Hizi kazi za wito

LISAH

Senior Member
Jan 28, 2012
108
24
Hivi imekaaje kazi moja ikaitwa ya wito na nyingine si ya wito wakati watu wote wanafanya kazi kwasababu wanataka kuweka mkono kinywani na kuishi maisha bora?
 
Na hizi kazi za wito watu wanachaguliwa au wanajitolea kwenda huko?
 
Na je wanasomeshwa na serikali bure?
Ukizingatia cost sharing!
 
Hamna cha wito wala nini hapo wanataka tu kuendeleza nidhamu ya uoga kwa watu na kuwapotezea malengo ya kudai haki zao za msingi kwa kusngizia wito. Kama serikali inajua habari za Wito kwa nini wasiuheshimu huo wito wao?
 
hata wachungaji wanakula kile kinachopatikana madhabahuni, sembuse mi ambaye ni secular,labda wapewe universal smart card hata marekani unapeta
 
hakuna kazi ya wito kwani kama aingekuwa ni wito wasingekimbila/kuingiza suala la kodi kwa kile kidogo kinachopatikana kwa huo witowa mazingira magumu ya kazi..
 
Hamna cha wito wala nini hapo wanataka tu kuendeleza nidhamu ya uoga kwa watu na kuwapotezea malengo ya kudai haki zao za msingi kwa kusngizia wito. Kama serikali inajua habari za Wito kwa nini wasiuheshimu huo wito wao?

Mie najiuliza huo wito wanaambukizwa vipi?
 
Hamna cha wito wala nini hapo wanataka tu kuendeleza nidhamu ya uoga kwa watu na kuwapotezea malengo ya kudai haki zao za msingi kwa kusngizia wito. Kama serikali inajua habari za Wito kwa nini wasiuheshimu huo wito wao?

Umenena mkuu... Kwanini wasiuheshimu basi huo wito? Yaani kwa kuwa imepewa jina (sijui lini na wapi),kuwa ni kazi ya wito,ndiyo huo wito umwelemee mfanyakazi?

Yaani kuwafanya wajute kwa kozi walizochukua?

Lazima tukubali kuwa si kila mtu anaweza kuwa Daktari jamani.. Ila si shida kwa Daktari kama akiamua,akahamia Msc ya Uhasibu,na fani nyingine yeyote..
Kuna watu wanaongea kwa kuwa hawaijui kazi yenyewe..

Kukutana madonda makubwa ya kutisha na mengine yana harufu mbaya..
Kufanya oparesheni ambazo wakati mwingine unalazimika kusimama muda mrefu hata saa 8 mfululizo!
Na mambo mengine mengi ya ajabuajabu...

Halafu mtu wa aina hiyo alaumiwe kwa kutokuwa na wito..
 
Kwa mazingira ya kazi za madrc na manesi nadhani ingekuwa vyema sana wangekuwa na mishahara minono na marupurupu ya kuvutia mtu kufanya kazi huko.
Pia marupurupu yaliyoshiba ya kufanya kazi katika mazingira magumu.

Serikali iangalie madai ya hawa watu, kwani ni muhimu sana kwa wananchi. Kazi zingine zaweza simama lakini si hii huduma ni hatari tuache siasa!
 
Huwezi ukasomea kazi alafu ikawa wito. Ukishasomea hiyo ni taaluma. Mimi nadhani wito ni kuitwa kufanya kazi ambayo hukuwai kufikiria kufanya.
 
Na huitaji ujira kwani huo ni wito.
So unaweza ukawa na kazinya kukufanyab uishi na nyingine ya kujitolea uliyoitwa kuifanya hasa na mungu
 
Back
Top Bottom