Hivi vyuo vikuu vyetu vinaboreka au vinaboronga tuu

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,639
516
Hivi wana JF tuulizana hivyi vyuo vikuu vetu kama UDSM, UDOM, MZUMBE na vingine vyote vinaendelea katika utafiti au katika kuboronga? Kwani mwisho wake havitakuwa na maana. Je nini kifanyike kuviboresha?
 
Ni serikali kuu ktenga pesa za kufanyia utafiti kwa kila idara na sio kutegemea wafadhali ambao wao kule makwao ndio wanapata misukosuko ya matetemeko makubwa sana na kupunguza ,misaada yao kwetu.. Kwa kuwa serikali haina mpango wa kutenga bajeti katika utafiti ndio inaleta shida sana leo hata bajeti zao. Tazama UDSM wakiomba bajeti na kiwango chao wanachopewa ni kidogo sana ilinganishwa na maudhui yake
 
Peleka mada yako kwenye jukwaa la elimu......hakuna uhusiano wa our university na siasa......................
 
only83

Usikiri siasa na kuandaa maandamano, kupiga kampeni na kumjadili Dr. Slaa na Kikwete. Siasa ni zaidi ya hapo. Elimu, Uchumi na vitengo vingi vinavyogusa maisha ya kila siku haviwezi kutenganishwa na siasa. Kwa hiyo elimu ni msingi mkuu katika maisha; na kuboronga au kuboreka kwake ni lazima kuhusishwe na siasa za nchi husika. Hope umenipata.
 
Back
Top Bottom