hivi wanaume mbona mna mioyo migumu hivyo

Hapa ndipo ule uzi wa Rutashubanyuma wa UTII unahusika. Na waje sasa watuambie kama wanachotaka ni Utii au Uchi? Huyu mwanamke kamtii mumewe hadi kufikia kuacha kazi, leo hii ametendwa. dah! Kweli kisicho riziki hakiliki
 
Last edited by a moderator:
huyo mwanamke hakumjua huyo mwanaume mapema? Mwanaume akikushawishi uache chuo au kazi ujue hafai, kimbia.....
 
Akome kuach kaz na chuo!eti litokee lijanaume linaniambia niache kaz,ntachukua mtwangio wa kinu nimpige nao kchwan!
 
akome ujinga wake mwenyewe!
hivi ninyi wanawake wengine mna akili au matope kichwani, maana ningesema mna colgate ingekuwa afadhali. wewe wazazi wamehangaika na wewe mpaka ukafika chuo, halafu linakuja li mwanaume na kukushawishi uache likuoe, na wewe unakubali, halafu yakitokea hayo unalalamika!! shame on you, big shame.
Mi ni mwanaume, lakini ningekuwa na mwanamke wa type hiyo hata sitaki kufikiria ningekufanya nini maana badala ya kutumia akili kufikiria we unatumia kidudu chako, in the name of love,,, haaaaaa! na siajabu aliolewa bila hata kuhusisha wazazi,
akome kabisa

Ok umesema meeengi mwisho wa siku hujajibu swali la mtoa mada
Kwa nini mtu anakosa huruma hata kwa wototo aliozaa mwenyewe
Kama mama Kilaza hiyo mpango wake watoto je?
 
inakuwaje mwanaume huwapendi watoto wako wa damu yako mke waweza mchukia lakini hadi watoto nimesikiliza hekaheka huyo baba alivyokua ana pesa lakini anamuachia mke wake sh 2000 ,wakati mwingine haachi hela kabsa,watoto wamelala anapuliza dawa ya kunguni kweli huo ubinadamu ukizingatia amemuachisha mkewe chuo na kazi hataki afanye bado anamnyanyasa anampiga na kumdhalilisha mbele ya wanae jamani inauma sana

Hii ni nini?
Imetoa wapi?
Imekuaje??

Walitudharau hahahaaaa who z laughing now? Exponential potential hahahaaaaa,Kaukimbilia muhogo mwenyewe wacha aione gondoigwa.
 
most of them

Dada wapo wengi wanaojali watoto wao ila usijibebeshe mimba bila sababu, maana wako wanawake wengine kabla hajaolewa anajibebesha mimba na akiwa ndani ya ndoa hashauriani na mumewe kwamba tuzae wangapi anaendelea tu kufyatua kama kuku tena wengine utasikia nikizaa wengi hawezi kuniacha. ndio mwisho mwanaume yanamshinda familia inakuwa kubwa sana inabidi akuachie tu 2000 atafanyaje na kipato hakiruhusu.

Na wanawake waache kujibweteka tufanye kazi tusaidiane maisha, huyo mdada ni mjinga na mvivu pia, hivi dunia ya leo kuna mwanaume anaweza kumkataza mkewe asifanye kazi kweli? huyo mwenyewe hataki kufanya kazi
 
Akome kuach kaz na chuo!eti litokee lijanaume linaniambia niache kaz,ntachukua mtwangio wa kinu nimpige nao kchwan!

Wewe kunamtu anakugusa sehemu hujawahi kuguswa utaishia kupiga mayowe na kusema yes sir kwa kila kitu atakachokufanyia
 
Dada wapo wengi wanaojali watoto wao ila usijibebeshe mimba bila sababu, maana wako wanawake wengine kabla hajaolewa anajibebesha mimba na akiwa ndani ya ndoa hashauriani na mumewe kwamba tuzae wangapi anaendelea tu kufyatua kama kuku tena wengine utasikia nikizaa wengi hawezi kuniacha. ndio mwisho mwanaume yanamshinda familia inakuwa kubwa sana inabidi akuachie tu 2000 atafanyaje na kipato hakiruhusu.

Na wanawake waache kujibweteka tufanye kazi tusaidiane maisha, huyo mdada ni mjinga na mvivu pia, hivi dunia ya leo kuna mwanaume anaweza kumkataza mkewe asifanye kazi kweli? huyo mwenyewe hataki kufanya kazi

We unaongea hivyo kwa sababu hayajakukuta wapo wanaume ambao hawataki kusikia mwanamke wake anafanya kazi(abaki home tu) halafu mwanamke huyu alikua anafanya biashara lakini kutokana na maisha yalivyokua magumu alijikuta akitumia ile hela ya biashara na faida akabaki hana kitu
 
hizo tabia kwa kweli sio nzuri...na sheria yetu ya tz haiwajali or kuwakinga akina mama na watoto from abuse...
 
mbona mnasemea huyo mama je watoto

Hao watoto unaowaonea huruma si ndio ambao wanawake huwa mnazitoa mimba kabla hawajazaliwa au na hili nalo ni geni?. Wanawake wengi kutoa mimba ni ishu ya kawaida ss hv, inakuwaje tena mjifanye mnawaonea huruma watoto wanalazwa njaa na kusahau wale mnaowauwa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom