Hivi viongozi wa Tanzania wana 'Job Description' kwenye kazi zao?

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
Heshima kwenu wanajamvi,

Naomba kupata ufafanuzi kama viongozi wa ngazi za juu katika serikali ya Tanzania hususan Rais na Makamu wake, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Watendaji wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Makatibu watendaji wao na wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi wanapewa 'job description' wanapoanza kazi zao au kuapishwa?

Hili linanitatiza hasa kwa kuwa mara kadhaa kumetokea kauli tata, au maamuzi tata yanayosababisha wananchi tujiulize, nani anapaswa kufanya nini au kusema nini katika suala hili.

Mfano dhahiri wa hivi karibuni ni Edward Lowassa (Mbunge) kusema Tanzania iko tayari kuingia vitani na Malawi. Yeye anasema hivyo kama nani? Ni kazi ya mbunge kutoa taarifa kama hiyo, ama kwa kuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu pengine bado anayo ruhusa kutoa hadharani matamko ya serikali au jeshi, ndiyo 'job description' ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu?

Pili nani anawapa mamlaka wake wa viongozi wakuu kuwa wasemaji au wataalamu wa kuwafundisha na kuwakemea watendaji wa serikali? Nimeona mara nyingi wake wa viongozi wanawapa 'semina' waandishi wa habari, maofisa wa kilimo, wataalamu wa uvuvi n.k. Hivi ukishakuwa mke/mume wa kiongozi serikalini basi ghafla unakuwa mtaalamu hata kama hiyo siyo fani yako? Ama ndio 'job description' ya mke wa kiongozi?

Naomba radhi kama kuna watakaokwazika kwa hili, lakini nafikiri kazi ya mke au mume ni kutoa ushauri kwa mwenzi wake wa ndoa na kumpa msaada wa mawazo wanapokuwa faragha. Kujileta mbele ya kadamnasi na kutoa somo kwa wataalamu wakati hiyo si fani yake ni kuvuka mipaka. Tafadhali kwa wale watakaoshiriki kwenye mchakato wa katiba kama hili jambo halijawekwa bayana naomba lifikiriwe kwa undani zaidi. Tujue mipaka ya viongozi ni ipi na wenza wao mipaka yao ni ipi. Sivyo tunajikanganya!
 
majini na mashetani kisiwe kigezo cha kumsaidia mtu kuongoza nchi matokeo yake wote tumeyaona umefika wakati tumuweke mungu mbele kuongoza nchi hii kama marais watatu waliotangulia walikuwa wacha mungu.
 
Back
Top Bottom