Hivi yule 'Babu wa Loliondo' bado anatibia?

Tatizo watanzania wazuri wa kushabikia mambo ya hovyo tukishapigika ndio tunaanza kulaumu serikali....sijui huu ujinga utatuishia lini?
 
Kuna jamaa anatumia ARV s,yeye hataki kabisa hiyo dawa ya babu kwa sababu ameambiwa dawa nyingi za kienyeji zinaharibu mfumo mzima CD4,hivyo ukipima unaweza kudai umeanza kupona.Na hii ndio imeponza wangu wengi.
 
Guys, I have a different problem. Ninataka kuangalia TBC1 kupitia mtandao kwenye computer yangu. Nilipata hii link lakini niiweka kwenye VCL player ya computer yangu inaniuliza username na password: rtsp://196.28.65.226/diactus/movie.3gp?weUE9Qdy3GHWo2-5Tpic3b47H(i8afKugOTAdmjZcV1ljArP1641PQ7ee3h-yN20%20%0A. ​Ninaomba msaada.
 
Babu wa Samunge bado anapiga kazi bila kupumzika!
Shida Watu wanataka waone maandishi na Picha kwenye magazeti ndio wajue kinachoendelea Samunge!
Tuulizeni tunaojihusisha na mambo ya huko tuwajuze yanayojiri!
Kwa report yenu ni kwamba SASA HIVI NDIO WATU WENYE PESA YAO WANAENDA KWA BABU, na wanahudumiwa bila bugza!
Foleni bado zipo, japo anamanage kuhudumia wote!
Watu wasikurupuke kuongea wasichokijua!
JWTZ ndio kwanza wanaweka kituo chao hapo ili kuhakikisha usalama, na bado mambumbumbu wengine wanategemea huduma zimepungua!...Shiiit!

crap! ....
 
Ivumayo haidumu

Yupo memba amesema hapo awali ... kwamba waandishi wamehamia ktk maswala mengine ndio maana babu hayuko kwenye "headlines" tena.
Lakini ukweli ni kwamba bado watu wanamiminika huko kila kukicha. On the average kuna kama magari 200 to 300. Most of the people are from Kenya, Uganda Rwanda na Wa TZ wachache.

So Babu bado anatesa.
 
desperate Tanzanian!! katika hali ya kawaida ni ajabu kuamini tiba isiyo na uchunguzi wowote wa kisayansi..si kwamba nadharau tiba asilia zilizopo lakin ukweli ni kwamba kikombe cha babau ni kama alkadabra!! yaani kitu cha kufikirika wengi waliotumia hasa wagonjwa wa ukimwi wanasema hakuna badiliko hivyo bado si sahihi kuamini tiba hii. Na serikali yetu ilibariki kwasababu kilikuwa kipindi kigumu cha mambo ya ufisadi na richmond ikakaa kimya na wabunge na mawaziri wakamiminika kupata tiba,baada ya hali kutulia waziri wa afya akasema hakuna uthibitisho wa kitaalamu kuhusu tiba ya kikombe! ni danganya toto tuamke change we need wake up!
 
Kwei kabisa.Tz imekuwa nchi ya kuishi na kuhamishwa kwa matukio,ufisadi (ambao hauishi),chakachua,kikombe cha babu,symbion,umeme,mafuta,uda nk nk,labda itajirudia tena.
 
Yupo memba amesema hapo awali ... kwamba waandishi wamehamia ktk maswala mengine ndio maana babu hayuko kwenye "headlines" tena.
Lakini ukweli ni kwamba bado watu wanamiminika huko kila kukicha. On the average kuna kama magari 200 to 300. Most of the people are from Kenya, Uganda Rwanda na Wa TZ wachache.

So Babu bado anatesa.
Kwa hiyo mkuu unashauri watu waendelee kumiminika huko na waache tiba zao.Mbona watu hawaponi na kutupa ushuhuda?
 
hv wandugu yule babu wa kikombe cha loliondo ameishia wap?mbona habar zake hazivumi sana kama awal!
 
yupo na mambo yake yanaenflea kama kawa. na watu wanapona vilevile. wakati nyie mnamponda, wakenya wanamfaidi kwa kumtangaza na kumfanyia biashara kwa kwenda mbele. ukifika waso magari ya kenya ni tisini asilimia.
 
Wakati WATANZANIA wanagwaya WAKENYA wanasema ''Naaam Babu'' uko wapi? Na kuna tetesi ya kwmb wamemweka kwny mtandao ya kwmb yuko nchi kwao na yupo kusini mwa Jiji la Nairobi. Yani Nchi ye2 imeshakuwa ya kwao. Mmmmhh!!
 
Back
Top Bottom