh ofisini, mood ya kuwepo ofisini haipo unatamani utoke ukazurure kidogo ndo urudi ofisini.

4. Mtu anakupa kazi ambayo siyo ya kwako, ukiharibu hiyo kazi imekula kwako

5. Mengineyo ntaongezea.......
 
Ajira Mpya nini Kaka? Huyo mwenzio ni kabila gani? yapo makabila kama wahaya wanafanya ofisi kama nyumbani kwao, kila kitu anataka kumiliki yeye, yeye ndo aonekane, ana maamuzi utadhani yupo peke yake nk. samahani baadhi ya ndiugu zangu wa Kanyigo, Kanazi, Katerero, Kachabalo...your behaviours sometime zina bore wengine!.
 
Umesahau majungu mkuu! Watu wanafanya ofisini ndo mahali pa kusearch identity zao,rubish kabisa! Anataka kila mtu arecognise uwepo wake.inakera sana.
 
1. Unafika ofisini hujakaa vizuri mara, "Kaka Mentor nikiuwekee chai?"
2. Mara ghafla HR anapita on her way to her office, mkononi kashika kibahasha cha kaki kimelowa mafuta, "Leo nimeona nikununulie kachapati kamoja Mentor, umeamkaje?"
3. Bosi naye kapita mida ya sa tatu kama kawaida yake akashout kuanzia mwanzo wa corridor, "Habari zenu bhanaaa??" nasi bila hiyana tukamjibu, "Haina majotrooooooo"

Yani hizi kero ofisini kwangu sijui nifanyeje...
 
Watu ndo hupata mahali pa kujiachia,si unajua home muda/mazingira ya kufanya vurugu hamna.
 
Watu ndo hupata mahali pa kujiachia,si unajua home muda/mazingira ya kufanya vurugu hamna.
So, yale mazoea ya kuonesha maukorofi wa primary na secondary ndo huyaleta maofisini!!? Dah kazi kweli kweli...!
 
Hii sredi nimeipenda sana. Kero zangu:
1. Uko bize na kazi mtu anakuja kukaa kwenye kiti mbele yako anatia storii hazina kichwa wala mguu
2. Una share office na mtu/watu anaongea kwa simu kwa sauti kubwa utadhani anahutubia mkutano wa hadhara
3. Office mate wajo kila baada ya dk anakuuliza swali ambalo halina msingi
4. Hasa wanawake, anakueleza story za mume, watoto, mpaka jana yake mtoto wake alivyotapika kabichi nzima nzima na mumewe alivyo na allergy ya dagaa
Aaaarggghhhh
 
kha! hivi maofisini kwenu kukoje??
mimi sasa hivi nimekerwa na huyu mdada tunayefanya naye kazi hapa ati, "Mentor, leo nataka nkutoe lunch..."
 
Na wewe kwani kukutoa Lunch ni tatizo?

Yani ndo kero zangu hizi za kila siku...yani ninaweza kukaa wiki nzima sijatumia pesa yangu..mara ooh, Mentor hivi mentor vile....mpaka sometimes inabidi nilazimishe kuwanunulia wao!
Ni kero zinazofurahisha..ndo maana nashangaa za wenzangu ni kero ova kero!
 
uuuuhhuhuuhuhuhuhu miiii hoiii jamani na hawa mate zangu. wao kutwa wanazoza kikwao tu kelele kibaaaaao. yani mh.
 
1. Upo rum mmoja na mwenzio, anaweka AC juu kupita uwezo wa mwili wako kuhimili ile baridi kali.
2. Upo rum mmoja ofisini, mwenzio wageni ni vidosho tu kwa kwenda mbele.

3. Ile unafika asbh ofisini, mood ya kuwepo ofisini haipo unatamani utoke ukazurure kidogo ndo urudi ofisini.

4. Mtu anakupa kazi ambayo siyo ya kwako, ukiharibu hiyo kazi imekula kwako

5. Mengineyo ntaongezea.......

Duu sijui umefikiria nn leo? kero zipo za aina mbalimbali mwingine
anaweza kukuta unakula nae akaanza kudokoa chakula chako
katika sahani huku akikusemesha kero tupu.
 
hizo zote sio kero

kero ni hizi..

1.ofisi inajua wewe ni addicts wa internet unakuta ki memo
kuanzia leo marufuku kuingia mitandao mingine isiyo ya kiofisi....

2.net kwako iko slow,unamuita administrator anakudengulia..
kisa anatembea na bosi wa head office

3.unaingia ofisini unakuta kuna ma trainee wanawake wapya
walivyovaa utasema wanatangaza biashara

4.unafika ofisini,unakuta kuna mabadiliko,
umekewa pc nyingine ya zamani na software za zamani...
unauliza unaambiwa ile nyingine inafanyiwa service
ikirudi wamefuta kila kitu...

5.kuna mgao wa umeme na ofisi haina bajeti ya genereta

6.kuna mgao wa umeme na genereta la ofisi lipo dirishani kwako
 
  • Maji kazini hayatoki na hamna akiba hali uko porini.
  • Boss kukulazimu mtoke lunch alafu kutaka muende stage inayofuata.
  • kufanya ofisi haina sare ya kazi - presha tupu kuhusu mavazi!
  • Kuomba assistance kwa mfanyakazi mwenzio ambae hujifanya yuko busy kweli kumbe yuko jf.
 
Back
Top Bottom