kiongozi,
sina uhakika na efficiency ya hizi solutions 2. Labda nieleze ninavyoona.
Unajua watu tunapoketi kujibizana na akina barubaru na kundi lake, na hoja zao, ni wakati huohuo tunapoteza makali ya jf ya kukata ishu. Kukata ishu kwetu ndiko kulikoi-define jf na mpaka serikalini inafahamika hivyo. Tukiendelea na hizi petty discussions za hawa ndugu ni jambo zuri, lakini ndivyo hivyohivyo tuna-divert efforts from main issues. Issues ambazo zinatujenga na zipo dynamic kuelekea mabadiliko.
mkuu unajua watu wote humu ndani ya jamvi hawafanani kifikra. Na kitendo cha kutoa nafasi kwa yeyote anayependa kujiunga irrespective of fikra zake ndiyo kumeleta mgongano. Kwani baadhi wanapotoa mawazo yao yanayoenda kinyume na mawazo ya wengine then inakuwa kasheshe. Nafikiri tuvumiliane na kueleweshana kama tukipelekana kijeshi wengi tutawaacha njiani. Nawakilisha.