hizi kazi za magazeti na internet huwa wanaita watu kwenye interview

Dec 4, 2011
13
3
wakubwa habari zenu! jamani hivi hizi kazi za kwenye magazeti huwa wanaita watu kwenye interview au hata kuwapatia watu kazi? mwenzenu mie ni graduate yani nimetuma barua za kazi zisizopungu 70, ila sijawahi itwa, hapa nilipo nimejikatia tamaa, au kama kuna sehemu nakosea naomba msaada wenu
 
Huwa wanaita, mimi nishaitwa mara mbili kazi za kwenye internet, na saizi ninapofanya kazi niliona tangazo online.
 
Mimi nasema ni bora ukatumia hizi za online. mwenzako nilipata kazi kwa kutumia internet na sasa nachapa mzigo.
 
Kwa waajiri naomba wawe wanatoa timelines kidogo zaidi ili waombaji wajue kama wamo au hawamo kwene mchakato. Kutoa deadline ya kupokea maombi nadhani haitoshi. Mlitakiwa mseme waombaji wasipoitwa hadi tarehe flani wajue kuwa hawakuwa succesful, ndio uungwana maana kumuacha mtu ana-hang tu bila kujua si kitu kizuri.
 
we jifunze kuandika cv...na apply kazi relevant na qualification zako.sio umesoma upishi unataka kuwa programme manager kama sisi
 
wakubwa habari zenu! jamani hivi hizi kazi za kwenye magazeti huwa wanaita watu kwenye interview au hata kuwapatia watu kazi? mwenzenu mie ni graduate yani nimetuma barua za kazi zisizopungu 70, ila sijawahi itwa, hapa nilipo nimejikatia tamaa, au kama kuna sehemu nakosea naomba msaada wenu

Mkuu usikate tamaa kabisa, huwa wanaita na watu wanapata kazi. Wewe endelea tu kutuma barua za maombi kila unapoona nafasi za kazi.
 
Zinapatikana sana tu, tena bila refa. Confidence is everything. Watu hawaandiki cv wala applications na hata wakiitwa kwenye interview mawazo yote yapo kwenye kutafuta mapandikizi/mamluki. Hata kama huna refa, Mungu ndo refa wa wote. Jivikeni ujasiri vijana, mjiandae vema na kazi zinapatikana however long it takes!
 
Na mimi namaliza mwaka sasa napiga mzigo kupitia kazi za kwenye internet. angalau hizi huwa hazina kujuana!
 
wapendwa nawashukuru kwa mawazo yenu, hizo za online wengi tunatumia zoom, kama kuna nyingine hebu turushieni ndugu zenu
 
du wakuu mbona naona humu kama watu wanatambiana ohoo mimi nilipata hivi ohoo cv yako imefanyaje sijui, bwana mdogo tuma tu maombi mengi usikate tamaa wakati mwingine na bahati inachukua nafasi yake omba na mungu akusaidie pia usikate tamaa
 
Mkisema kazi za kwenye internet mnamaanisha nini? hizo hizo za kwenye internet si ndio hizo wanazoadvertise na kwenye magazeti au?
 
mmh inabidi nimtafuta mwajiriwa m1 anipe hints za kuandika hizo ma cv na vitu kama hizo mana na mie najiona kama ninagundu mana siitwi popote na nimeaply sehem kibao
 
Back
Top Bottom