............................ Dr.Shein hakushinda, lakini wazanzibari hawakujadili hilo akiwemo M.Seif.Kama wewe ni mzanzibari ungelifahamu vizuri maamuzi aliyofanya Seif yamelenga wapi.................................
Hapo kweli ndipo CCM imewaingiza CUF mjini tena kwa kuwavalisha sketi mchana kweupe. Subiri hoja zipelekwe bubgeni uone Zanzibar siyo nchi na uone kuwa muafaka siyo lolote au chochote zaidi ya changa la macho kwa CUF na CCM kutwaa ushindi kwa ridhaa ya CUF. Hapa nimeona kuwa CUF ni wavivu wakufikiri (msemo mtamu wa BWM). Makamu wa pili wa raisi kazi yake ni nini? Je wale mabingwa akina Mwinyi na Mkapa walikuja kufanya nini? Faida ya tamaa na usaliti ndiyo hiyo subirini muone.
Iwapo hilo mtalikataa ni lazima mvunje muungano. Itakuwa furaha ya shirazi kwani itawatawala kama wanavyotaka na mtakubali kwa mtindo huohuo. Mtaungana na Iran, kama redio Teheran inavyo kampenia kila wakati.
CCM haikushinda Zanzibar, raisi angekuwa Maalim Saifu, tamaa, uchu wa madaraka na kuvunja muungano kwa maslahi binafsi na ya wachache wao na zaidi kwa kurudisha usultani ndiyo azma ya Saifu na CUF. CCM kwa hilo sijui niwapongeze au vipi?
Mapinduzi daima ni neno zuri sana