Hivi zama za ukweli na uwazi ni za Mkapa au Kikwete?

Revolutionary

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
456
86
Baada ya Kukumbuka na kupitia utendaji wa serikali ya awamu ya tatu ya Mjomba Ben Mkapa pamoja na bashasha za sera na slogan yake ya ZAMA ZA UKWELI NA UWAZI! na pia nakumbuka alilivalia njuga hili la uwajibikaji/Accountability na Anticorruption.

Lakini ukiangalia ni kipindi cha Mkapa ndicho ambacho ufisadi uliota mizizi, haswa wakati unafanyika ubinafsishaji wa mashirika ya uma, nyumba za serikali. Viongozi watendaji na wanasiasa (mawaziri) wa serikali ambao walikua ndio watekeleza sera ya ubinafsishaji walijibinafsishia wenyewe mashirika pamoja na kujiuzia nyumba za serikali tena kwa bei waliojipangia wenyewe.

Hatimaye viongozi hawa wakawa wanaenjoy benefit pande zote, nyumba walizojiuzia na zile za serikali ambazo walizipangisha na kujipatia kipato huku gharama za ukarabati zikifanywa na kodi zetu (serikali). Nyumba hizi walizitumia pia kama collateral ya kupata mikopo mabenki ili kuendeshea biashara zao kwa kuwa zilikua kaitka maeneo nyeti [mnayajua] tofauti na wananchi wa kawaida ambao hata kumiliki kiwanja ilikua ngumu.

Kuingia kwa viongozi hawa wa serikali na wanasiasa na wanafamilia zao kukafanya wao wamiliki biashara karibu zote nyeti hapa nchini, iwe ni mafuta, usafiri nk. Hii imepelekea conflict of interest, leo hii hata wananchi tulalamike vipi kuongezeka bei za mafuta, serikali inajiumauma tu kwa kuwa hawawezi kushusha bei kwani watapata hasara katika biashara zao, kwa hiyo wanaendelea kutukamua.

Toka kipindi hicho viongozo wa watendaji na wanasiasa wa serikali walijirimbikizia mali na biashara, maskini wakaendelea kuwa maskini na matajiri [wenye tabasamu za kifisadi] ni matajiri hadi leo.

Ukiachilia mbali mafanikio ya serikali ya Babu Mkapa, yaliyosifika na IMF na World Bank. Ufisadi uliofanyika kipindi hicho ndio hadi leo hii unaendelea. Lile gamba linalogoma kuvuka sasa lilipata ukomavu kipindi hicho. Sasa nadhani ile 'Zama za ukweli na uwazi' haikua kweli, kwani ufisadi wote wa enzi za Mkapa ulifanyika kwa kulindana na kwa kubadilishana vijiti.

Enzi za JK ndio mambo hadharani na hiyo ni kwa kulazimika au kwa kujikuta tu inakua hivyo, na nadhani baada ya wananchi kujanjaruka sasa ukitoke tu ufisadi inajulikana, Nadhani zama za JK ndio zama za ukweli na uwazi sio zama za Mkapa. Kweli ni haki ya CCM kupoteza uelekeo.
 
Zama za JK NI ZAMA ZA 'KULIPUANA' FULL MABOMU..we lipua tu kila aina ya mabomu..
 
Back
Top Bottom