Elections 2010 Hizi gharama zisizo la lazima za uchaguzi atazilipa nani?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Kwa mara ya kwanza serikali ya chama tawala imetikiswa na vyama vya upinza, hasa hasa Dr Slaa.
Katika hali ya kutatanisha kumekuwepo na ucheleweshwaji wa hali ya juu katika majimbo ambayo CCM walikuwa hawakubaliki, kuna tetesi pia kulikwa na nguvu za dola kulazimisha matokeo ya Mwanza mjini, vile vile kuna tetesi ambazo zilizagaa jana mjini Shinyanga kuwa Rais Kikwete alifika hapo akitokea Mwanza, masaa machache baadaye kulitokea vurugu ambazo zimeghalimu rasilimali nyingi katika kuhakikisha amani na askari wengi kuendelea kuweka doria (ninaamini wanalipwa kifuta jasho kwa kazi hii ya hatari).
Kuna wasimamizi na wasaidizi wa uchaguzi wengi pia ambao wanaendelea kujumulisha kura zilizopigwa masaa takribani 80 tangu uchaguzi upigwe, hawa pia naamini wanalipwa kwa kufanya hivyo.
Swali langu, kwa nini tume hawakufanya maandalizi stahiki ya teknolojia hii mpya. Na pale ambapo wanasiasa wameingilia zoezi zima la uhesabuji wa kura, je wanadhani hii ndiyo kazi waliyotuomba kututumikia?
Kama kweli JK na watu wake walijaribu kubadilisha matokeo jambo lililosababisha uvunjifu wa amani na uharibifu basi ameshindwa kabla ya matokeo kutangazwa, hata kama tume watampa ridhaa ya kuwa Rais, ajue amejivunjia heshima na ameidhalilisha nchi yetu.
 
Back
Top Bottom