Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Kupigwa kwa kura za maoni zanzibar juu ya kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa kwa kiasi kikubwa ni jambo lililoleta faraja kwa wananchi wengi wa visiwa hivyo. Na huenda ikawa ni tiba ya matatizo yaliyokuwa yakitokea huko kwenye mfumo wa uongozi. Mabadiriko ya katiba ni wazi yatafungua njia kuelekea katika utulivu zaidi.
Swali langu, ni je kwa nini na sisi watanganyika tusidai kupigwa kura ya maoni juu ya kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa Tanganyika? Kwa mtazamo wangu hii serikali ya CCM kwa kiasi kikubwa imekuwa ikifanya kazi kwa kusinzia na huenda inatokana na viongozi wake wana-CCM kuijisahau na kuona kuwa ni wao tu wenye uwezo wa kufanya kazi ya kiuongozi.
Tumeona ni jinsi gani mawaziri wa kikwete walivyovuruga mambo na bila kuchukuliwa hatua yoyote. Mifano michache ni Uvujaji uliokithiri wa mitihani kuanzia shule za msingi mpaka sekondari na waziri yupo tu anadunda,Matukio ya wananchi kupoteza maisha kwa kukosa maamuzi na utendaji thabiti wa wizara husika mfano wanafunzi waliokufa maji mto rufiji, wanafunzi waliokufa maji ziwa victoria.
Ujambazi wa kutumia silaha uliokithir utadhani nchi haina serikali. Napendekeza tuwe na kura ya maoni ambapo pia serikali itakayoongoza nchi uwe na wawakilishi kutoka vyama pinzani ili kuondoa uzembe wa wazi unaondelea.