Hivi wakenya wanatuzidi wapi jamani?

Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia haya mashindano yanayoandaliwa na kituo cha television cha CNN.kwa waandishi wa habari na watangazaji,kila mwaka.mbona watanzania cwaoni wakiibuka washindi! Kila mwaka wakenya ndio wanaochukua tuzo hizo kwa wingi!tatizo lipo wapi jamani?au ndio mambo yetu yale yale..,
Matatizo ya watanzania mengi yanasababishwa na;
kutowajibika,
kutokujituma,
kutopenda kutimiza majukumu!
kufanya mambo nusunusu!
kutojiamini,
kuhisi kuonewa!
kutotaka kuthubutu...
woga bila sababu!
 
Lugha sio quality. Ina maana wapasha habari wa russia ni wabaya wanapolinganishwa na US? unaweza kufanya kazi ya quality nzuri kwa lugha yoyote. Tatizo itakua kwenye professionalis. Watanzania wanaspecialize katika udaku. Hawatoi source, wanaongelea hisia zao hawafati facts etc. Lakini kuna wale wazuri pia na kama gazeti na vyombo vingine vya habari vitawapa nafasi kama wanavopewa wapasha habari wa kikenya basi watatoboa pia.

very well summary kuhusiana nasi watz
 
Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia haya mashindano yanayoandaliwa na kituo cha television cha CNN.kwa waandishi wa habari na watangazaji,kila mwaka.mbona watanzania cwaoni wakiibuka washindi! Kila mwaka wakenya ndio wanaochukua tuzo hizo kwa wingi!tatizo lipo wapi jamani?au ndio mambo yetu yale yale..,
Very simple,wanatuzidi kichwani.
 
Tanzania na Kenya ni kama Pwagu na Pwaguzi hakuna haja ya kujilinganisha au kujifananisha na looser mwenzako. Kenya 40% ya watu wanaishi chini ya $1 kwa siku!!. Tufikirie mbali jamani

Unajua watanzania wangapi wanaishi chini ya $1, ni wengi zaidi kuliko wakenya. Angalia wakenya wameweza kuvutia zaidi investors kuliko sisi, na angalia vilevile nani ni mwekezaji mkubwa hapa Tanzania, ni Kenya si South Africa, tembelea duka lolote hapa Tanzania utaona ni maandazi tu na chapati ndio made in Tanzania vingine vyote ni foreign made vikiongozwa na Kenya. Angalia quality ya elimu, hapo ndio utaona kuwa wakenya wako two steps ahead of us.
 
Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia haya mashindano yanayoandaliwa na kituo cha television cha CNN.kwa waandishi wa habari na watangazaji,kila mwaka.mbona watanzania cwaoni wakiibuka washindi! Kila mwaka wakenya ndio wanaochukua tuzo hizo kwa wingi!tatizo lipo wapi jamani?au ndio mambo yetu yale yale..,

Hakuna mahali ambako mother nature amepapendelea na pakawa na maendeleo (maana maendeleo huletwa na challenges). Hata kwetu Bongo mikoa yenye matatizo ya ardhi na opportunities haba nyingi zimepiga hatua zaidi ya zile ambako ardhi si tatizo au kuna opportunities nyingi.
Ukienda Mpanda unaweza kukuta ki-baa/kiduka kinaendeshwa na mchagga, umeshawahi kuona baa inayoendeshwa na mfipa Moshi? Hata wanariadha mahiri huvunja rekodi wakikabiliwa na upinzani wa kutosha (ulishawahi kusikia mtu anakimbia peke yake akavunja rekodi?)

Halikadhalika Kenya. Hakuna sehemu ya ardhi unayoweza kusimika kidole Kenya ikakosa mwenyewe. Kwa hivyo wamelazimika kuchangamka na kujiajiri wenyewe maana vinginevyo watakufa njaa (bongo nikienda hata Kilosa sikosi eka angalau moja nikajilimia). Middle class ya Kenya pia ipo more advanced (kumbuka nchi zote duniani middle class ndiyo inayokabiliwa na changamoto zaidi za maisha hadi kuzifanya serikali ziwe macho nazo). Ni middle class inayotegemea huduma za kijamii (lower class hawamudu na high class wana njia mbadala). Kwa hiyo umeme ukikatika high class anawasha jenereta, maskini haoni tofauti maana siku zote hana umeme, ni middle class ndie atakaeathirika zaidi. Kwa hiyo the more advanced the middle class is in the society the more enterprising people they become.

Ukiangalia hata Kenya walio wajanja zaidi ni kule kusikokuwa na ardhi inayopatikana kiurahisi (Central na Rift Valley) so no wonder Wakikuyu wapo hadi Tunduma wanauza baa. Jamaa zangu Mombasa (Kilifi) kuna ardhi ya waarabu ambao wenyewe hawajawahi kuitembelea siku nyingi kwa hiyo Wakilifi wanaishi kama ma-squater. Akijilimia ki-eka chake cha mihogo na akapata kipande cha papa, shida iko wapi?

My two cents: Wakenya wanakabiliwa na changamoto nyingi sana za maisha (na hawana cheap alternative) ndio maana wamechangamka kutuzidi.
 
Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia haya mashindano yanayoandaliwa na kituo cha television cha CNN.kwa waandishi wa habari na watangazaji,kila mwaka.mbona watanzania cwaoni wakiibuka washindi! Kila mwaka wakenya ndio wanaochukua tuzo hizo kwa wingi!tatizo lipo wapi jamani?au ndio mambo yetu yale yale..,
Amani, upole, unyenyekevu, ujinga, umaimuna na UMAGAMBA
 
shule ndogo, hatuna tabia ya kujisomea kujua mambo kwa upana. Tunasoma tu ili kupita mitihani na baada ya hapo vitabu vinawekwa kwenye shelf.
 
