hivi wajua NYANYA na VIAZI ni SUMU?(chips)

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
1,488
908
JE WAJUA.??? NYANYA NA VIAZI
Leo nikiwa Kwenye maktaba ya Nyumbani nikawa najaribu kuchimba kujua asili ya baadhi ya viungo vya vyakula vyetu Kama nyanya, vitunguu, biringanya, hoho Na vinginevyo manake sijawahi kuvisoma kwenye Historia ya kawaida kuhusu asili ya mazao hayo

Nikagundua Nyanya ni kijizao tu ambacho juzijuzi miaka ya 1650 ndipo kimeanza kutumika Kama chakula, Na mwaka 1696 ndipo Kitabu Cha kwanza cha mapishi Kwa kutumia nyanya kilipovumbuliwa, lakini zao Hili lilivumbuliwa tokea miaka 500 kabla ya KRISTO Na wanajimu wa Uganga. Nyanya ikawa inatumika Kwenye makafara Na matambiko(divination) wakiamini ukila nyanya ni Kama umekula Damu inakutia nguvu Za kiroho kuwasiliana Na miungu.. So those time nyanya ilipandwa Kwa nasibu Na waganga wachache sana Kama zao mbadala la Damu. Mtu wa kawaida huwezi hata kuiona nyanya licha ya kuila,

mtabibu Wa madawa ya mimea huko Ulaya Dr Pietro Andrea, akagundua nyanya Ina uwezo wa kutibu baadhi ya magonjwa Kama Athma ambayo ilikuwa tatizo Ulaya kutokana Na msongano Wa Makazi ya watu Na mabadilishano ya Hewa.

Taratibu nyanya ikapata kupenya Na kuanza kulimwa Na mwanzoni watu waliitumia Kama protective food Kwa magonjwa ya hewa Kama kukohoa, Athma Na MENGINEYO Na hatimae kizazi kilichofuata wakarithi mapishi hadi Leo hii twala tu..

Athari kubwa ya NYANYA Na VIAZI ni uwepo Wa sumu inayoitwa SOLANINE[C15H73NO15] ambayo ni hatari Kwa mwanadamu.. Sumu hiyo ambayo hutengenezwa Na mimea hiyo hufanya ulinzi juu ya mashambulizi ya wadudu Na wanyama wasiokula majani.. Labda kitu Cha kujiuliza kwanini predators Kama simba,mbwa nk hawali mbogamboga, ni Kwa sababu ya uwepo Wa sumu harufu kama solanine ambayo kwao ni Kama mwanadam kunusa kinyesi..sumu hiyo ambayo hupatikana Kwa wingi Kwenye nyanya Na VIAZI huleta madhara Kwa mwanadamu.

Solanine wataalam hawa wanasema inaua seli Za mwili, Na dalili zake Kuu ni kichefuchefu, kuumwa tumbo au kichwa, kukosa ham au ladha ya chakula, kuharisha, matatizo ya Uzazi (kushindwa kujifungua Kwa njia ya kawaida), unene, uchovu, kulala Na hatimae KANSA..

Mabandiko yanasema Kwenye seli ya mwanadam kuna chambehai inayoitwa mitochondria, chembehai hii ndio mlinzi mkuu wa seli, ndio itoayo kemikali Za kuikuza seli na ndio nguvu ya uwepo wa seli Za wanadamu, Wanasema mwili hutoa kemikali kupambana Na magonjwa, Sasa kemikali hizi huzalishwa Na mitochondria. Wanasema Sumu ya Solanine huingia kwenye wajenzi Wa kemikali Kwenye mitochondria ambao ni potassium potential Na kuhamisha Ca2+ kuwa Maji Kwenye process inayoitwa opoptosis Na kuangamiza seli yote.. Kimsingi Kwa makuzi ya binaadam opoptosis process huua seli Kati ya billioni 30-70 Kwa siku Kwa watu wazima ilihali opoptosis Kwa Watoto 8-14 years huua seli billioni 20 kwa siku. Sasa Solanine huongeza maangamizi ya seli Kwa opoptosis Na Kufanya baadhi ya tishu Kufa Na kuzua sehemu ya mwili kupoteza uhai(Kansa).

Kansa inapotibiwa Kwa mionzi (irradiation) huua seli Ilizoathirika ili kujaribu kusimamisha zoezi la opoptosis.

Kwa maana hiyo ulaji sana wa nyanya Na VIAZI hasa Kwenye michips yenu hiyo angalia sana.. Watu wa vijijini hula fresh food, ni nadra sana kupata magonjwa hasa matatizo ya kujifungua au kansa.. Watu wa mijini hutumia sana nyanya Kwenye takriban milo yote Na VIAZI ..

Ushauri wangu Adui number moja wa Mtu ni msosi.. FUNGA..!!
 
Familia yote ya nyanya, including ndulele inaitwa Solanaceae na ina hiyo solanaie, inatofautiana kwa kiasi tu (uwingi). Aliyegundua nyanya kuwa yaweza kuliwa bila kuua, alitaka kucommit suicide so akala nyanya za kutosha tu lkn hakidhurika badala yake akawa mvumbuzi.

Source: Mwalimu wangu!
 
Kimsingi vyakula vyote ni sumu, ila miili yetu ina uwezo Mkubwa wa kuondoa most of the poisons zisitudhuru! Mkuu ebu jaribu kusoma na vyakula vingine kama vile nyama nk. Utajikuta umebaki bila choice ya chakula gani ule! kwanza kuishi tu duniani upo kwenye sumu za mionzi kutoka outer space na zingine tunazitengeneza wenyewe!
 
Paracelsus, an influential German scientist, noted that "All things are poisons and nothing is without poison, only the dose permits something not to be poisonous"
 
Mkuu sasa naona tunaanza kutishana hadi utajikuta unaowatisha wanakufa kwa pressure kabla ya kile ulichowatishia kinawaua..Kila kitu in large doses ni kibaya mfano hata ukinywa pipa la maji daily hakika utakufa.., katika kuangaza kwangu nimeona kwamba hii solanine inakuwa poorly absorbed na quickly excreted angalia following extract... http://www.sciencebasedmedicine.org/index.php/killer-tomatoes-and-poisonous-potatoes/Solanine

Solanine is indeed a poison in large doses, causing everything from gastrointestinal symptoms to hallucinations, paralysis and death. Large amounts are toxic, but the amounts usually found in food are innocuous.

It is poorly absorbed and rapidly excreted. It is estimated that it would take 2–5mg per kilogram of body weight to produce toxic symptoms. A large potato weighs about 300g and has a solanine content of less than 0.2mg/gm That works out to around 0.03mg per kilogram for an adult, a hundredth of the toxic dose; I figure a murderous wife would have to feed something like 67 large potatoes to her husband in a single meal to poison him. Unless he’s a phenomenally big eater, arsenic would be a better bet.

Potatoes that are diseased with blight or that have sprouted have a larger than usual amount of solanine. They will have a bitter taste and often a green discoloration; such potatoes should be avoided. Even integrative health guru Andrew Weil is not afraid of solanine, pointing out that there hasn’t been a single case of solanine poisoning in the US from eating potatoes in the last 50 years.

Kwahio conclusively naweza kusema tuendelee kula nyanya na viazi kama kawa unless kama vimeharibika
 
Hata madawa tunayokunywa ni sumu mbaya kabisa, lakini ukiugua unapewa unywe. Pombe ni sumu lakini ukitaka kuburudisha mwili unainywa.Niliwahi pia kuambiwa maziwa ni miongoni mwa vimiminika vyenye sumu chaajabu ukinywa sumu unaambiwa unywe maziwa kuipooza.
 
Mimi sikulijuwa hili kwa hakika.
Ngoja niendelee kufanya utafiti. Maana nyanya ambazo nimeshakula mpaka sasa, sihitaji kujuwa zimeathiri seli zangu kwa kiasi gani. Itakuwa kutiana presha tu!
 
mbona tunaambiwa kuwa nyanya zinapunguza uezekano wa kupata kansa ya korodani!!:thinking:
 
hata uki-google tu kujua benefits or advantages and disadvantages of eating tomatoes utapata faida nyiingi hata kuliko hasara, mimi bado naamini haina tatizo naendelea kukong'oli tu....
 
Ni kweli uwepo wa solanine huzuia wanyama wala nyama(carnivorous) kula vegetables(including nyanya)?Vipi kuhusu their dental formula,inaruhusu kula vegetables?
 
Nimeagiza hapa nyama choma na KachUmbari pembeni,ngoja nisitishe hiyo kachumbari nikitafakari kwanza
 
Back
Top Bottom