mzanganyika
JF-Expert Member
- Sep 3, 2009
- 257
- 6
Kwa hiyo sasa wazungu wanaamini kwamba hiyo nadharia yake haikuwa sahihi?
Ninavyoona mimi kutokana na interaction zangu na wazungu na matukio mbalimbali ni kwamba hawana doubt juu ya ukweli kwamba intellect haitofautiani capacity kwutokana na asili ya mtu, yaani mzungu ama mwafrika.
Lakini naomba nikuwambie jambo moja.
Ninaamini kwa kwa kiwango kikubwa kwamba sisi waafrika hatuna 'sense of responsibility' na wazungu pia wanatambua hilo. Kutojali majukumu ndio kumetuweka nyuma. Ukiangalia hata mabaraza yetu ya mawaziri, wapo wengi waliofika shule lakini hakuna utendaji kwa kuwa tuna tatizo la kutowajibika na kutowajibishana.
Omari Mahita alijaribu kukwepa jukumu la kumwangalia mtoto wake mwenyewe, sasa unadhani huyo akiwa kiongozi atakujali wewe wakati mwanawe mwenyewe hakumjali?