Baba wetu wa taifa JK Nyerere alifanya mambo mengi mazuri lakini aliharibu hapo kwenye lugha tu na ndpo wenzetu walpotuzd, tumuombe mungu baba wetu wa pili wa taifa hili Dr Slaa akiingia mwaka 2015 hili jambo lazma alichukulie kwa mapana yake la sivyo tutaishia kila siku kuhangaika.

Ufasaha wa lugha ya kiingereza Tanzania ulianza kupotea wakati uchumi ulipoanza kuharibika sambamba na kuporomoka kwa elimu ya msingi na sekondari. Hiyo ni kwa vile waalimu na wanafunzi walianza kujihusisha na biashara za mitaani na kuacha tabia ya kujisomea. Kutokusoma vitabu hasa vya riwaya kulichangia sana kushusha ukuaji wa vocabulary miongozi wa vijana wetu na hivyo kuwaondolea confidence ya kuongea lugha hiyo mbele za watu; halafu kufa kwa utaratibu wa debate mashuleni kukafanya watoto wasiwe hata na uwanja wa kuwalazimisha kufanya mazoezi ya lugha hiyo, ndipo ikajifia kabisa. Vitabu vya akina James Hadley Chase, Nick Carter, Agatha Christie, Denise Robins, No Longer At Ease, na vingenevyo vya aina hiyo vikawa havina soko tena Tanzania. Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya tisini tumejikuta na vijana engi sana wakiingia vyuoni huku lugha ya kiingereza ikiwagonga ile mbaya. Leo hii kuna Mawaziri wetu ambao pis lugha hiyo inawagonga vibaya sana; wakiwa kwenye mikutano ya kimataifa wanalala usingizi kwa vile hawajui linaloongelewa.

Niligundua kuwa waalimu wale wale waliofundisha kiingereza kizuri miaka kabla ya 1975, baada ya miaka kumi na tano kupita walikuwa hawatoi wanafunzi wanoongea kiingereza kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mashindano ya kuongea kiingereza kwa kupitia debate na kujaza vitabu vya hadithi fupifupi mashuleni kutasaidia sana kukuza lugha hiyo bila kusubiri waalimu wa kutoka Kenya.
 
Kiingereza ni muhimu sana katika kuchimba chimba habari pale na pale. . Kenya wapo juu sana kihabari kwa sababu bado walikuwa wana lelewa na Ronho aliyekuwa mmiliki wa Daily news(tz) na Kenya Nation.Utamaduni wa kuisomea vitabu majumbani ulikwisha toweka mara baada ya kuvunja kiingereza mashuleni. Maana vitabu vingi vya kusismua na maarifa mengi vipo kwa lugha ya kiingereza. Mwandishi wa habari anatakiwa kusoma vitabu vingi sana ili apanuke kimawazo. angalia ile filamu ya Tausi. Kenya walifikia kutengeneza filamu ile na maactors wao hawakuwa na matabasamu ya sheepesh smile! Lakini angalia sana Bishanga alipoanza kuigiza na kikundi chake miaka ya 96 utaona waactors wake wengi walikuwa wana matabasamu ya ushamba wa video.
 
Lugha inaweza kuwa kikwazo katika ngazi za kimataifa. Lakini hebu tuangalie pia katika mazingira ya kienyeji (Local News). Wakenya wametuacha mbali sana. Linganisha taarifa ya habari kutoka vituo vinavyotangaza kiswahili kati ya Kenya na TZ, taarifa za habari za Kenya utapenda kuangalia hadi mwisho. Matukio ni yale yale sawa na ya kwetu MFANO; ujambazi, mauaji, wanasiasa, dini etc lakini jinsi wao wanavyoripoti kwa ufasaha, kina na kusawiji habari hakika utafurahia.

Tatizo letu sisi ni ukilaza. Utasikia ''watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia na kuua''.......hao hawasadikiwi tayari hao ni majambazi na wauaji. Kwanini magazeti, radio na Runinga wanaripoti kama watu hao ni wahisiwa. Mfano; matukio ya ajali, mauaji au ujambazi chanzo chao cha habari ni Kamanda wa polisi, hawajishughulishi hata kutafuta upande wa pili wa stori.

Hakuna cha lugha wala nini, tatizo ni ukilaza, uoga, ushamba, kupenda dezo na kutokuwa siriasi na fani. Mfano, hivi juzi Nape na Mwiguru? wamemponda Maalim Seif, ungetegemea mwandishi wa ITV au Channel Ten anu TBC aliye ZNZ tayari kisha mhoji Maalim Seif, huko walioko Dar wamemuhoji Katibu Mkuu wa CCM, na Waziri Mkuu kuhusiana na kauli hizo.

Mfano; Magazeti, radio na Tv zote zimeripoti kuhusu barua ya David Jairo, lakini hakuna hata mmoja aliyemhoji bwana huyo kujua upande wa pili. Wala hakuna aliyeandika kuhusu Mh.Pinda kusema alitaka kumfukuza kazi Bwana Jairo, lakini ''watu'' wakamwambia mzee unaingilia anga za President. Kwangu mimi habari ingekuwa PM hakujua mipaka yake ya kazi...................................angalau kwa wakati wa tukio hilo.
 
Back
Top Bottom