Hivi waandishi wa habari wa Nchi ii hawawezi kususia kutoa habari za upande kandamizi

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Feb 11, 2012
1,389
285
Wanabodi,baada ya Waziri mkuu kusema serikali itaendelea kutumia sheria iliyopo ya habari bila kufanyia mabadiliko,sasa naomba kuuliza je wanahabari hawawezi kushinikiza kwa kususia kuandika habari za upande kandamizi? Eg.kususia Daily news,uhuru,habari leo,na mengine yafananayo.
 
Usifanye utani na njaa ndugu yangu. Yani wakiambiana mbinu hii ndiyo umewatangazia deal watoe zaidi na dau kuongezeka pia.
 
inawezekana wakiamua. ifike hatua kuburuzwa kukome tanzania. viongozi wa serikali yetu wanajifanya Mungu-watu. lakini ipo siku watajua mbivu na mbichi.
 
[h=2]Pinda: Mwanahalisi likate rufaa[/h]


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amemtaka mtu yoyote asiyeridhika na uamuzi wa kulifungia gazeti la MwanaHalisi kukata rufaa katika vyombo vinavyohusika.

Alitoa wito huo jana wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo bungeni jana.

Mbowe alisema Julai 30, mwaka huu, serikali ililifungia gazeti la MwanaHalisi kwa muda usiojulikana kwa kutumia sheria ya magazeti ya mwaka 1976. Alihoji maadam katika siku za hivi karibuni serikali imetambua umuhimu wa Mahakama ni kwanini imelifungia gazeti hilo badala ya kulipeleka mahakamani na wahusika wapate nafasi ya kujitetea kabla ya hukumiwa?

Akijibu swali hilo, Pinda alisema ni kweli Serikali imechukua hatua hiyo, lakini imechukua hatua hiyo kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Alisema mtu yoyote kwa msingi wa sheria hiyo anayeona hajatendelewa haki ni juu yake kukata rufaa kwa kuzingatia taratibu zilizopo. "Mimi nadhani ushauri mzuri ungekuwa ni huo," alisema Pinda.

Katika swali lake la nyongeza, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema sheria iliyotumika imekuwa ikilalamikiwa na wadau wengi na vyombo vya habari kwa muda mrefu ambayo inaipa mamlaka ya ziada serikali kuyadhibiti bila ya kuyasikiliza magazeti.

Alihoji iwapo Pinda haamini kwa kutumia sheria hiyo ni kunyima haki na ni msisitizo wa utawala usio bora?

Akijibu Pinda alisema: " Mimi siamini hivyo kwa sababu sheria hiyo imetungwa na Bunge na kwa kuwa bado inatumia ni sheria halali, sisi tutaendelea kuitumia mpaka hapo itakapokuwa imerekebishwa."


CHANZO: NIPASHE

Serikali ndio iliyofungia inaulizwa kwa nini badala ya kueleza kwa nini wamefungia wao wanasema nendeni mahakamani, kwa tone hii sidhani kama mwanahalisi watapata haki hata kama wakienda.

Wakate rufaa katika mahakama gani Tanzania? Ni bora waende mahakama ya Afrika, Hii statement ni ya kibabe kwelikweli ambayo inaonesha dhamira ya dhati ya serikali ya kuzima njia za mawasiliano.


 
Back
Top Bottom