Hivi wana CCM mumeshindwa kabisa kuendesha chaguzi zenu bila kutumia rushwa?.

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
11,450
8,243
Kutokana na kushamili kwa rushwa ndani ya ccm katika chaguzi mbalimbali za ndani ya chama hicho na nje ya chama.ninashindwa kuelewa kuwa ndani ya ccm hakuna mwanachama ambae anaweza kuchaguliwa mpaka atowe rushwa?.katika chaguzi zinazo endelea hivi sasa ndani ya ccm nimefuatwa na wanachama zaidi ya 2 ambao walikuwa na nyazifa mbalimbali kwenye ccm na wanataka kuzitetea nyazifazao kuwa niwape fedha ili wakawaweke wajumbe sawa.

Kwa vile sina uwezo wa kifedha nimejaribu kukataa lkn naona imeshindikana kwa sababu imekuwa kelo kwangu. kwani hao watu wananifuatafuata utafikili walinikopesha imebidi niwaahidi kuwatafutia.nilipo wauliza kwanini wanatafuta hela kwa ajili ya kuwaweka wajumbe sawa?.nimejibiwa kuwa mnasema kwa watumishi ndiko kuna rushwa?

Iiliopo kwa watumishi siyo rushwa ni takrima rushwa iko kwetu wanasiasa huwezi ukapata uongozi bila kutoa rushwa halafu huwezi ukasubiri siku ya kujinadi eti ndio uweze kujinadi huwezi kupata kura unatakiwa kwanza uwazungukie kwanza wajumbe wote hukohuko ili umalizanenao
 
Sasa si uache kugombea?Kuna ulazima gani kutoa rushwa wakati unajua wazi siyo sahihi na ni dhambi?
Ningekushauri uache kugombea hiyo nafasi.
 
Sasa si uache kugombea?Kuna ulazima gani kutoa rushwa wakati unajua wazi siyo sahihi na ni dhambi?
Ningekushauri uache kugombea hiyo nafasi.

Hilo swali nalo nilimuuliza mmoja wao na nikaongeza kuwa wewe ni mtu mwenye uwezo wa kuongoza na unakubalika kwa watu.la kwanza alijibu kuwa nimesha zoea kuongoza hivyo kuacha inakuwa vigumu.la pili alijibu kuwa wajumbe wanachokiangalia siyo uwezo tu au kukubalika kwa watu bila kutoa kitu kidogo unaweza ukapigwa chini pamoja na kuwa na sifa zinazotakiwa kwani wanahesabu kuwa kukupa uongozi nisawa na kukufaidisha.
 
Hayo mambo ya kumalizana kwa kificho mwisho 2015. Nguvu ya umma haiwezi kumezwa na watu wachache wanaochukua hela kwa uficho halafu wakifika majukwaani ni kuwananga wagombea wasio na kasoro na kuwapamba kwa maua wagombea wala rushwa na watoa rushwa ambao hawakubaliki na jamii miongoni mwao wakiwemo wale wabakaji na waeneza ukimwi
 
Hatutumiii rushwa bali tunakata majina kwa ushauri wa kamati ya wazee chini ya mzee mtei,umesahau tulichomfanya zitto?
 
huku kwetu rushwa ndio rangi ya chama so msishangae sana...........kama wakubwa wala wacha na sie wanyonge tule...KULA CCM , KURA CDM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom